GE2025 Polepole: Tarehe 29 sitaonekana kwenye kituo chochote cha kupiga kura kwa sababu hakuna Uchaguzi ni kiini macho

GE2025 Polepole: Tarehe 29 sitaonekana kwenye kituo chochote cha kupiga kura kwa sababu hakuna Uchaguzi ni kiini macho

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Chamoto

Platinum Member
Joined
Dec 7, 2007
Posts
9,856
Reaction score
22,189
Anaandika Humphrey Polepole kupitia ukurasa wake wa Instagram:

1758712975786.jpeg

"Ukiona ukiwasikiliza ndani ya moyo wako hawakupi amani ya moyo, ukiona wanatumia nguvu kubwa kukushawishi hata kwa mambo ya kawaida na bado unahisi na kuona kutokuwaamini, ukiona wakitajwa unahofia usalama wako, ukiona hauwezi kuongea kwa uwazi, uko sahihi..

Mtu huyo, ambaye nyuma yake kuna genge la mtandao, halindi, haheshimu, hathamini, hahangaiki wala hahangaishwi na utu wako kubagazwa, kubanangwa, kutindinganywa na kutokuheshimiwa!

Mimi sitatoa uhalali kwa mtu wa aina hiyo kuwa kiongozi kwenye nchi yetu, sitaonekana kwenye kituo chochote cha kupigia kura!

Siri - Saiz kinachowanyima amani yao na usingizi ni sisi kuwaachia na kuwasusia wanachoita uchaguzi wao, mimi naita kiini macho, wako bize kufanya mikutano ya hadhara na husikii masuala yanayobananga nchi yetu yakiwekewa mikakati ikiwemo Haki za watu, Usalama wa Raia, Vita dhidi ya Rushwa, Ufisadi na wizi uliokithiri wa rasilimali na madini yetu (utajiri wa nchi hii tuliopewa na Mungu wetu).

Mjuze siri hii na mwingine"

Kwenda kwenye kituo cha kupigia kura kwaajili ya kuhalalisha huu ushetani ni kujishiriki uovu. Kila mwenye akili timamu, mtu asiye mwovu, kamwe hawezi kushiriki kwenye uchaguzi huubkwa namna yoyote ile. Tuyaache mafisi yanayosombwa kwenye malori kila siku kwenda kuhalalisha uovu.
 
Hv siku ya kupiga kura wataruhusiwa na sheria kusomba watu kwa malori kwenda kupiga kura?!.
 
Kwenda kwenye kituo cha kupigia kura kwaajili ya kuhalalisha huu ushetani ni kujishiriki uovu. Kila mwenye akili timamu, mtu asiye mwovu, kamwe hawezi kushiriki kwenye uchaguzi huubkwa namna yoyote ile. Tuyaache mafisi yanayosombwa kwenye malori kila siku kwenda kuhalalisha uovu.
Kwa mtu anayependa haki, anatakiwa kuwa mbali sana na kituo cha uchaguzi.
 
Ivi sheria ya uchaguzi inasemaje mgombea asiye fikisha 50% ya kura zote kupigwa.
 
Ivi sheria ya uchaguzi inasemaje mgombea asiye fikisha 50% ya kura zote kupigwa.
Mgombea atapataje kura chini ya 50% wakati tunaambiwa mifumo wa NIDA, CCM na tume ya uchaguzi inasomana?
 
Umeshasema mgombea haram,uchaguzi batili halafu unaongelea kupiga kura.

Sasa alitaka akampigie nani?
Hiyo sasa ndiyo definition ya mtu aliyepoteza mwelekeo ma asiye na dira.

Hawa wote pamoja na MangeKimambi tuwazoee tuishi nao
 
Mgombea atapataje kura chini ya 50% wakati tunaambiwa mifumo wa NIDA, CCM na tume ya uchaguzi inasomana?
Tuanze na sheria kwanza.
Mifumo ikisomana wkt nchi nzima watu wamesusia kufika kwenye vituo kupiga..mifumo itafel tu.
 
Hiki kiini macho mbona kilianza kitambo sana...; Tofauti sasa hivi ni kwamba anayedanganywa anajua kwamba anadanganywa...

Kwa ufupi anasisitiza watu wasiende kupiga vote. Maana yeye twajua hajatumiwa fare ya kurudi toka Cuba
 
Back
Top Bottom