Pole sana Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

Pole sana Rais Mstaafu Jakaya Kikwete

Baada ya ule Waraka wa Kinana kwani bado hujawajua wanaomtuma Musiba?

Mbona wameshajitokeza tayari...

labda nyie ndio mkioneshwa Mkia wa Mbuzi ulipoanzia bado unauliza KINYEO kiko wapi!
 
*Pole sana Rais Mstaafu Jakaya Kikwete*

Kwa siku nne sasa kumekuwa na sintofahamu katika siasa za chama tawala Tanzania (CCM) baada ya kuvuja kwa mawasiliano ya simu kati ya Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Mtama Ndg. Nape Nnauye wakipanga mipango ya namna ya kutekeleza mkakati wa sambaza barua ya Makatibu Wakuu Wastaafu Ndg. Kinana na Ndg. Yusuf Makamba kwa Baraza la Viongozi Wastaafu linaloongozwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi.

Barua hiyo imezua gumzo katika siasa za Tanzania kwa kudai mwanaharakati Cyprian Musiba anatumwa na viongozi wenye mamlaka makubwa na wenye kinga ili kuwachafua. Bila kificho barua hii inaonekana waziwazi kuwa inamtuhumu Rais John Pombe Magufuli.

Kwa namna mjadala unavyokwenda haina mashaka kuwa Ndg. Kinana na Kijana wake Nape wameonesha wazi kufanya hujuma dhidi ya uongozi wa sasa wa Rais John Magufuli.

Ni hujuma kwa sababu jambo walilolifanya halikuzingatia utaratibu wa Chama na dhamira yao imeonesha wazi kuwa ilikuwa kuzimwaga shutuma hizo hadharani ili kuibua hasira za wananchi hasa wana CCM dhidi ya uongozi.

Kwamba hawakutaka kuwasiliana na viongozi wa chama kwa utamaduni wa Chama bali kwa uharamia. Kwa vyovyote vile barua hiyo waliyoimwaga kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari walivyovichagua na ambavyo vimekuwa vikitoa kipaumbele kwa habari hasi dhidi ya Chama na Serikali ya Rais Magufuli haikuwa na nia njema.

Imekuwa ni aibu ya wazi na watu wana kiu ya kujua watatoka vipi kuonesha nyuso zao mbele ya Watanzania wenye mapenzi na kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Rais Magufuli na CCM inayoongozwa na Dk. John Magufuli akiwa Mwenyekiti wake.

Imekuwa mbaya zaidi siku mbili baadaye baada ya kuvuja kwa sauti zingine za Nape Nnauye akiongea na Mbunge wa Sengerema Mhe. William Ngeleja katika muktadha huo huo wa kuulalamikia uongozi wa chama na Serikali chini ya Rais Magufuli. Ni aibu nyingine kubwa kwa mazungumzo yale kuvuja. Ngeleja nae akionesha kuuponda uongozi wa Rais Magufuli na kushabikia barua iliyoandikwa na Ndg. Kinana na Ndg. Makamba.

Kuvuja kwa mazungumzo haya kumezua gumzo kubwa sana, na imeonekana wazi kumbe wapo viongozi wakubwa wanaoendesha mapambano ya kumhujumu Rais Magufuli na imeleta watu kuamini kuwa maneno yanayosemwa na Cyprian Musiba yana ukweli.

Kwa wengi waliofuatilia sakata hili wamepata ujumbe mmoja mkubwa kuwa hawa viongozi waliohusika wanaonekana kuwa wazoefu wa mchezo huu. Na kama ndivyo basi hawajaanza leo, wameanza zamani.

Wengi imewakumbusha mvurugano wa viongozi na madhara makubwa ambayo yalikipata Chama na Serikali wakati wa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Dk. Jakaya Kikwete.

Ndg. Kinana, Ndg. Makamba, Ndg. Nape na Ndg. Ngeleja wote walikuwa viongozi wakubwa walioshika nafasi za Katibu Mkuu wa CCM, Waziri, Mkuu wa Mkoa na Wajumbe wa vikao vikuu vya Chama yaani Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu.

Hawa ndio walikuwa miongoni mwa washauri muhimu wa Rais Mstaafu Kikwete. Na hawa ndio waliokuwa na ushawishi mkubwa hadi Rais Kikwete alipokabidhi madaraka.

