Polisi: Marehemu Ally Zona aligongwa na kitu kizito na sio Risasi

madibira1

Member
Dec 18, 2011
80
16
Nimeona katika Channel Ten polisi wametoa ripoti kwamba marehemu Ally aliyeuawa katika maandamano ya Chadema Morogoro amefariki kutokana na kugongwa na kitu kizito sio risasi, hiyo ni baada ya uchunguzi wa madaktari.

Alhamisi, Agosti 30, 2012 05:12 Na Merina Robert, Morogoro

BAADA ya kufanyika kwa uchunguzi wa kitabibu kuhusu kifo cha mfuasi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Ally Zona, matokeo ya madaktari yamebaini jeraha lililosababisha kifo chake limetokana na kugongwa na kitu kizito na si risasi kama ilivyokuwa inadaiwa.

Tukio hilo lilitokea Agosti 27, mwaka huu mjini Morogoro, wakati polisi wakitawanya maandamano ya wanachama wa chama hicho wakitokea eneo la Msamvu Lupila kuelekea Viwanja vya Fire kulikofanyika mkutano huo ambapo awali yalikatazwa na jeshi hilo.

Akieleza matokeo ya uchunguzi huo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Morogoro, Faustine Shilogile, alisema jeraha hilo la marehemu lililokuwa kichwani lilitokana na kugongwa na kitu kizito kilichorushwa na si risasi kama ambavyo watu walikuwa wakidhani.

Alisema uchunguzi huo ulifanywa na madaktari wawili wa mkoani hapa pamoja na Dk. Ahmed Makata kutoka Dar es Salaam na kushuhudiwa na mwanasheria wa CHADEMA, Amani Mwaipaja, pamoja na baadhi ya askari wa Jeshi la Polisi.

Alisema baada ya matokeo hayo ya daktari, polisi sasa wanaendelea na uchunguzi wa kubaini kitu hicho kilichorushwa na kusababisha kifo cha mfuasi huyo.

Alisema baadaye watachukua hatua za kisheria kwa askari ama mtu mwingine atakayebainika kuhusika kurusha kitu hicho, ikiwa ni pamoja na kumkamata mtu ama kiongozi wa chama hicho aliyechochea ama kuandaa maandamano hayo yaliyozua vurugu.

Alisema katika kubaini mwenendo mzima wa tukio hilo, Serikali imeunda tume ya kuchunguza ambayo inahusisha askari polisi na watu wengine watakaosaidia kukamilisha uchunguzi huo.

Hata hivyo, alisema tume hiyo ambayo tayari imeshafika mkoani hapa, itatafuta maelezo na ushahidi kutoka kwa watu mbalimbali walioshuhudia tukio hilo, wakiwamo wanahabari na kuwaomba wote watakaohitajika kutoa ushirikiano.

Akielezea kuhusu majeruhi, Hashimu Seiph, aliyejeruhiwa mguu katika vurugu hizo, alisema uchunguzi umebaini kuwa alijeruhiwa na bomu lililomuangukia mguuni na anaendelea vizuri na bado yuko Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kwa ajili ya matibabu zaidi.

Kwa upande wake, Mwanasheria wa CHADEMA, Aman Mwaipaja, ulikiri kupokea taarifa ya matokeo ya uchunguzi wa madaktari hao na kusema wanafanya mawasiliano na viongozi wakuu wa chama hicho kuona hatua gani zitachukuliwa.

Alisema kwa sasa anafanya mawasiliano na Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa, aweze kumpatia taarifa hiyo na hatua zozote zitakazochukuliwa zitatolewa taarifa kwa vyombo vya habari.

Alisema mwili wa marehemu huyo unatarajia kusafirishwa baada ya familia kukaa na kupanga siku ya mazishi mkoani Tanga na mazishi hayo yatahudhuriwa na baadhi ya viongozi wa CHADEMA mkoani Tanga na wengine.
 
ni ngumu sana kumkabidhi fisi bucha au zizi la mbuzi hatutaweza kupata suluhu hadi tume huru ya mahakama
 
Hili ni picha la kihindi hivi na wale majeluhi na wenyewe wapondwa na vyuma vizito? Nauliza mwenye habari zao atuhabalishe.
 
Ukweli anao mungu. Mungu hafichi kitu. Ipo siku itajulikana tu. Ee mola mrehem ally mpumzishe kwa aman. Damu yake imetumika na uonyeshe ukweli kwa kutumia damu yake. Amin.
 
Aahhh hawana jipya kama tume imeundwa na IGP kwa nini RPC anashupalia kutoa tamko??si angesubiri uchunguzi wa tume??
 
Mtu utarajie majibu gani kama unanituhumu kwa mauaji na mimi nichunguze mazingira ya kifo na thn nitoe taarifa mimi..." kabisa haiingii akilini...hatungeshangaa hata kma wangesema kafa kwa ajari ya basi!
 
Kweli siku hizi Binadamu kawa kama kuku anakufa watu wanakuja na majibu ya uongo anazikwa na kusaulika........Nasikitika sana
 
ahaa...kwahiyo nani kaua sasa...hii nchi kuna watu wanafikiri watanzania ni kama viongozi wa ccm....sisi akili zinafanya kazi hatupelekwi kama ng'ombe na tunajua nin kimetokea kwa hiyo hatudanganyiki...
 
Nimeona katika Channel Ten polisi wametoa ripoti kwamba marehemu Ally aliyeuawa katika maandamano ya Chadema Morogoro amefariki kutokana na kugongwa na kitu kizito sio risasi, hiyo ni baada ya uchunguzi wa madaktari

are u serious? Ngoja tusubiri kama kuna mwingine kaangalia hio taarifa, kama ni kweli basi kuna haja ya kukapindua haka kaserikali legelege
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom