Police Arusha wanatangaza mkutano wa CDM si halali | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Police Arusha wanatangaza mkutano wa CDM si halali

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Easymutant, Dec 22, 2010.

 1. Easymutant

  Easymutant JF-Expert Member

  #1
  Dec 22, 2010
  Joined: Jun 3, 2010
  Messages: 2,570
  Likes Received: 570
  Trophy Points: 280
  Wajamani bado nipo na hang over but nimeweza kusikia hii
  Kituo cha redio Triple A FM imetangaza kuwa mkutano wa chadema
  Ambao unatakiwa kufanyika leo wanasema si halali
  Hivyo tunatahadhalishwa na kusisitizwa tusiende, Je hizi ni zile
  Zao za Kiccm kuleta kauzibe ama ni vipi ?
   
 2. mopaozi

  mopaozi JF-Expert Member

  #2
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 17, 2010
  Messages: 3,290
  Likes Received: 105
  Trophy Points: 160
  hivi polisi kazi yao kutoa kibali au kutoa ulinzi katika mikutano nadhani hapa kuna umbumbumbu wa uelewa!
   
 3. Kaizer

  Kaizer JF-Expert Member

  #3
  Dec 22, 2010
  Joined: Sep 16, 2008
  Messages: 24,664
  Likes Received: 1,506
  Trophy Points: 280
  hawana lolote hao hawawezi kuuzuia mkutano kazi yao kutoa ulinzi.....
   
 4. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #4
  Dec 22, 2010
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,828
  Likes Received: 10,140
  Trophy Points: 280
  Hawa polisi watatupeleka pabaya sasa, namkumbuka sana RC alieondolewa, MUNGU atakukumbuka tu, acha huyu mpuuzi alieletwa kulinda maslahi ya wachache! hapa wanaanzisha vurugu ni cdm au polisi? au kuanzisha vurugu ni hadi urushe virungu? pambaf kabisa....mpwa hangover zikipungue utuletee updates basi
   
 5. BONGOLALA

  BONGOLALA JF-Expert Member

  #5
  Dec 22, 2010
  Joined: Sep 14, 2009
  Messages: 13,792
  Likes Received: 2,400
  Trophy Points: 280
  nahisi enzi za mahita zinarudi arusha!shame on rpc
   
 6. Mungi

  Mungi JF Gold Member

  #6
  Dec 22, 2010
  Joined: Sep 23, 2010
  Messages: 16,986
  Likes Received: 444
  Trophy Points: 180
  Mkutano utafanyika kama kawaida, hatuna silaha hatuna marungu, kwa hiyo kama watakuja na silaha nzito kuwatishia wanachi patachimbika.
  Andengenye angali sana usije fia kwenye kiti.
   
 7. P

  Paul S.S Verified User

  #7
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Nasikiliza sasa hivi live Clouds fm, rpc arusha anaongea kuwa sababu za kusitisha mkutano huo,
  <Anadai kuwa si kazi ya jeshi kutao kibali isipokuwa kisheria na taratibu chama husika kinapaswa kutoa taarifa polisi masaa 24 kabla ili kutimiza takwa la kufanya mkutano, lakini chadema taarifa wametoa jana hivyo masaa 24 yanaangukia kesho.
  <Pia akadai kwa taarifa zao za kiitelijensia wamepata taarifa kuwa kunawasiwasi wa hali ya usalama katika mkutano huo.
  <Pia inapaswa barua ya mkutano inapaswa kutaja madhumuni ya kufanya mkutano kitu ambacho cdm hawakufanya hivyo
  Kwahiyo wamesimamisha mkutano huo hadi itakapo tangazwa vinginevyo
   
 8. G

  Gagnija JF-Expert Member

  #8
  Dec 22, 2010
  Joined: Apr 28, 2006
  Messages: 6,316
  Likes Received: 618
  Trophy Points: 280
  RPC anasema pamoja na mambo mengine CHADEMA walipaswa kuijulisha Polisi mkutano huo utahusu nini. Hivi hii mahakama ya Ocampo haina jurisdiction kwenye mambo kama yanayofanyika Tanzania sasa hivi?
   
 9. Ibra Mo

  Ibra Mo JF-Expert Member

  #9
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 27, 2010
  Messages: 795
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  Hili jitu(Andeng'enye)limetumwa Arusha kuja kupora Haki za wana Arusha nimelisikia sasa iv Cloudz likijaribu kutumia Hila et huo Mkutano utakuwa na vurugu,Wana Arusha msikubali kutawaliwa Kiimla lazima leo muonyeshe msimamo wenu kama aliamuru Mbunge wenu apigwe tena live tumeona kwenye Tv leo hii nani amuamini,hizo Propoganda anazotumia zikataeni mnahaki yakwenda kumsikiliza Mbunge wenu huyo ni Mtu wakuja tu na Arusha ni ya Wana Arusha itajengwa nakutetewa na Wana Arusha Majasiri,Wasioogopa ambao wako tayari kufa kwaajili yakutetea Haki zao.Mbona ccm wanafanya Mikutano juzi hapa tumeshuhudia Mikutano ya Anna Makinda na Samwel Sitta ikija kwa Chadema uvunjifu wa Amani!!Andeng'enye usitufanye Wananchi tulichukie Jeshi la polisi nakujenga uadui nalo 4ua own purposes nguvu haitakusaidia na nivyema ukaiaproach njia aliyotumia mtangulizi wako Basilio Matei otherwise Kazi itakushinda.
   
