Polepole: Utaratibu wa CCM ni kuwa, Samia alitakiwa kuishia 2025 na kukabidhi kwa mwingine

Polepole: Utaratibu wa CCM ni kuwa, Samia alitakiwa kuishia 2025 na kukabidhi kwa mwingine

Rabbon

JF-Expert Member
Joined
Apr 16, 2022
Posts
25,938
Reaction score
41,098
Salaam!

Kuna kitu Polepole anekiongea kizito ambacho tumekuwa tukikisema humu mara nyingi.

Ameenda mbali na kudai, ikiwa tuna mashaka na akisemacho, tukamuulize Mzee Mangula!

1. Ni hivi, amesema Spika wa bunge, VP,Waziri Mkuu ni marufuku kupitishwa kuwa wagombea urais ,huo ni utaratibu ,miiko na desturi walizojiwekea wao wa ccm,ingawa ni haki yao kikatiba kugombea Urais.

2. Amedai pia kuwa, baada ya kifo Cha JPM, ilitakiwa amalizie awamu aliyoanza Magu Kisha kukabidhi kwa mwingine, huo ni utaratibu wa CCM,ingawa ni haki ya kikatiba kwa aliyepokea kijiti kugombea sawa sawa na isemavyo katiba.

Sasa alichofanya Samia ni kufumbia macho utaratibu uliopo ndani ya CCM ambao pia umemuondoa PM kugombea Ubunge kwa awamu ingine baada ya miaka 10 ya uwaziri Mkuu kwisha.

Tunakushukuru Mh Polepole kuliweka hili wazi maana hata huku kijijini kwa Hali ya kawaida, boss akifariki, ukapewa kushika Nafasi yake kwa muda, unatakiwa kukabidhi madaraka baada ya muda wa marehemu kwisha, Ili wana ukoo wamchague wamtakae, kulazimisha kuendelea ni kutengeza taswira mbaya juu ya...

Mungu ibariki nchi YANGU nzuri niipendayo Tanzania 🇹🇿

Nawasilisha 🙏
 
imetosha wapendwa huyu mama mta muua
Haya ni mambo ya nchi na mustakabali wetu na vizazi vijavyo.

Akiona tunamwandama, aachie ofisi akapumzike nyumbani aone kama tutamsema,

Utaratibu ufuatwe,

Akabidhi kijiti, utaratibu ufuatwe, watu wachukue fomu, mchakato uwe wazi, vyama vyote vya upinzani viruhusiwe kuingia uchaguzini,

Ccm iendelee kushika hatamu kwa haki.

Tofauti na hapo 🤔
 
Salaam!

Kuna kitu Polepole anekiongea kizito ambacho tumekuwa tukikisema humu mara nyingi.

1. Ni hivi, amesema Spika wa bunge, Waziri Mkuu ni marufuku kupitishwa kuwa wagombea urais ,huo ni utaratibu ,miiko na desturi walizojiwekea wao wa ccm,ingawa ni haki yao kikatiba kugombea Urais.

2. Amedai pia kuwa, baada ya kifo Cha JPM, ilitakiwa amalizie awamu aliyoanza Magu Kisha kukabidhi kwa mwingine, huo ni utaratibu wa CCM,ingawa ni haki ya kikatiba kwa aliyepokea kijiti kugombea sawa sawa na isemavyo katiba.

Sasa alichofanya Samia ni kufumbia macho utaratibu uliopo ndani ya CCM ambao pia umemuondoa PM kugombea Ubunge kwa awamu ingine baada ya miaka 10 ya uwaziri Mkuu kwisha.

Tunakushukuru Mh Polepole kuliweka hili wazi maana hata huku kijijini kwa Hali ya kawaida, boss akifariki, ukapewa kushika Nafasi yake kwa muda, unatakiwa kukabidhi madaraka baada ya muda wa marehemu kwisha, Ili wana ukoo wamchague wamtakae, kulazimisha kuendelea ni kutengeza taswira mbaya juu ya...

Mungu ibariki nchi YANGU nzuri niipendayo Tanzania 🇹🇿

Nawasilisha 🙏
NO REFORMS, NO ELECTION.
 
Tuseme kipindi cha JPM kinaisha 2025, anatakiwa mwingine. Atakaejitokeza aombe kama katiba inavyosema. Polepole yupo sahihi.
Ni sahihi kabisa,

PM kanaliza 10 yake kakaa Pembeni.

Samia naye kumi imeisha. Na utaratibu walliojiwekea ccm ikitokea Rais kafia madarakani ni kukabidhi kijiti kwa chama, chama kifanye mchakato wa wazi kizibe matundu Katika mtumbwi, apattikane Nahodha mwingine, safari iendelee.

Mzee Kikwete kama mshauri Mkuu, anakipekeka shimoni chama,

Wamuondoe haraka.
 
Back
Top Bottom