Polepole, Ati Mbeya ina ukabila, hapa umekanushwa!

masopakyindi

Platinum Member
Jul 5, 2011
17,882
13,172
IMG_20180510_194816.jpg


Kati ya matamko yaliyonikera mimi binafsi, ni lile tamko la Ndg Polepole alipotoka ziarani huko Mbeya.
Vyombo vya habari vilimnukuu akisema viongozi ndani ya mkoa wa Mbeya wana ukabila.

Sijui nini kilimsukuma kusema hivyo maana tuliotoka mkoa huo tupo pamoja katika mambo mengi ya kijamii.
Hata mila na heshima za watu wa mkoa huu zinalingana.

Kitendo cha Prof Mark Mwandosya kumpongeza Mbunge wa Mbeya Mjini Ndg Mbilinyi , ni kitendo ambacho watu wenye mawazo kama ya Humphrey Polepole kitawakanusha na kuwatia soni.
Picha ya Nd Mbilinyi na Prof Mwandosya imeongea mengi.

Wanasaikolojia wameshaanza kuhisi kuwa tamko lile la Polepole ni kutokana na kushindwa katika kile alichokiendea Mbeya.
 
Tanzania nzima kuna ukabila wala huna sababu ya kukataa labda useme ni kwa namna gani tutaupunguza lakini mbona ukiwa kwenye mkoa wenye kabila zaidi ya moja ushindani baina ya kabila na kabila huwa wazi mfano uchaguzi wa Lem arusha kuna vinasaba vya uchaga na umasai viliinuka
Ukienda morogoro yapo tanga yapo mara yapo kagera yapo singida yapo na mbeya yapo pia
 
Sugu ni mnyakyusa kama Mwandosya ...hilo jina la Mbilinyi sio lake amejipachika tu
Usamehewe tu maana hujui ukisemacho.....

Halfu ujuwe Mbeya haina kabila moja tu... TATIZO MNADHANI MTU AKITOKA MBEYA BASI MNYAKYUSA, AKITOKA RUVUMA BASI MNGONI... Mnasahau kuna wamatengo, wamanda, wanyasa, wanindi, wangoni, wayao, wandendeule, wanyasa etc.... Na huko Mbeya kuna wasafya, wandali, wamalila, wanyiha, wanyakyusa etc Tusisahau Tanzania kuna makabila zaidi ya 120...
 
Humphrey Polepole, huijui Mbeya, Na utapata shida sana wewe, CCM, Magurudumu ya gari lako Na Polisi.
Mbeya sio Dodoma.
Mbeya is a home of brave and determined people.
Ni kweli mkuu, wengi wameingia Mbeya kichwa kichwa na vichwa vikawauma.
Kama kuna kitu kibaya Pole pole kafanya ni kucheza na pride ya watu wa mkoa huu.
Huo ujumbe alioupata toka kwa Prof inabidi mzee Mangula aanze kumpa tuition ya siasa, maana anaumbuka.
 
Huyo jamaa kapewa kazi kubwa kuliko uwezo wake. Itikadi inahitaji maneno mengi lakini kuwe na mikakati madhubuti na akili itumike sana.
 
Back
Top Bottom