Police: CP Paul A. Chagonja hafai kuwa Msemaji Katika Matukio Makubwa.

Bado Kidogo 2015

JF-Expert Member
May 24, 2012
207
78
Kamishna wa Operation na Mafunzo Paul A. Chagonja ukweli hafai kupewa jukumu kubwa la kusemea Jeshi la Polisi katika matukio makubwa yoyote hasa ya kisiasa kwa sababu zifuatazo;

1.0 Ana jazba kubwa sana katika kuelezea mambo, kama anawaowaeleza hawana uelewa wa kuelewa chochote au ni kama watoto wa shule ya msingi wanaofundishwa masomo ya sekondari na hivyo ni vigumu kwao kuelewa.

2.0 Anaonyesha mapenzi ya wazi kabisa kwa chama tawala, wakati itikadi yeye hatakiwi kuonyesha yupo upande gani. Kazi hiyo angewaachia akina PM Pinda ambaye akizidiwa analia!

3.0 Hana mpangilio mzuri katika kueleza mambo, ni kama haeleweki.

Kwa sababu hizo na nyinginezo kama usafi wake machoni pa watu unatilisha mashaka nawashauri kabisa Jeshi la Polisi kuacha kuendelea kumtumua mtu huyu katika matukio makubwa hasa ya kisiasa maana anawapaka matope kuliko inavyodhaniwa.
 
Changoja ana matatizo sana;

Je uchunguzi hauwezi kufanyika bila viongozi wa CDM ?
 
Nimemwona ITV ni kama vile amenywea sana kawa mpole na kama vile hajiamini

Naona kaambiwa waandishi wa habari siyo mahabusu au unaongea nao kama unaamrisha parade, kapoa sana hata alichoongea kuhusu Mbowe sijakielewa zaidi ya kusikia viongozi wanafiki.
 
Yani hapa ni kuvurugana tuu haijulikani mkweli nani

"To know the enemy is half the victory"
 
Huyu ni kutoka ukoo wa panya buku 7 anatumiwa kuja kumwaga pumba zao hapa jamvini. Si ajabu ana IDs hata 30 katika kuandika upumbavu wake hapa akishirikiana na wapumbavu wenzake wa magamba.

Duh, mkuu unatisha, juzi tu una post zote hizi!
Join Date : 5th June 2013
Posts : 365
Rep Power : 376
Likes Received12
Likes Given0
 
Baada ya mlipuko wa bomu katika Mkutano wa kufunga Kampeni za Udiwani za CHADEMA mnamo tarehe 15/6/2013, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema aliunda timu ya Makachero wazoefu kwenda Arusha kuongeza nguvu na kufanya upelelezi juu ya tukio hilo ili wahusika watiwe nguvuni na hatimaye Sheria ichukue mkondo wake.

Kati ya Makachero hao toka Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam ni Kamishna wa Polisi Paul Chagonja. Kamanda Chagonja ni Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Tanzania.Ni Kachero mzoefu na mbobezi. Chagonja kama Kachero ni wa kumuamini sana.Lakini,tangu afike Arusha,Chagonja ameacha kilichompeleka huko. Sina uhakika kama kweli ameshaanza upelelezi uliompeleka Arusha. Sasa amemezwa na tukio la Soweto la kukamatwa Wabunge na wafuasi wengine wa CHADEMA.

Chagonja amekuwa ndiye msemaji wa kila kitu kitokeacho Arusha kwa sasa. Yupo 'bize' na vyombo vya habari-vya ndani na vya kimataifa.Amewapoka madaraka ya kufanya ayafanyayo sasa RPC wa Arusha Liberatus Sabas na Msemaji wa Polisi Tanzania, Advera Senso. Nilipokuwa Arusha,tuiikutana naye Hoteli ya Kibo Palace.Tukajaribu kumkumbusha kilichompeleka Arusha.

Akionekana kutuelewa, akacheka na kusema 'najua,lakiniPolisi tuna zaidi ya hayo'. Si vyema Kamanda Chagonja kumezwa na hali ya kisiasa iliyopo Arusha na kusahau kilichompeleka.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.
 
