Dr Adam Francis
JF-Expert Member
- Aug 12, 2011
- 464
- 687
Katika desturi za kimahakama, uamuzi ukisha fikiwa baina ya watu wawili kuhusu shauri fulani, mahakama hiyo hiyo hairuhusiwi tena kurudia kulisikiliza shauri hilo hilo baina ya watu hao hao tena. Hiyo ndio maana ya Res judicata.
Sasa hivi CCM tayari tuna mgombea urais, Dkt Samia, mchakato majimboni umepamba moto, uteuzi wa madiwani ndio unaelekea tamati. Ni ukweli uliowazi kuwa sasa haiwezekani kurudia huu mchakato. Kupinga uamuzi wa mkutano mkuu kumteua Dkt Samia sasa hivi ni usaliti. Samia ni mgombea wa CCM na wana CCM wote lazima tumtetee.
Ni ukweli, kukosoa, kujikosoa na kukosoana ni nyenzo ya mapinduzi, lakini wakati gani, mahali gani na kwa njia gani hilo linafanyika ni jambo la muhimu pia. Hili lisipozingatiwa tutashindwa kutofautisha kati ya kukosoana na kushambuliana.
Jambo la muhimu kwa sasa ni kuona ni namna gani tutavuka kivuko cha uchaguzi bila kupoteza umoja wa kitaifa, amani na utulivu wetu.