Kila mara tunasikia viongozi wakikemea 'uchochezi'
Pengine watu hawajui uchochezi si maneno, ishara inaweza, matendo yanaweza kuwa n.k.
Mwaka jana Polisi walisambaratisha mahafali ya vijana wa upinzani 'hali ya usalama haijatengamaa''
Tangu sambaratisho hilo hadi leo hakuna tangazo lililotolewa hali ya usalama imeaimarika
Ghafla vijana wa CCM kama wale wa Chadema , wameruhusiwa kufanya mahafali kama yale ya vijna wa Chadema katika ukumbi wa CCM kama ilivyokuwa nje ya Chuo kwa Chadema
Huu ni uchochezi kwasababu wa mwaka jana wanajiuliza , walikosea nini katika mahafali yao?
Kwanini wenzao wamefanya kwa amani bila doria au magari ya washawasha ya Polisi
Kwa upande mwingine jambo hili linaondoa credibility ya kauli za serikali.
Kwamba, siku litakapotolewa tangazo lingine halali wananchi watalichukuliwa ni la CCM na Polisi
Kinachofuata ni kuendelea kujengeka kwa makundi, kugawanyika kwa wananchi, kujaa chuki miongoni mwa wananchi, Taifa kugawanyika bila sababu za msingi wala zenye mashiko
Chuki inayojengeka hujitokeza kwa namna nyingi.
Polisi wa mwaka jana mbona leo wananchi hawaoni magari ya washawasha wala wenye virungu?
Baada ya muda tunajikuta na swali 'kwanini baadhi ya wananchi wana chuki na vyombo vya usalama''?
Tunaanza kutafuta majibu yasiyokuwepo, tukisahau kujiuliza chuki inajengekaje na kwanini