 10. Mdau

  Mdau JF-Expert Member

  #10
  Dec 22, 2010
  Joined: Mar 29, 2008
  Messages: 1,771
  Likes Received: 252
  Trophy Points: 180
  Hii nchi inafika penyewe sasa, nafurahi sana kwamba damu itaendelea kumwagika kuelekea ukombozi wa kweli....CCM ni sikio la kufa, haliwezi kusikia dawa mpaka tulikate!!!! And honestly speaking, bila damu hatuwezi kufika....
   
 11. Iza

  Iza JF-Expert Member

  #11
  Dec 22, 2010
  Joined: Jan 8, 2009
  Messages: 1,848
  Likes Received: 120
  Trophy Points: 160
  hawa polisi wanasahau wapo kwa ajili ya usalama wa raia na sio ccm...
   
 12. s

  sikujua Member

  #12
  Dec 22, 2010
  Joined: Feb 23, 2010
  Messages: 8
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 3
 13. m

  mtemiwao JF-Expert Member

  #13
  Dec 22, 2010
  Joined: Sep 5, 2010
  Messages: 384
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mwanzo wa ukombozi unaanza,twendeni tukiwa tumejiandaa tuwape fundisho hawa mabaradhuri,tuweke historia mkutano ni lazima haturudi nyuma
   
 14. Ndallo

  Ndallo JF-Expert Member

  #14
  Dec 22, 2010
  Joined: Oct 1, 2010
  Messages: 7,134
  Likes Received: 1,089
  Trophy Points: 280
  Wao wanapesa na wameshikilia dola! Lakini sisi tuna Mungu hakika tutafika!
   
 15. tanga kwetu

  tanga kwetu JF-Expert Member

  #15
  Dec 22, 2010
  Joined: May 12, 2010
  Messages: 2,165
  Likes Received: 1,125
  Trophy Points: 280
  ...nipo maeneo ya njia panda himo naja arusha kwa ajili ya huo mkuatano tu....halafu huyo rpc anasema nini? hiyo sababu ime-expire, whenever kuna mkutano wa CDM utasikia utumbo wa 'taarifa za kitelejensia zinasema mkutano utakuwa na vurugu'!!! stupid!!! siku zote nasema na naamini katika hilo bila kufinyana kidogo heshima itakuwa hamna. sasa waje waone! tuwe karibu na oil chafu maana yale maji ya kuwasha hayaoni ndani ukijipaka oil chafu!!! nimetoa nauli yangu kuusafiria mkutano halafu mtu kwa amri ya Makamba atuzuie tusiwasikie viongozi wetu!! pambaf zaio!!!
   
 16. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #16
  Dec 22, 2010
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Polisi Arusha wawalazimisha vijana kufanya mapenzi
  Tuesday, 21 December 2
  Mwandishi wetu,
  Arusha

  JESHI la polisi mkoani Arusha, limekumbwa na kashfa nyingine, baada ya polisi wake wawili kutuhumiwa kuwateka vijana watatu waliokuwa wakifanyabiashara na kuwapora fedha na kuwalazimisha kujamiiana huku wakiwapiga picha katika eneo la Ikulu ndogo ya Arusha.

  Tukio la aina yake, ambalo tayari limeripotiwa polisi, lilitokea juzi kuanzia saa 5:00 asubuhi hadi saa 8:00 mchana na polisi kuwaachia huru. Vijana hao, walikuwa wakifanya biashara ya kuuza virutubisho vya mwili aina ya Arovela.

  Wakizungumza katika ofisi za Mwananchi jana,wafanyabiashara hao, Victoria Agustine(22),Evance Fank(24) Godbless Shirima(18), walisema walikamatwa na polisi hao, wakiwa wanapita nje ya jengo la Ikulu ndogo ambalo lipo jirani na Mahakama Kuu Kanda ya Arusha.

  Frank alisema wakiwa wanatembeza bidhaa hizo ambazo zinatolewa nakampuni ya Mwema General Supply ya Arusha, walipita mbele ya Ikulu, na polisi wawili walikuwa lindo waliwaita nawalipoingia ndani na Ikulu walianza kuwahoji maswali kuhusu biashara hiyo.

  Alisema ghafla waliambiwa kupiga magoti na kuweka mikono juu, na kuanza kupewa mazoezi ya kupiga pushapu, kuruka kichurachura na baadaye waliwataka kuwakabidhi fedha zote walizonazo.

  "Tulisema hatuna fedha, lakini mmoja alianza kutupekuwa na kuchukua Sh 200,000 za mauzo kwa kiongoziwetu Shirima,” alisema Frank.

  Frank alisema pamoja na kuchukua fedha hizo, pia waliwataka kutoa sadaka na walichukua kwa nguvu Sh 2,500 kutoka kwa kila mmoja.

