Kundi la wachimbaji wadogo lavamia geti kuu la mgodi wa Mwadui na kufanya uharibifu

nyampanaga

JF-Expert Member
Nov 16, 2012
1,104
559
Wakuu wa Fikra'

Habari zilizonifikia hivi punde ni kwamba, majira ya saa 9 mchana jana, kundi la wachimbaji wadogo maarufu kama WABESHI wapatao 80 wakiwa na silaha za mbalimbali za jadi kama manati,kombeo, sululu, mapanga, nondo na mawe, walivamia lango kuu la kuingilia mgodini hapo na kusababisha walinzi waliokuwepo kutimua mbio ili kunusuru maisha yao

Wavamizi hao walikuwa wakieleza wazi kuwa wanataka kulipiza kisasi kwa askari wa mgodi huo kwa madai kama yaliyovyoripotiwa na vyombo mbalimbali juma lililopita kuwa mchimbaji (mbeshi)mmoja alipigwa risasi na walinzi wa mgodi huo na kuvunjika mguu.

Mara baada ya walinzi wa geti kukimbia, wavamizi hao waliamua kufanya uharibifu kwakuvunja madirisha na samani kadhaa zilizomo ndani ya jengo la ofisi ya ulinzi getini hapo na kutoweka.Uhusiano kati ya wafanyakazi wa mgodi huo hasa walinzi na wakazi wa vijiji vinavyozunguka eneo la mgodi umezidi kuzorota na juzi mtu mmoja alipigwa na wananchi wanaosadikiwa kuwa wakazi wa kijijini Maganzo kiasi cha kupoteza fahamu alipokuwa akitokea kijijini hapo akifuata barabara inayoenda mgodini na hivyo kushukiwa kuwa ni mfanyakazi wa mgodini.

Kama inavyoelekea kuzoeleka sasa, chama cha demokrasia na maendeleo kimenyooshewa vidole juu ya hali hiyo kwani diwani wa kata ya Mwadui Mh. Magembe anayetokana na chama hicho amekuwa akihisiwa kuchochea kutokana na kuw akaribu sana na vijana wengi japo kuwa naye ni kijana tu.

Source: Jamaa yangu anayefundisha pale Mwadui A Primary School.
 
Huu sasa upu.mbavu kila kitu cdm hivi anayeshika dola ni nani?CCM si wasarende inchi kwa CDM kama ndo hivi?
 
Back
Top Bottom