mechard Rwizile
JF-Expert Member
- Sep 21, 2011
- 1,571
- 875
Ndugu zangu mwacheni Ndugu Polepole aendelee na ujinga wake, simkumbuki katibu mwenezi wa CCM mwenye heshima kwa watu hasa wapinzani. Namkumbuka Mhe. Ramadhan Mapuri, Mhe. Nape Mnauye na sasa ndugu Polepole. Wote walipitiliza, ila wanakuja kugundua baadaye kuwa wapinzani nao ni watanzania na wanauwezo wa kufikiri na kutenda bora kama watu wengine. Hebu mkumbuke Mhe. Nape alivyokuwa anamsema Dr. Wilbroad Peter Slaa, Balozi wa Tanzania Sweden. Kumbuka Prof. Kitila Mkumbo alivyokuwa anapuuzwa. Kumbuka Mama Anna Mghwira alivyokuwa anaonekana wakati ule wa kampeini za urais na sasa akiwa Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro? Kuna wakati najiuliza kuna kitu huwa wanalishwa ( Makatibu waenezi na itikadi wa CCM)?View attachment 776562
Kati ya matamko yaliyonikera mimi binafsi, ni lile tamko la Ndg Polepole alipotoka ziarani huko Mbeya.
Vyombo vya habari vilimnukuu akisema viongozi ndani ya mkoa wa Mbeya wana ukabila.
Sijui nini kilimsukuma kusema hivyo maana tuliotoka mkoa huo tupo pamoja katika mambo mengi ya kijamii.
Hata mila na heshima za watu wa mkoa huu zinalingana.
Kitendo cha Prof Mark Mwandosya kumpongeza Mbunge wa Mbeya Mjini Ndg Mbilinyi , ni kitendo ambacho watu wenye mawazo kama ya Humphrey Polepole kitawakanusha na kuwatia soni.
Picha ya Nd Mbilinyi na Prof Mwandosya imeongea mengi.
Wanasaikolojia wameshaanza kuhisi kuwa tamko lile la Polepole ni kutokana na kushindwa katika kile alichokiendea Mbeya.