Polisi aliyekataa hongo ya Mil.10 na kupanda cheo, akataa zingine 250,000

Ipo siku sifa zitamtokea puani...mi Kuna mwamba nakumbuka nlimpaga sh 800 na akaniachia kisa pikipiki bima imeisha muda....yle mwamba aishi miaka 10000...ana njaa na hela balaa
Kuna siku watamuhonga Hakimu akufunge ndio utapojua vizuri faida za rushwa.
 
Kiki tu Zakipumbavu sasa 250k mbona hela ndogo ukiwa police na Elimu ya lasaba au form four zero unakuwa boya.
 
Taasisi ya kuzuia na kupambana na Rushwa Takukuru mkoa wa Arusha,inawashikiria watu watatu wanaodaiwa kutaka kumhonga Askari polisi , Staff Sajenti,Meshack Laizer kiasi cha sh,250,000 ili kuwasaidia kesi inayowakabili ya kukutwa na pombe haramu ya gongo.

Maafisa wa takukuru waliwatia mbaroni watuhumiwa hao wakati wakijiandaa kutoa fedha hizo katika bar ya city garden iliyopo Sanawari Mataa,jijini Arusha walipokuwa wamekubaliana kukutana na askari huyo.

Inadaiwa kuwa Meshack alikutana na watuhumiwa hao na baadaye walimweleza nia yao ya kumpatia kiasi hicho cha fedha ili kuwasaidia kulimaliza suala la ndugu yao ili kuepuka kufikishwa mahakamani.

Watuhumiwa walikamatwa Jana,Julai 3,2020 majira ya mchana wakiwa na fedha mezani wakijiandaa kumkabidhi askari huyo ili asiwafikishe mahakamani kwa kosa la kuuza Pombe haramu ya Gongo.

"Walitaka kunihonga iliniachane nakesi inayomkabili ya kukamatwa na Gongo"

Watuhumiwa wanaoshikiliwa ni Fotunata RAPHAEL aliyekabiliwa na kesi ya Gongo, RAPHAEL MOLLEL na Frank Julias ndio waliokamatwa wakijaribu kumhonga askari huyo.

Meshack aliwahi kupanda cheo kuwa Staff Sanjenti ,baada kudaiwa kukataa hongo ya shilingi milioni 10 kutoka kwa kampuni moja ya kuuza mafuta jijini hapa baada ya kuwakamata wakiuza mafuta mtaañi kinyume cha sheria ambapo kesi hiyo bado ipo mahakamani.

,....View attachment 1497392
Kiki ni kiki
 
Jamani eee mi sipokei rushwa ,acheni sheria ichukue mkondo wke,inatosha mpaka kwendaaa baaaaa
 
Kwahyo Tanzania nzima police ni yeye tu? au yeye ndy mtiifu kuliko wote?
Kutokuwa polisi mwenyewe kunamfanya akikutana na wavunja sheria asiwatangaze?

Ujengaji hoja wako sio mzuri. Acha nyeupe iwe nyeupe nyeusi iwe nyeusi.

Kwa hiyo kwako...kwasababu sio polisi mwenyewe na sio polisi mwenyewe anayekamata wahalifu basi ameikosa haki ya kuwakamata watoa rushwa.

Hapana.
 
Kutokuwa polisi mwenyewe kunamfanya akikutana na wavunja sheria asiwatangaze?

Ujengaji hoja wako sio mzuri. Acha nyeupe iwe nyeupe nyeusi iwe nyeusi.

Kwa hiyo kwako...kwasababu sio polisi mwenyewe na sio polisi mwenyewe anayekamata wahalifu basi ameikosa haki ya kuwakamata watoa rushwa.

Hapana.
Hivi hizo sifa anazozipata akifa masikini atawaambiya nini watoto wake?kuna kipindi watu husaidiana ili na wao wasaidiwe,,,ili maisha yaende,,,hivi atajifikiriaje amekataa milioni kumi ,,,halafu pesa hizi hizo wanapewa wenzie? yeye kabaki na cheo chake ,,,wenzie wanapaua nyumba zao...yeye kabaki na magwanda,,,huyo ni mkuda tu,,tena wapo wengi sana police kama hao,,wanashindwa kukusaidia kwa kingi ,,anakupeleka sehemu unatoka kwa kidogo....hiko cheo chake kitawasaidia nini watoto wake?zaidi ya sifa tu?kama mnakamata watu kwa rushwa mbona hamuwahoji police wenu wenye magari na mijumba ya thamani? Wamepata vipi?na sidhani kama wenzie wana furaha nae...
 
Hivi na sisi wanaotuita raia, tukiamua tufanye hivyo ....je watabaki? Nakumbuka kipindi fulani huko nyuma ilikuwa ngumu. Unaenda iliyoitwa PCB kutoa taarifa kisha ukitoka inapigwa call..." tunakuja na hela ya moto"....
Kama sasa ni wasafi basi na sisi raia tuanze kuwakamatisha
 
Back
Top Bottom