Polepole amesema kuwa amekutana na mshauri mmoja ambaye anampenda sana Rais Samia, na kwamba wakati wote wa majadiliano yake, yeye Polepole alipotaka kuzielekeza lawama zake kwa Samia, huyo mshauri alikataa kabisa na kusema kuwa Rais Samia ni mtu mzuri sana ila kuna watu waovu ndio wanaomharibia.
Baadaye Polepole akamweleza kuwa kama anayoyasema ni kweli kwa nini asionane na Samia na kumshauri juu ya hao watu wabaya waliomzunguka wenye nia ya kumharibia, kwa maslahi yao binafsi? Ndipo huyo mtu akasema anaenda kuonana na Rais. Baadaye amempa taarifa kuwa alipoenda ikulu amekataliwa kuonana na Samia.
Akaamua kwenda kwa makamu mwenyekiti wa chama Mzee Wasira ili amsaidie kumfanyia appointment, mzee Wasira amekataa. Akaomba basi yeye Wasira amfikishie Samia ushauri wake, Wasira amekataa.
Ni dhahiri kuwa huko ndani ya CCM, huenda kuna watu wanaumia kwa maovu yanayoendelea kuliko tuliopo huku nje.
Mungu azidi kuwajalia ujasiri wale wote wenye dhamira njema na Taifa hili bila ya kujali wapo upande gani.
Kwa namna Samia alivyokuwa ameanza, na ukiangalia yanayoendelea leo, yawezekana kweli kuna waovu wamemzunguka.