Polepole aulizwa: Je, CCM inakiri kuwa ndiyo imetuangusha kama Taifa kwa mikataba mibovu ya madini?

Huyu siyo yule pole pole wa kudai katiba. Sijui wakishangia huko CCM wanapewa kinywagi gani yarabi.
 
KWANZA TV TUMEULIZA:
Kwa kurejea ripoti ya tume iliyoshughulikia sakata la mchanga na kukabidhiwa Rais Magufuli, je, CCM inakiri kuwa ndiyo iliyotuangusha kama Taifa kwa kutuingiza kwenye mikataba mibovu ya madini?
Humphrey Polepole kajibu hivi:


Black politics never admit the shit happened...... at their own wrong
 
Ni kama alivyokuwa anajibu Bashite. Vita ya madawa ya kulevya haijawahi kumwacha mtu salama kwa kila swali,
 
Maswali mepesi kabisa yanawashinda kujibu, mimi ningejibu la hasha, bali baadhi ya viongozi ndani ya ccm ndio waliotufikisha hapa, hoja ingejibiwa vizuri tu vielelezo vikiwepo. Tatizo hawafikirii haya mambo kwa ufasaha wanakuwa emotianal kijuibu maswali ya msingi japo ni mepesi tu.
 
Tunaomba ccm ituombe radhi Watanzania kwa aya yanayotokea maana waho ndio waliyafuga mafisadi na majizi,mikataba mibovu ivyo tunawaomba mutuombe radhi kwanini ccm mpya inaanza kuja kupitia Dr J Pombe our President
 
Tetetete majambazi kila kitu kwao ni makofi sasa makofi yanawageukia chenge wapi


Swissme
 
tafadhar wapendwa naomba anaeweza kuandka au kukieleze alchoksema huyu bwana nataman kujua majbu mana swal la kibabe kwel kwel, kacm kangu akana uwezo wa kufungua vdeo
 
Pole pole naomba nikufundishe jinsi ya kujibu maswali uliyoulizwa kwa kifupi sana.
Swali: Mnakiri kuwa tumefika hapo kwa sababu ya CCM?
Jibu: Ndiyo, lakini tumeamua kujisahihisha ili kusimama imara kwa kutekeleza majukumu kwa kuwahudumia wananchi kiamilifu.
Ungejibu hivo tungekuelewa na tungerudisha imani yetu kwenu.
 
ccm hovyo kabisa, kwamba mkiomba kura na mkizipata mnajifanyia tu mambo hovyo kwa kisingizio eti wananchi ndivyo wanavyotaka, mh kwa hivo je wananchi ndo walisema mwingie mikataba ya kishetani? Richmond, Meremeta, Kagoda, Escrow, hayo yote ni Wananchi si ndiyo.
 
Huo uozo ulifanywa na rais aliyekuwepo na kama ni kukataa lisifanyike basi hata Magufuli alikuwa waziri, je yeye kwenye baraza la mawaziri atuambie alitoa wazo lolote juu ya madini?

CCM wameharibu, halafu vinara wla uharibifu wakimaliza kazi wanapewa hifadhi CHADEMA! Sumaye alikuwa Waziri Mkuu na kiongozi wa serikali bungeni wakati sheria ya kinyonyaji ikipitishwa, na kwa miaka 10 alitulia kwenye kiyoyozi wakati mchanga unasafirishwa.

Mkataba wa mwanzo uliondelezwa kipindi cha JK na Lowassa alikuwa Waziri Mkuu, leo hii yuko CHADEMA anapigania 'demokrasia'?

Mwisho, unaweza kusema usiku wa kusaign mkataba wa Buzwagi Karamagi aliongozana na nani? Tafuta jibu ndio utajua kwanini Lissu anapiga siasa kwenye hii saga ya mchanga. Na bado atapata shida na hivyo vipande 30.
 
Mmmh kumbe hakuna mtu hapo kama vile upepo umekalia kiti.
Basi ngoja tusubiri mwenye akili katika ccm labda atawaza tofauti na kwa aina hii ya akili , No WONDER WHY WE LOSE ALL OUR RESOURCES TO THE WHITES
 
Umetumia vigezo gani vya kumsamehe mwinyi ambavyo havi apply kwa hao wengine

Sidhani kama Mwinyi alikuwa na elimu ama NGUVU za kimawazo za kutosha kuwa Rais, sidhani kama alikuwa ana uwezo wa kuiongoza nchi, waliokuwa wakiiongoza nchi Wakati huo ni wengine kabisa, tungeshitukia Tanzania imekuwa Oman. Kwa ujumla alikuwa Rais kwa jina tu, hakujua la kufanya.

Hawa wawili, haswa Mukapa, anayejiita musomi, anayezungumza kwa authority, nimeshuhudia kwa macho yangu wakati wa mukutano huko Uingereza wa kuondowa njaa Afrika akiwa yeye na TIBAIJUKA, kwa hotuba zao wakisema Afrika ni tajiri lakini inaibiwa left, right, na wote wawili wameonyesha ni viongozi selfish, hawaaminiki, wameonyesha ni wenye tamaa bila kujali wananchi. Baba wa Taifa Nyerere amefariki na UCHUNGU sana kwa dharau Mukapa aliyomuonyesha Wakati akiiuza Benki zetu. Tibaijuka ni mwanamke nilikuwa namuhusudu kwa elimu yake, hata aliposhambuliwa Kenya nakupoteza kazi yake nilifikiri wanamuonea, lakini alipopokea mabilioni ya Watanzania ya account ya Esclow na kwa ujeuri kusema amenunua mboga, niliona Tanzania hatuna Viongozi.


Kikwete alikuwa sio Rais, alikuwa mutalii, mpenda raha, alikuwa hana clue nchi inaongozwa namna gani. Pesa alizotumia kusafili nje ni kama mchanga ulivyokuwa ukiibiwa. Aiikabithi nchi kwa cartels, alituona na kuamini Watanzania ni wajinga. Na kumbuka kuna wakati heshima la polisi lilikuwa likipiga watu bila ya kujali haki zao, kama Rais mpaka nakumba alichosema. ALISEMA aangalieni jamani, hawa watu siku hizi wanajuwa haki zao. Hiyo ndiyo statement ya Rais. Watanzania shida ni kwa kuwa tumegawanyika, wachache sana tunaconfidence, wengi hatuna, tunaona kila kitu ni sawa tu. Wengi tuna ugonjwa mkubwa wa woga., na wengi wanataka kuingia kwenye siasa ili wafanye vitendo vya hawa MARAIS waliopita. Kuiokowa Tanzania forensic audit ya Mali za MARAIS wetu haswa Kikwete na Mkapa na familia zao zingepitiwa. Mali walizonazo ziangaliwe, inawezekana mali walizonazo zatosha kulipa made ni yetu, na wachukuliwe hatuwa. Katiba yetu lazima ibadilishwe, haiwezekani maisha ya Watanzania zaidi ya millions 50 kuwekwa mikononi kwa mtu mmoja ambaye hatuwezi hata kumushitaki akikosea, hii ni katiba ya kikoloni Wakati Wazungu wakitutawala. Ama sivyo miaka ya Rais Magufuli ikiisha tutarudi kule kule even worse.
 
Back
Top Bottom