Poleni Wanafunzi Mliokosa nafasi za kujiunga na vyuo vikuu 2017/2018

Samba

Member
Nov 24, 2013
74
65
Hivi kweli TCU NA Serikali hamjaona watoto wanavyoteseka na kukosa nafasi vyuoni? Kweli Elimu siyo priority I can see!!!!
 
Dah.... Wakato mwingine analia kukosa mkopo mwingine hata admission anakosa...
Mungu awape moyo wa uvumilivu wote waliokosa admission
 
Hivi kweli TCU NA Serikali hamjaona watoto wanavyoteseka na kukosa nafasi vyuoni? Kweli Elimu siyo priority I can see!!!!
Sio lazima kila mtu asome chuo kikuu. Wengine wakasome vyuo vya 'size yao'. Msitake tuanze kusema kuwa waliokosa vyuo ni vilaza ili mtuelewe. Serikali haiwezi kupoteza pesa kusomesha vilaza. Bora hizo pesa tuziweke tuje kusomeshea vichwa watakaojiunga vyuo mwakani!
 
Ungefafanua wamekosaje. walikuwa na sifa ila wameachwa au hawakuwa na sifa kulingana na vigezo volivyowekwa
 
Kuna mdogo wangu kapata One pointi 7 PCB Dogo alikuwa na ambition ya kuwa Daktari kakosa chuo Bugando na Muhimbili yaani yupo tu Nyumbani na kasema hawezi kusoma Course nyingine tofauti na hiyo
 
Asikate tamaa awe mvumilivu ndoto yake itatimia mwakani siyo mbali atapata tu
 
Poleni sana vijana.

Nadhani wengi wenye sifa waliokosa ni wale waliokomalia vyuo vyenye "majina" wakiamini kwakuwa wana sifa basi lazima wapate!
 
Serikali imeshindwa vibaya sana kwenye hili. Pamoja na kubana matumizi na kama wanavyodai wenyewe kuongeza makusanyo ya mapato ya kodi 2017/2018 wametoa 32% ya mikopo iliyotolewa 2015/2016.

Mikopo ya 2015/2016 ilikuwa 459 billions kwa wanafunzi 122,000 2017/2018 mikopo ni 147 billions tu kwa wanafunzi 31,000!!!! Yuko busy kuinyoosha nchi!!!

Hivi kweli TCU NA Serikali hamjaona watoto wanavyoteseka na kukosa nafasi vyuoni? Kweli Elimu siyo priority I can see!!!!
 
Poleni sana vijana.

Nadhani wengi wenye sifa waliokosa ni wale waliokomalia vyuo vyenye "majina" wakiamini kwakuwa wana sifa basi lazima wapate!
Hapo sasa, kuna haja ya vijana akupewa mwongozo wa namna ya kuchagua chuo na fani husika, kwa kuangalia ufaulu wake na ushindani uliopo katika kazi husika, lakini pia wazazi wengi wengi wanatamani watoto wao wangechaguliwa katika vyuo vya maeneo wanayoishi ili kuepuka gharama wawapo maeneo ya mbali matokeo yake ni kukosa kabisa chuo
 
dah!hii ishu inawagharimu wengi hata mwaka jana wapo waliokosa vyuo kwakukomaa na vyuo vyenye majina wakasahau ushindani na ufaulu
 
Na si hilo tu asilimia kubwa pia wameingia katika fani ambazo sio ndoto zao ni ili mradi amepata nafasi chuo sijui nini kifanyike
 
Sio lazima kila mtu asome chuo kikuu. Wengine wakasome vyuo vya 'size yao'. Msitake tuanze kusema kuwa waliokosa vyuo ni vilaza ili mtuelewe. Serikali haiwezi kupoteza pesa kusomesha vilaza. Bora hizo pesa tuziweke tuje kusomeshea vichwa watakaojiunga vyuo mwakani!
1.8 PCB ni kilaza?
 
Serikali imeshindwa vibaya sana kwenye hili. Pamoja na kubana matumizi na kama wanavyodai wenyewe kuongeza makusanyo ya mapato ya kodi 2017/2018 wametoa 32% ya mikopo iliyotolewa 2015/2016.

Mikopo ya 2015/2016 ilikuwa 459 billions kwa wanafunzi 122,000 2017/2018 mikopo ni 147 billions tu kwa wanafunzi 31,000!!!! Yuko busy kuinyoosha nchi!!!
Kuna watu sijui kwanini Mungu hawachukui????
Situation kama hizi ndo watu huwa wanakuwa wapinga uwepo wa hizi imani. Inakuwaje mtu mmoja anaetesa maisha ya wengi especially wanyonge wasio na msaada anaishi tu mpaka miaka 90 while wale walio mstari wa mbele kwaajili ya wengine wanaweza dumu au potea katika umri ambao bado wanahitajika
 
Mwaka huu malalamiko ya kukosa vyuo kwa wenye sifa ni makubwa mnooo.
Inauma zaidi pale unaona chuo qualification ni 1.6 lakini mtu wa 2.10 amechukuliwa.
Mwingine unafanya application mpaka mara tatu chuo kimoja ndo unakuja kupata admission na kumbuka kila application unalipia.
Hii system ni Mbovu.
 
Back
Top Bottom