Police Arusha wanatangaza mkutano wa CDM si halali

Police Arusha wanatangaza mkutano wa CDM si halali

Wajamani bado nipo na hang over but nimeweza kusikia hii
Kituo cha redio Triple A FM imetangaza kuwa mkutano wa chadema
Ambao unatakiwa kufanyika leo wanasema si halali
Hivyo tunatahadhalishwa na kusisitizwa tusiende, Je hizi ni zile
Zao za Kiccm kuleta kauzibe ama ni vipi ?
polisi hawaombwi kibali, bali wanapewa taarifa ndani ya saa 48, kama kuna upungufu wa askari wakutoa ulinzi, na wenyewe wanatakiwa kutoa taarifa kuwa, kutokana kutokuwa na askari wa kutosha tunaomba usitishwaji wa mkutano huo, then wanatakiwa kutoa sababu kwanini hawana askari wa kutosha, kama sababu zao zinaeleweka ndipo na nyie mnaweza kuridhia na kuahirisha mkutano huo mpaka hapo mtakapo panga tena
lakini siyo kusema hamna askari kwasababu hazina nyuma wa mbele, CHADEMA FANYENI MKUTANO WENU SHERIA ZIPO ZINAWALINDA, ACHENI CCM WATUMIE UBABE WAO SISI TUSONGE KWA NGUVU YA UMMA WAO WANA DOLA SISI TUNA MUNGU
 
kuna magari 9 maeneo ya uwanja yote kuhakikisha cdm hawafanyi mkutano
 
Wafuasi wa Mbunge wa CHADEMA Arusha waandamana kuelekea makao makuu ya Polisi kudai haki ya kufanya mkutano wao leo uliozuiwa.
SOURCE: www.ippmedia.com
 
Wabunge wa chadema wanaandamana kwenda polisi arusha kudai haki zao za kufanya mkutano wa uchaguzi. Source ITV
Wajamani bado nipo na hang over but nimeweza kusikia hii
Kituo cha redio Triple A FM imetangaza kuwa mkutano wa chadema
Ambao unatakiwa kufanyika leo wanasema si halali
Hivyo tunatahadhalishwa na kusisitizwa tusiende, Je hizi ni zile
Zao za Kiccm kuleta kauzibe ama ni vipi ?
 
mkutano ni saa 9 lakini watu wameanza kuja saa nne..
 
hivi polisi kazi yao kutoa kibali au kutoa ulinzi katika mikutano nadhani hapa kuna umbumbumbu wa uelewa!

Sheria ya Vyama Vingi inaruhusu viongozi wa vyama vilivyosajiliwa kufanya mikutano na wananchi. Havihitaji kibali cha Polisi, bali chini ya Kanuni zilizotungwa kwa mujibu wa Sheria ya Polisi, Polisi wanahitaji taarifa ya masaa 48 kabla ya mkutano wa hadhara, ili waweza kuleta ulinzi mahali panapofanyika mkutano. Nasema haya kwa uhakika kutokana na uzoefu wangu, na nikiwa ni Muasisi wa Chadema.

Inaonekana sasa Polisi wanaegemea "taarifa za ki-intelligensia" ili kuzuiya vyama vya upinzani visifanye mikutano: eti taarifa zinaashiria kutakuwa vurugu na uvunjifu wa amani. Hivi hawa Polisi wataibeba CCM mpaka lini? Hata wao wenyewe wanaweza kufanya fujo na kuanza vurugu mahali mkutano unapofanyika ili kuthibitisha kwamba taarifa zao za "intelligensia" zilikuwa sahihi! Tunaanza kutoa sababu za kipuuzi sana!

Ningetaka kushauri serikali ya Jakaya Kikwete ipime kwa makini zaidi maono na maslahi ya Watanzania wa leo. Wengi wameonyesha kuchoshwa na mienendo ya viongozi wengi wa CCM na Serikali. Hawa viongozi hawahitaji ushahidi zaidi ya jinsi kura zilivyopigwa wakati wa Uchaguzi Mkuu huu uliopita. Watanzania wamechoka na uongozi wa CCM. Wanataka mabadiliko.

Nimefarijika kidogo kuona juzi kwamba hata Waziri Mkuu amekubali hoja yetu kwamba Katiba ya Tanzania inahitaji tathmini ya kina. Kama ni hivyo, basi ni vema umma ukaanza mapema kujadili hadharani mambo yanayopaswa kuzingatiwa katika mjadala wa marekebesho ya Katiba. Hayo ndiyo madhumuni ya msingi ya mikutano mingi ya Chadema inayoandaliwa sasa. Viongozi kama IGP Mwema aandae maofisa wake ili waone vyama vya upinzani vinaongozwa na Watanzania wanaojali maslahi ya taifa pia.

Hivi visingizio vya taarifa za kiintellijensia za uvunjifu wa amani na vurugu vikome. Elimu ya Uraia mwema itolewe kwa Polisi na watumishi wengine wa serikali, kwamba Upinzani wa kidemokrasia utaboresha maendeleo ya nchi kwa faida ya vijana wa Polisi na watu wote wa Tanzania. Hilo lieleweke hasa kwa Polisi.
 
Back
Top Bottom