GE2025 Polepole pamoja na kutekwa ninaamini watekaji hawatomfanya kitu. Ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama na CCM (ukitoa Polisi) ana kishindo kikubwa

GE2025 Polepole pamoja na kutekwa ninaamini watekaji hawatomfanya kitu. Ndani ya vyombo vya ulinzi na usalama na CCM (ukitoa Polisi) ana kishindo kikubwa

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Tajiri wa kinyankole

JF-Expert Member
Joined
Jun 12, 2019
Posts
1,959
Reaction score
4,862
Vyombo vya habari tangu jana vimeripoti aliyekuwa balozi nchini CUBA hampfrey polepole kutekwa na kupelekwa. kusipojulikana na shuhuda mmoja ambaye alijitambulisha kwa jina la augustino polepole alimtaja waziwazi mhusika mkuu wa utekaji kuwa ni mtu mmoja ajulikanaye kwa jina la MAFWELE hata hivo baada ya taarifa hizo kusambaa mitandaoni chombo cha habari cha BBC kilifika katika familia ya bwana polepole wajathibitisha kuwa ndugu yao ametekwa na kwamba wameripoti kituo cha polisi mbweni jijini dares salaam kutoa taarifa za ndugu yao.

Pamoja na taarifa hiyo kamanda wa polisi kanda maalumu muliro jumanne mliro alipohojiwa na chombo cha habari cha BBC kuhusu kutekwa kwa bwana polepole alisema kwamba mtu huyo taarifa zake mara nyingi anasema hayuko nchini kwa hiyo hana taarifa yoyote juu ya utekaji huo na kwamba anafuatilia.

Aidha wakati vyombo vya habari vikiripoti tukio hilo jeshi la polisi lilitoa taarifa kwamba halijamshikilia mtu huyo na kwamba bado wanamuhitaji afike ofisi ya DCI kwa ajiri ya mahojiano.

👉Kitu pekee nawaambia jeshi la polisi yawezekana mnatumiwa na watesi wa polepole huko mlipompeleka mjiulize huyo anakosa gani ! Nafsi zenu ziwafanye muwe na huruma kwa kijaba huyo ambaye hana hatia kwa kukosoa serikali yake , amri mtakazo pewa kwa ajiri ya kumdhuru kijana huyo mjitafakari kwa kina na wala msitingishike mtende haki , maana kama kuna chochote ambacho mtakuwa mmepewa amini nawambia hakita kuwa na maana yoyote isipokuwa mtakuwa mmezima sauti ya umma kwa ajiri ya wachache waliowatuma ambao nyie mtastaafu hakuna atakayekuwa na habari na nyie isipokuwa familia zao zitaendelea kufanya yaliyokuwa yanasemwa na polepole.

👉Polepole ni kiongozi ndani ya ccm na ndani ya vyombo vya ulinzi na usalaama ana watu nyuma yake isipokuwa polisi ambao upepo kila unapovuma na wao ni hukohuko , mkitambua hilo hamtaweza kumfanya chochote maana kukaa nchini alijuwa nini kingemtokea ndiyo maana aliamua kusema , polisi msikubali mtego huo mkiamni kwamba mnafanya kazi vizuri ccm ambao wanachukizwa na mambo haya wapo kimya na viongozi wa vyombo wapo kimya huyo kijana muwe makini naye msijaribu kumfanya chochote mtaharibu kila kitu amini na waambia mtaharibu kila kitu kitakachotokea ni hatari kwa taifa, baadhi ya viongozi wa nchi miongoni mwao ni rafiki zake pia na bado wapo madarakani.

Mbegu hiyo mkiipanda itakula vizazi vyenu huku waliowatuma wakila mema yawezekana ndani ya nchi au nje ya nchi.

Mimi ninaimani kubwa polepole kama tetesi zinavyosemwa kushikiliwa na watesi wake kwamba watamdhuru ni vigumu mno kutekeleza walichopanga ingawa wanapenda iwe hivo trust me ni vigumu mno.
 
Mpaka sasa tumeshajionea wazi hakuna wa kuwapigania Watanzania mamlaka zote zipo upande wa muuwaji.
Tukiendelea kujidanganya kwamba kuna mwingine zaidi ya sisi wenyewe tutamalizwa kama Vifaranga vya Kuku.
 
Tukiendelea kujidanganya kwamba kuna mwingine zaidi ya sisi wenyewe tutamalizwa kama Vifaranga vya Kuku.
Swala la mtu huyo haliwezi kupita hata ndugu wanajuwa nani yuko naye na vyombo pia vinajuwa , huyo mtu akiuawa ni hatari mkuu. trust me kishindo kilichopo kati ya tarehe 20 hadi kufika 29 ya kiini macho mhuu! Acha nigune tu ! Huyo watamwachia hawana njia nyingine ya kumfanya
 
Tukiendelea kujidanganya kwamba kuna mwingine zaidi ya sisi wenyewe tutamalizwa kama Vifaranga vya Kuku.
Kaa kwa kutulia siku wanafunga kampeni ni. Siku ambayo watafunga mitandao sasa kitakachofuata mungu ndiye anajuwa ndani ya CCM! Tafakatlri CCM walivyokaa kimya hadi sasa. Amsha amsha zinakuwepo aliyejichagua anapokuwa eneo husika akitoka wanabaki kumteta.
 
Back
Top Bottom