Polepole alikataa kuwa DC sasa auvalia suti

Ha haaa haaaaa.. . Mkuu huyu jamaa ni noma.... Cameron pamoja ya kuwa muda wake wa kuwa waziri mkuu wa UK haujaisha, lakini kajiudhuru kutunza kile anacho kiamini.... Polepole hawezi kuishi yale anayo yahubiri na kuyaamini......
Ni kiongozi gani wa upande wa pili anayeyaishi maneno yake. Si mda mrefu karibia wote waliyapuuza maneno yao kisa njaa.

Hakuna mwanasiasa anayetanguliza masrahi ya mtu mwingine badala ya masrahi yake kwanza. Acheni ajitengenezee jina katika medani za siasa. Au yeye hapaswi kugraduate toka kuwa mwanaharakati na kuwa mwasiasa kama wengine? Mwacheni apigiwe saruti bwana.
 
Wana jamvi tutakumbuka ni jinsi gani Polepole alivyokuwa anapinga nafasi za wakuu wa wilaya kwa kuisimamia rasimu ya katiba ya jaji warioba, alienda mbali zaidi kwa kusema kuwa vyeo hivyo ni vya kupoteza fedha! Sasa nashangaa kuvalia suti kuingia ofisi hiyo hiyo baada ya kupewa nafasi hiyo na mh rais magufuri, je tuendelee kumwamini polepole?View attachment 365900
Yaani hapa nimeshikwa na hasira hadi nimeshindwa la kusema kwani huenda nyumba yangu ikapewa ulinzi wa bure.
 
Siasa hazina maana, Yericko, Mnyika na Lema jinsi walivyomtukana Lowassa usingeamini kuwa leo wapo pamoja.

Umewasahau wengi, wapo akina Lissu, kubenea, Mbowe na hili la Sumaye vs Lowassa sumaye aliwahi kusema hawezi kaa meza moja na fisadi Lowassa. Sasa sijui wote hawa na wengine wa namna hii nao tuendelee kuwaamini? Bora huyu aliyekuwa anaongelea rasimu ya katiba ambbayo yalikuwa mapendekezo tu, kuliko hawa waliokuwa wanajiapisha
 
taifa la wanaoongea tu bila kufikiri

Polepole ndie alipigania katiba ya wananchi kuliko mtu yeyote yule

ile katiba ilikuwa pendekezwa na haikupita

ile katiba wapinzani walitaka serikali mbili...ila hazijatokea na hatujasikia mpinzani akisema hataki uongozi kwa sababu serikali ni tatu

kuna mengi ambayo kama tutaamua kuishi kwa maamuzi yetu au misimamo yetu hatutautendea haki upande wa pili...

halafu angeukataa huo u a DC asingewekwa mwingine kwa sababu polepole kagoma??

be genuine
 
Wana jamvi,

Tutakumbuka ni jinsi gani Polepole alivyokuwa anapinga nafasi za Wakuu wa Wilaya kwa kuisimamia rasimu ya katiba ya Jaji Warioba, alienda mbali zaidi kwa kusema kuwa vyeo hivyo ni vya kupoteza fedha! Sasa nashangaa kuvalia suti kuingia ofisi hiyo hiyo baada ya kupewa nafasi hiyo na mh. rais Magufuli, je tuendelee kumwamini Polepole?View attachment 365900
Ndugu!! Mkono usioweza kuukata ulambe.
 
Wana jamvi,

Tutakumbuka ni jinsi gani Polepole alivyokuwa anapinga nafasi za Wakuu wa Wilaya kwa kuisimamia rasimu ya katiba ya Jaji Warioba, alienda mbali zaidi kwa kusema kuwa vyeo hivyo ni vya kupoteza fedha! Sasa nashangaa kuvalia suti kuingia ofisi hiyo hiyo baada ya kupewa nafasi hiyo na mh. rais Magufuli, je tuendelee kumwamini Polepole?View attachment 365900
Njaa haina baunsa mjomba , huyu muda si mrefu utasikia akiamrisha polisi wamkamate Kubenea !
 
Back
Top Bottom