Kamishna wa Operation na Mafunzo Paul A. Chagonja ukweli hafai kupewa jukumu kubwa la kusemea Jeshi la Polisi katika matukio makubwa yoyote hasa ya kisiasa kwa sababu zifuatazo;

1.0 Ana jazba kubwa sana katika kuelezea mambo, kama anawaowaeleza hawana uelewa wa kuelewa chochote au ni kama watoto wa shule ya msingi wanaofundishwa masomo ya sekondari na hivyo ni vigumu kwao kuelewa.

2.0 Anaonyesha mapenzi ya wazi kabisa kwa chama tawala, wakati itikadi yeye hatakiwi kuonyesha yupo upande gani. Kazi hiyo angewaachia akina PM Pinda ambaye akizidiwa analia!

3.0 Hana mpangilio mzuri katika kueleza mambo, ni kama haeleweki.

Kwa sababu hizo na nyinginezo kama usafi wake machoni pa watu unatilisha mashaka nawashauri kabisa Jeshi la Polisi kuacha kuendelea kumtumua mtu huyu katika matukio makubwa hasa ya kisiasa maana anawapaka matope kuliko inavyodhaniwa.

mkuu haeleweki kwasababu ujanja wa kiintelijensia umeshawaishia kwa tukio hili , wameshabanwa kotekote.
 
Tupatupa unanipaga raha sana post zako mkuu. Kweli kabisa jamaa kajigeuza unga wa ngano kila kitu yeye.
 
Baada ya mlipuko wa bomu katika Mkutano wa kufunga Kampeni za Udiwani za CHADEMA mnamo tarehe 15/6/2013, Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini, IGP Said Mwema aliunda timu ya Makachero wazoefu kwenda Arusha kuongeza nguvu na kufanya upelelezi juu ya tukio hilo ili wahusika watiwe nguvuni na hatimaye Sheria ichukue mkondo wake.

Kati ya Makachero hao toka Makao Makuu ya Polisi Dar es Salaam ni Kamishna wa Polisi Paul Chagonja. Kamanda Chagonja ni Mkuu wa Operesheni wa Jeshi la Polisi Tanzania.Ni Kachero mzoefu na mbobezi. Chagonja kama Kachero ni wa kumuamini sana.Lakini,tangu afike Arusha,Chagonja ameacha kilichompeleka huko. Sina uhakika kama kweli ameshaanza upelelezi uliompeleka Arusha. Sasa amemezwa na tukio la Soweto la kukamatwa Wabunge na wafuasi wengine wa CHADEMA.

Chagonja amekuwa ndiye msemaji wa kila kitu kitokeacho Arusha kwa sasa. Yupo 'bize' na vyombo vya habari-vya ndani na vya kimataifa.Amewapoka madaraka ya kufanya ayafanyayo sasa RPC wa Arusha Liberatus Sabas na Msemaji wa Polisi Tanzania, Advera Senso. Nilipokuwa Arusha,tuiikutana naye Hoteli ya Kibo Palace.Tukajaribu kumkumbusha kilichompeleka Arusha.

Akionekana kutuelewa, akacheka na kusema 'najua,lakiniPolisi tuna zaidi ya hayo'. Si vyema Kamanda Chagonja kumezwa na hali ya kisiasa iliyopo Arusha na kusahau kilichompeleka.

Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam.

Siku zinakuja hata yeye atakuwa raia kama sisi, Yuko wapi Mahita na Visu vya CUF? Watu wengi hatujui kwamba sio kila siku ni Jumapili. Inteligensia inamtuma kuwaweka ndani CHADEMA.
 
Huyu Chang'onja Mi kwa mtazamo wangu wa haraka haraka nina hofu sana uongozi wake!
Na kwa ujumla ataipeleka Taifa pasipo kwa dalili anayokuja nayo!
Nyambafu kabisa!
 
Some of the people joined the force in the past...I can imagine they are now in the positions of power and decisions
 
Back
Top Bottom