Kwa tabia hii waliyoionesha ndio maana Serikali ya Awamu ya Nne ilijikuta ikikumbwa na kashfa mbalimbali, halikadhalika kashfa ndani ya CCM.

Ni wakati wao ambapo kulizuka kashfa zilizosababisha kujiuzulu Waziri Mkuu Edward Lowassa, kujiuzulu Mawaziri kwa sababu mbalimbali ambazo wengi tunazifahamu, kutukuzwa kwa ufisadi mkubwa wa ndani na nje ya chama, matumizi mabaya ya mali na fedha za chama na mwisho mwa uongozi wa Rais Mstaafu Kikwete kukatokea funga kazi ya tukio la aibu la wajumbe NEC kuimba wimbo wa “Tuna imani na Lowassa” kwa lengo la kushinikiza kikao kimpitishe Edward Lowassa kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu wa 2015, tena wakiimba mbele ya Mwenyekiti wao na wajumbe wa Kamati Kuu.

Kwa hivyo, leo kwa sauti hizi zinazoonesha uhaini wa hali ya juu na mipango michafu dhidi ya Rais Magufuli ni mwendelezo wa tabia zilezile za kuwepo makundi ya wana CCM ambao kazi yao ni kupika mikakati ovu ya kutimiza matakwa yao, lakini sasa wamekutana na kisiki cha mpingo WAMEUMBUKA.

Kwa hali hii Rais Mstaafu Kikwete anastahili kupewa pole nyingi sana kwa kuongoza nchi akiwa na watu ambao wanamsaliti kwa muda wote wa miaka kumi ya uongozi wake.

Ni watu aliowaamini lakini kumbe walikuwa na maslahi yao tofauti yaliyofanya Chama na Serikali kuchukiwa na wananchi. Yaliyosababisha hatari ya CCM kung’olewa madarakani mwaka 2015.

Pole sana Rais Mstaafu Kikwete kwa sababu sasa tumewajua waliofanya ukawa unatukanwa kila mahali kwamba wewe ni kiongozi dhaifu.

Pole sana Baba Kikwete kwa sababu sasa tumewajua waliojifanya wasaidizi wako kumbe waliandaa mpango wa kukuzomea kule Dodoma mbele ya waandishi wa habari wakitaka Lowassa awe Rais baada yako, kinyume na utaratibu wa chama.

Pole sana Mzee wetu Kikwete kwa sababu sasa tumewajua waliosababisha wana CCM kuogopa kuvaa sare za CCM kwa kuhofu kupopolewa mawe na watu waliodai chama hiki kimechoka na kinapaswa kuondoka madarakani.

Pole sana Rais Mstaafu Kikwete kwa kukaa na watu ambao walijifanya wema kwako kumbe wapigaji wakubwa. Na sasa wanaumbuka baada ya Rais Magufuli kuchukua hatua bila kumuonea haya mtu yeyote. Kuziba mianya ya wizi na upiga dili.

Pumzika Rais wetu Mstaafu Kikwete kwa sababu sasa Watanzania wamejua kosa halikuwa lako na wamewajua waliokuwa wanakuhujumu na kuharibu mipango na malengo yako makubwa kwa ajili ya Tanzania.

Nawapongeza watu waliofanikisha kufichua mipango hii miovu dhidi ya nchi yetu. Kwa hakika wamefanya kazi nzuri sana kwa sababu angalau sasa Watanzania wanajua nani Kondoo na nani Chui.

Nawasihi wenye uwezo wa kiteknolojia ya kuwafichua watu wanaojifanya wana heshima kubwa, ama wazito ama wana uchungu na nchi hii kumbe maharamia wakubwa, waendelee kufanya hivyo ili nchi ibaki kuwa safi na Rais Magufuli na Serikali yake waachwe waendelee kufanya kazi nzuri wanayoendelea nayo.

Tunataka kuona reli sio tu ya kati bali pia ya kusini Lindi, Mtwara na Ruvuma. Tunataka kuona umeme ukiwaka kila mahali, barabara za lami, maji ya kutosha, huduma za afya, elimu bora na kilimo kikikua na mengine mengi.

Tunataka kuona nidhamu ya Serikali inakuwepo na Watanzania wanapata huduma muhimu na sio kuwatukuza watu wachache wanaojiona wao ndio vigogo wa nchi na wana uwezo wa kufanya chochote.

