PreGE2025 POTOSHI Polepole amesema ACT ni mali CCM na CHAUMMA inafadhiliwa na CCM

PreGE2025 POTOSHI Polepole amesema ACT ni mali CCM na CHAUMMA inafadhiliwa na CCM

Mijadala ya Uchaguzi Mkuu wa Tanzania 2025 (Kabla)
Uhalisia wa taarifa hii umepindishwa ili kupotosha
Source #1
View Source #1
Wakuu ni kwamba mimi kuna kipande kilinipita ama vipi? Je ni kweli Humphrey Polepole alitamka maneno haya?

Fatma Vs Polepole Agosti 08.jpg
fATMA jaMBO Agost 08.jpg
 
Tunachokijua
Madai

Agosti 08, 2025 mtumiaji mmoja wa mtandao wa X alichapisha Taarifa iliyoambata na video ya aliyekuwa Balozi wa Tanzania nchini Cuba, Humphrey Polepole na kuandika

“Aisitii ni Mali ya CCM na Chaumwa inafadhiliwa na CCM” na kudai kuwa maneno hayo yametamkwa na Polepole katika mazungumzo yake aliyoyafanya Agosti 08, 2025 kupitia mitandao mbalimbali ya kijami.

Uhalisia wa Taarifa hiyo

Ufuatiliaji uliofanywa na JamiiCheck umejirirdhisha kuwa Taarifa hiyo inapotosha uhalisia.

Taarifa hiyo iliyochapishwa katika mtandao wa X na mtumiaji huyo inapotosha uhalisia wa kile alichokisema Humphrey Polepole katika mazungumzo yake ya Agosti 08, 2025. Maneno hayo yanakinzana pia na video iliyoambatanishwa pamoja na Taarifa hiyo.

Mtumiaji huyo alikuwa akirejelea maneno aliyoyatoa Humphrey Polepole ambapo katika mazungumzo yake alihoji kuwa Rais Samia Suluhu anataka kwenda kwenye uchaguzi kushindana na Luhaga Mpina wa ACT Wazalendo pamoja Salum Mwalimu wa CHAUMMA?

Polepole alisema “Simama ile njia ambayo umepewa, heshima yako ibaki lakini unataka ulazimishe? Ukagombee na Salum Mwalim wa CHAUMMA? Unapa amani ya moyo ukagombee na Salum Mwalimu, Unapata kabisa manai ya moyo mama? Unapata kabisa amani ya moyo ukagombee na Luhaga Mpina wa ACT kweli?

Kwanini sisi CCM hatuijui ACT? Hatuijui ACT? Mimi sisemi habari za ACT ndiyo hao unataka ukagombee nao Urais? Luhaga Mpina ACT pamoja na Salum Mwalimu wa CHAUMMA ndiyo unataka uchaguzi uwe namna hii na unahisi utapata uhalali wa kuongoza kwenye nchi yetu? Kataa mama Samia."
Jamii Chek hamjajibu kitu, mmerudia tu maneno ya Balozi Polepole.
Sasa kama habari hiyo ni potoshi, nini uhalisia wake?
 
Mbona mmeandika Potosi wakati wenye chama chao wanatoa taarifa wanazozijua wao inakuaje ninyi Wazee mpinge tena..
 
Back
Top Bottom