  "Mimi nilikuwa nawaambia kama tumefanya makosa watupeleke polisi waligoma kabisa na walikuwa wakisisitiza tumefanya makosa kupita mbele ya Ikulu,"alisema Frank.

  Alisema baaday waliwavua nguo na kuwataka kufanya mapenzi na Fank na Victoria waliambiwa kukubatiana nakunyonyana ulimi.

  "Mimi nilikataa kufanya mapenzi wakanilazimisha huku, wakinipiga, lakini nilikataa na kulala ndipo walilazimisha tunyonyane ulimi na Victoria huku wakitupiga picha kwa simu ya mkononi,"alisema Frank.

  Naye Shirima ambaye alikuwa kiongozi, alisema wakati wanapigwa alimtambua polisi mmoja na akamuita kwa jina huku akiomba wasiendelee kuwatesa, lakini aligoma na kuendelea kuwapiga.

  "Tuliwakuta wamelewa na mimi namjua mmoja kabisa kwa jina(jina linahifadhiwa) nikamwambia mimi namjua na kaka yangu alikuwa polisi na pia kuna ndugu yangu ni ofisa wa Magereza Manyara, aliposikia hivyo alianza kunihoji ni wapi nilimuona nikamwambia ndipo alisema anatupeleka polisi, lakini tulipofikanjiani alituacha na kuondoka,"alisema Shirima.

  Mwandishi wa habari hizi, juzi aliwakuta wafanyabiashara hao, wakiwa wanatoa maelezo katika ofisi ya Mkuu wa upelelezi wilaya ya Arusha na baadaye kwa kamanda wa polisi mkoani Arusha, lakini hadi jana hakuna hatua ambazo zilikuwa zimechukuliwa.

  "Yule mkuu wa upelelezi badala ya kufungua kesi ya malalamiko yetu alianza kuzungumza na kiongozi wa walinzi wa Ikulu na kuomba tukutanishwe ili waombe msahama na akatuomba tuache namba za simu lakini hadi leo(jana) hajatupigia,"alisema Shirima.

  Vijana hao, wamelishauri jeshi la polisi kuchukua hatua kali dhidi ya polisi na kuwalazimisha kufuta picha walizowapiga ili zisisambaa mitaani.

  Alifafanua kuwa baada ya kufika kwa kamanda wa polisi mkoani Arusha, Thobias Andengenye alitusikiliza na kutueleza kuwa atatupigia simu, lakini pia hadi leo (jana) bado hajatupigia.

  Kamanda wa polisi mkoani Arusha, Thobias Andengenye hakupatikana jana kuelezea tuhuma hizo, baada ya simu yake ya mkononi kupokelewa na msaidizi wake aliyedai kuwa yupo katika kikao ofisi ya mkuu wa mkoa wa Arusha. Pia saa 8:52 Mwananchi lilimpigia tena lakini simu yake haikupokelewa na ilikuwa ikita tu muda wote bila kujibiwa.

  Tukio hili ni mfululizo wa matukio ya unyanyasaji wa polisi kwa raia na hivi karibuni walituhumiwa kumpiga mbunge wa Jimbo la Arusha, Godbless Lema na pia waliwahi kutuhumiwa kuwauwa kwa risasi vijana wawili eneo la Kijenge, lakini hata hivyo hakuna hatua zilizochukuliwa.

  Source: MWANANCHI
   
 17. Ndachuwa

  Ndachuwa JF-Expert Member

  #17
  Dec 22, 2010
  Joined: Mar 8, 2006
  Messages: 4,530
  Likes Received: 725
  Trophy Points: 280
  Masaa 48 siyo 24; inawezekana kichwa chako kila jambo linagawa kwa mbili huenda hata pesa zilizoko benki ni mara mbili ya unavyokumbuka nenda kaangalie salio haraka
   
 18. Ulimbo

  Ulimbo JF-Expert Member

  #18
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 14, 2009
  Messages: 678
  Likes Received: 41
  Trophy Points: 45
  Nipo Arusha kwa sasa maeneo ya stand kuu. Kuna Land cruiser ya polisi imefika hapo na matangazo wanayotangaza ni kuwa MKUTANO WA CHADEMA ULIOPANGWA KUFANYIKA HAUTAFANYIKA.
  Sasa mimi najiuliza, ni kazi ya polisi kutangaza mikutano kufanyika au kutofanyika?
   
 19. Saharavoice

  Saharavoice JF-Expert Member

  #19
  Dec 22, 2010
  Joined: Aug 30, 2007
  Messages: 2,644
  Likes Received: 131
  Trophy Points: 160
  Kuna haja ya kutoa fundisho kali kwa polisi ili wasije rudia tena upuuzi wao.

  CDM tangazeni adui namba moja ni polisi from now on
   
 20. kagumyamuheto

  kagumyamuheto JF-Expert Member

  #20
  Dec 22, 2010
  Joined: Nov 5, 2010
  Messages: 286
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  notisi ya masaa 24 ipo kisheria. huwezi kwenda kinyume halafu ukategemea public sympathy.
   
Loading...