Polepole mgeni rasmi Mahafali ya UVCCM UDOM

Omary Kipingu

Member
Feb 22, 2016
40
48
*Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi CCM kuwanoa Wahitimu na kukabidhi Vyeti 402 ktk Mahafali Umoja wa vijana CCM Vyuo na Vyuo Vikuu.*

Tarehe 13/05/2017 Umoja wa Vijana idara ya Vyuo na Vyuo vikuu walikuwa na Mahafali ya kuwaaga wahitimu wa Vyuo Mkoa wa Dodoma ambao ni wanaCCM .

Hafla hiyo imefanyika katika ukumbi wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi Makao Makuu.Hafla hiyo imehudhuriwa na viongozi wa CCM mkoa wa Dodoma na Baadhi ya Wabunge wa Bunge la Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ambao wanatokana na CCM, Wakuu wa wilaya, Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana Taifa Ndugu Sadifa Juma na Katibu wa NEC itikadi na Uenezi akiwa ni Mgeni Rasmi wa Hafla hiyo.

Umoja wa vijana idara ya Vyuo na Vyuo vikuu wamemuhakikishia Mgeni rasmi Ndugu Humphrey Polepole kuwa wanavyuo wengi Mkoa wa Dodoma wanakiunga Mkono Chama Cha Mapinduzi pamoja Utendaji wa Serikali ya Chama Cha Mapinduzi chini ya Rais Dk.John Pombe Magufuli.

Ndugu Humphrey Polepole amewakabidhi vyeti vya pongezi wanavyuo 402 wanaCCM wanaotarajia kuhitimu mwaka huu katika fani mbalimbali na Vyuo mbalimbali mkoa wa Dodoma.

Ndugu Humphrey Polepole Amewaambia Vijana wahitimu wa Vyuo Vikuu wakawe mfano mwema katika Jamii yao. Pia Ndugu Humphrey Polepole amewasisitiza wale wenye sifa na vigezo wasisite kuomba nafasi ndani ya Chama Cha Mapinduzi katika wakati huu ambao CCM ipo kwenye uchaguzi wa ngazi zote na jumuiya zote, Amewahikishia CCM Mpya hakuna Mtu atakayehujumiwa akiomba uongozi ndani ya CCM.
"Ole wao watakao wahujumu wenzao kwenye uchaguzi huu na kumkata mwenye haki yake tutalalanao mbele" Alisema Ndugu Humphrey Polepole.

Chama Cha Mapinduzi kinajali makundi yote,hivi karibuni wasomi wengi wa Vyuo vikuu wamekuwa wakikiunga Mkono Chama Cha Mapinduzi Jambo ambalo ni ishara nzuri kwa Chama hiki kikongwe barani Afrika. CCM imara Tanzania Imara.
IMG-20170514-WA0301.jpg
IMG-20170514-WA0263.jpg
IMG-20170514-WA0261.jpg
IMG-20170514-WA0262.jpg
 
Hivi sio kwamba siasa haziruhusiwi mashuleni na vyuoni? Halafu hiyo quotation ya marehemu J. K. Nyerere kwenye hilo bango ina maanisha muda wote au katika ule uchaguzi wa kwanza baada ya vyama vingi kurejeshwa? Halafu sio kila kuyumba kuna matokeo mabaya. Mfano, shake well before drinking!!!!!
 
Kuuliza sio ujinga...Hivi hivyo vyeti wanapewa baada ya kuhitim nini ?Mwenye taarifa nitoe tongo tongo
 
Viongoz wa kula rambi rambi hao. Siku hiz ramb rambi ndiyo mtaji wa ccm. Wanaomba litokee janga lingine zaid ya ile ya Arusha wakale hela. Nilishangaa baada ya kuona timu ccm wameenda Arusha hela ndizo wameenda kufuata
 
Back
Top Bottom