Tunataka kuona chama kilichoachwa na Hayati Mwl. Nyerere, chama cha Watanzania wote, chama cha wafanyakazi na wakulima kinatekeleza hasa malengo yaliyokusudiwa na sio kuwa chama cha wapiga dili na kuwaomumiza wanyonge.

Mwisho niwatakie jioni njema.

Ni mimi Mzee Yusuf Makali Jumbe,
Naishi Kinondoni Dar es salaam
Leo tarehe 19.07.2019

Sawa, binafsi nimekusikia ...umeandika vizuri kabisa...Ila tumpe pole pia Rais Magufuli kwa pressure anayopata kutoka kwenye mijitu hii iliyozoea makundi, ubinafsi, upendeleo, ufisadi, wizi na ambayo yanaendelea kumshinikiza Rais wetu atoke kwa mstari sahihi...mijitu hii ni ya kutimuliwa ndani ya chama na ikibidi iswekwe ndani...
 
Akina Kinana,Nape na Membe tuwaiteje sasa mkuu.

Kuna mtu ameandika mahali humu JF kuwa kuna watu midomo ni mikubwa kuliko ubongo na kwamba eti matumbo yao ni makubwa kuliko nchi yetu...nilicheka sana kwa kweli...dah...
 
Pale Magu na wapambe wake wanapojiandikia barua wenyewe kutengeneza taswira isiyokuwepo, hii game iishe haraka tuone tukio litakalofuata litahusu kitu gani.
Pole kwa victims wa huu mchezo mchafu kwani hatuna mwenye muda wa kutaka kujua ukweli hasa ni upi bali kila mtu anatiririka na muelekeo wa upepo, jamaa yupo radhi hata maraisi wastaafu wachafuliwe bora njia yake izidi kuwa nyeupe na grip yake kwenye chama izidi kuwa firm.
Nakumbuka usemi wa visionary mmoja kuwa 'akimalizana na sisi atakuja kumalizana nanyi pia', waliona kama anaongea ngojera.
The big question is who is next?
Ila Jiwe ana akili nyingi kuliko watu wanavyomdhania, kila mtu kawa muoga. Imagine wazee hao wastaafu kila mtu anawaruka, bingwa wa goli la mkono naye linamtokea puani. Hii ndiyo tunaita shukrani ya punda ni mateke.
 
Jibu swali,matusi hayasaidii sana.
 
Aliyaendika hawazi kuwa mzee. Wazee niwajuao mimi hawaandiki upupu kama huu. Anyway ungeweka na namba yako ya simu
 
Upumbavu ni mzigo mzito! Mleta mada ni mpumbavu wa kiwango cha Phd!

Suala ni dogo tu, ni kwanini Musiba hakamatwi na kuhojiwa kwa kutukana watu? Ni nani anayemlinda na kumfadhili?!
 
Pale Magu na wapambe wake wanapojiandikia barua wenyewe kutengeneza taswira isiyokuwepo, hii game iishe haraka tuone tukio litakalofuata litahusu kitu gani.
Pole kwa victims wa huu mchezo mchafu kwani hatuna mwenye muda wa kutaka kujua ukweli hasa ni upi bali kila mtu anatiririka na muelekeo wa upepo, jamaa yupo radhi hata maraisi wastaafu wachafuliwe bora njia yake izidi kuwa nyeupe na grip yake kwenye chama izidi kuwa firm.
Nakumbuka usemi wa visionary mmoja kuwa 'akimalizana na sisi atakuja kumalizana nanyi pia', waliona kama anaongea ngojera.
The big question is who is next?
Ila Jiwe ana akili nyingi kuliko watu wanavyomdhania, kila mtu kawa muoga. Imagine wazee hao wastaafu kila mtu anawaruka, bingwa wa goli la mkono naye linamtokea puani. Hii ndiyo tunaita shukrani ya punda ni mateke.

Sijatukana popote pale...siyo kawaida yangu kutukana...sijalelewa hivyo...
 
Hata mimi ukinisema hadharani,nitakujibu hadharani.Msiba anachafua watu hadharani kwa kuita waandishi wa habari,halafu we unataka wakajitetee vichochoroni,kwanini huyo Msiba asianze yeye kupeleka malalamiko yake ndani ya chama?si anayo kadi ya CCM?tena aliwahi gombea ubunge?so anajua taratibu,why mnamuacha anazivunja?Ukisoma ule waraka wa wazee hilo ndilo tatizo lao,kwamba wanachafuliwa na mtu hadharani(ccm mwenzao anavunja taratibu)halafu chama kiko kimya!anaeshitakiwa mahakamani,atajitetea mahakamani,mmeacha wachafuliwe mbele ya jamii,na nyie subirini wajibu mapigo mbele ya jamii watz wote tujue mbivu na mbichi.tena ina faida kwetu wananchi.
 
