nyampanaga
JF-Expert Member
- Nov 16, 2012
- 1,104
- 559
Wakuu wa Fikra,
Jana majira ya jioni kulitokea mapigano makali kwenye mgodi wa Almas wa Mwadui, Shinyanga kati ya Polisi na wachimbaji haramu maarufu kwa jina la WABESHI ambao walivamia eneo la mgodi huo nakuanza kuchimba mchanga wa madini kwa nguvu.
Katika kadhia hiyo askari polisi mmoja alipigwa na kitu kizito kilichorushwa na Wabeshi kwa kutumia Kombeo na kuzimia na amelazwa katika hospitali ya mgodi huo.Polisi walilazimika kuongeza nguvu kutoka mkoani, na wilayani Kishapu.
Mapambano yaliendelea mpaka saa 6 usiku na kupelekea wabeshi wapatao 10 kutiwa nguvuni na mmoja kati yao amelazwa katika hospitali ya mgodi huo baada ya Polisi nao kumpiga kwa vitu vizito mara walipomtia nguvuni.
Source: Kaka yangu ambaye ni Mwalimu pale Mwadui A Primary School