Polepole anazungumza sana na watu wanamuelewa ila haeleweki

Elius W Ndabila

JF-Expert Member
Jul 17, 2019
322
645
KWA NINI POLEPOLE HATA AKIELEWEKA HAELEWEKI?

Na Elius Ndabila
0768239284

Mhe Polepole anazungumza sana na watu wanamuelewa ila haeleweki. Mhe Polepole haeleweki kwa kuwa aliyoyatetea akiwa kwenye Vieiti (V8) ndiyo yale anayoyapinga baada ya kuondolewa V8. Hivyo anaonyesha ni mtu ambaye akipewa cheo anakuwa na uwezo tofauti wa kupambanua mambo.

Wiki iliyopita amedai kuwa baada ya Rais kuwa kuna mawaziri hawali urefu wa kamba na ndio maaba wanavimbiwa basi walitakiwa Mawaziri wajitokeze kupinga au kukubali. Hapa Mimi nilimuelewa Polepole kwa kuwa hata Mimi baada ya statement ya Rais nilitoa ushauri wangu. Lakini pamoja na kumuuelewa Polepole bado hakueleweka anata mawaziri Wamuulize Rais ili iweje?

Polepole akiwa Katibu Mwenezi wakati aliyekuwa Rais akihalalisha Rushwa kwa mkutadha wa dawa ya kiatu hakukemea. Tulishuhudia waliopewa uhalali wa kuchukua pesa za dawa za viatu wakikusanya pesa kana kwamba hizo kiwi zitablashi viatu nchi nzima. Siku chache zilizopita kina picha ilitembea ikionyesha sample ya fedha za kublashia viatu ikiwa kwenye gari ya Askari ambaye Kwa tetesi ni kuwa amefukuzwa.

Kama Polepole hakuweza kukemea uhalali na mkutadha ya Polisi kuruhusiwa kuchukua fedha ya dawa ya viatu ambayo ni illigality, anapata wapi authority ya kuwataka Mawaziri wajitokeze kukataa?

Tunakuelewa ila haueleweki.
 
1643622969773.png
 
Back
Top Bottom