*Pole sana Rais Mstaafu Jakaya Kikwete*
Kwa siku nne sasa kumekuwa na sintofahamu katika siasa za chama tawala Tanzania (CCM) baada ya kuvuja kwa mawasiliano ya simu kati ya Katibu Mkuu Mstaafu wa CCM Ndg. Abdulrahman Kinana na Mbunge wa Mtama Ndg. Nape Nnauye wakipanga mipango ya namna ya kutekeleza mkakati wa sambaza barua ya Makatibu Wakuu Wastaafu Ndg. Kinana na Ndg. Yusuf Makamba kwa Baraza la Viongozi Wastaafu linaloongozwa na Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassan Mwinyi.
Barua hiyo imezua gumzo katika siasa za Tanzania kwa kudai mwanaharakati Cyprian Musiba anatumwa na viongozi wenye mamlaka makubwa na wenye kinga ili kuwachafua. Bila kificho barua hii inaonekana waziwazi kuwa inamtuhumu Rais John Pombe Magufuli.
Kwa namna mjadala unavyokwenda haina mashaka kuwa Ndg. Kinana na Kijana wake Nape wameonesha wazi kufanya hujuma dhidi ya uongozi wa sasa wa Rais John Magufuli.
Ni hujuma kwa sababu jambo walilolifanya halikuzingatia utaratibu wa Chama na dhamira yao imeonesha wazi kuwa ilikuwa kuzimwaga shutuma hizo hadharani ili kuibua hasira za wananchi hasa wana CCM dhidi ya uongozi.
Kwamba hawakutaka kuwasiliana na viongozi wa chama kwa utamaduni wa Chama bali kwa uharamia. Kwa vyovyote vile barua hiyo waliyoimwaga kwenye mitandao ya kijamii na vyombo vya habari walivyovichagua na ambavyo vimekuwa vikitoa kipaumbele kwa habari hasi dhidi ya Chama na Serikali ya Rais Magufuli haikuwa na nia njema.
Imekuwa ni aibu ya wazi na watu wana kiu ya kujua watatoka vipi kuonesha nyuso zao mbele ya Watanzania wenye mapenzi na kazi nzuri inayofanywa na Serikali ya Rais Magufuli na CCM inayoongozwa na Dk. John Magufuli akiwa Mwenyekiti wake.
Imekuwa mbaya zaidi siku mbili baadaye baada ya kuvuja kwa sauti zingine za Nape Nnauye akiongea na Mbunge wa Sengerema Mhe. William Ngeleja katika muktadha huo huo wa kuulalamikia uongozi wa chama na Serikali chini ya Rais Magufuli. Ni aibu nyingine kubwa kwa mazungumzo yale kuvuja. Ngeleja nae akionesha kuuponda uongozi wa Rais Magufuli na kushabikia barua iliyoandikwa na Ndg. Kinana na Ndg. Makamba.
Kuvuja kwa mazungumzo haya kumezua gumzo kubwa sana, na imeonekana wazi kumbe wapo viongozi wakubwa wanaoendesha mapambano ya kumhujumu Rais Magufuli na imeleta watu kuamini kuwa maneno yanayosemwa na Cyprian Musiba yana ukweli.
Kwa wengi waliofuatilia sakata hili wamepata ujumbe mmoja mkubwa kuwa hawa viongozi waliohusika wanaonekana kuwa wazoefu wa mchezo huu. Na kama ndivyo basi hawajaanza leo, wameanza zamani.
Wengi imewakumbusha mvurugano wa viongozi na madhara makubwa ambayo yalikipata Chama na Serikali wakati wa uongozi wa Serikali ya Awamu ya Nne ya Dk. Jakaya Kikwete.
Ndg. Kinana, Ndg. Makamba, Ndg. Nape na Ndg. Ngeleja wote walikuwa viongozi wakubwa walioshika nafasi za Katibu Mkuu wa CCM, Waziri, Mkuu wa Mkoa na Wajumbe wa vikao vikuu vya Chama yaani Kamati Kuu, Halmashauri Kuu na Mkutano Mkuu.
Hawa ndio walikuwa miongoni mwa washauri muhimu wa Rais Mstaafu Kikwete. Na hawa ndio waliokuwa na ushawishi mkubwa hadi Rais Kikwete alipokabidhi madaraka.
Kwa tabia hii waliyoionesha ndio maana Serikali ya Awamu ya Nne ilijikuta ikikumbwa na kashfa mbalimbali, halikadhalika kashfa ndani ya CCM.
Ni wakati wao ambapo kulizuka kashfa zilizosababisha kujiuzulu Waziri Mkuu Edward Lowassa, kujiuzulu Mawaziri kwa sababu mbalimbali ambazo wengi tunazifahamu, kutukuzwa kwa ufisadi mkubwa wa ndani na nje ya chama, matumizi mabaya ya mali na fedha za chama na mwisho mwa uongozi wa Rais Mstaafu Kikwete kukatokea funga kazi ya tukio la aibu la wajumbe NEC kuimba wimbo wa “Tuna imani na Lowassa” kwa lengo la kushinikiza kikao kimpitishe Edward Lowassa kuwa mgombea Urais kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu wa 2015, tena wakiimba mbele ya Mwenyekiti wao na wajumbe wa Kamati Kuu.
Kwa hivyo, leo kwa sauti hizi zinazoonesha uhaini wa hali ya juu na mipango michafu dhidi ya Rais Magufuli ni mwendelezo wa tabia zilezile za kuwepo makundi ya wana CCM ambao kazi yao ni kupika mikakati ovu ya kutimiza matakwa yao, lakini sasa wamekutana na kisiki cha mpingo WAMEUMBUKA.
Kwa hali hii Rais Mstaafu Kikwete anastahili kupewa pole nyingi sana kwa kuongoza nchi akiwa na watu ambao wanamsaliti kwa muda wote wa miaka kumi ya uongozi wake.
Ni watu aliowaamini lakini kumbe walikuwa na maslahi yao tofauti yaliyofanya Chama na Serikali kuchukiwa na wananchi. Yaliyosababisha hatari ya CCM kung’olewa madarakani mwaka 2015.
Pole sana Rais Mstaafu Kikwete kwa sababu sasa tumewajua waliofanya ukawa unatukanwa kila mahali kwamba wewe ni kiongozi dhaifu.
Pole sana Baba Kikwete kwa sababu sasa tumewajua waliojifanya wasaidizi wako kumbe waliandaa mpango wa kukuzomea kule Dodoma mbele ya waandishi wa habari wakitaka Lowassa awe Rais baada yako, kinyume na utaratibu wa chama.
Pole sana Mzee wetu Kikwete kwa sababu sasa tumewajua waliosababisha wana CCM kuogopa kuvaa sare za CCM kwa kuhofu kupopolewa mawe na watu waliodai chama hiki kimechoka na kinapaswa kuondoka madarakani.
Pole sana Rais Mstaafu Kikwete kwa kukaa na watu ambao walijifanya wema kwako kumbe wapigaji wakubwa. Na sasa wanaumbuka baada ya Rais Magufuli kuchukua hatua bila kumuonea haya mtu yeyote. Kuziba mianya ya wizi na upiga dili.
Pumzika Rais wetu Mstaafu Kikwete kwa sababu sasa Watanzania wamejua kosa halikuwa lako na wamewajua waliokuwa wanakuhujumu na kuharibu mipango na malengo yako makubwa kwa ajili ya Tanzania.
Nawapongeza watu waliofanikisha kufichua mipango hii miovu dhidi ya nchi yetu. Kwa hakika wamefanya kazi nzuri sana kwa sababu angalau sasa Watanzania wanajua nani Kondoo na nani Chui.
Nawasihi wenye uwezo wa kiteknolojia ya kuwafichua watu wanaojifanya wana heshima kubwa, ama wazito ama wana uchungu na nchi hii kumbe maharamia wakubwa, waendelee kufanya hivyo ili nchi ibaki kuwa safi na Rais Magufuli na Serikali yake waachwe waendelee kufanya kazi nzuri wanayoendelea nayo.
Tunataka kuona reli sio tu ya kati bali pia ya kusini Lindi, Mtwara na Ruvuma. Tunataka kuona umeme ukiwaka kila mahali, barabara za lami, maji ya kutosha, huduma za afya, elimu bora na kilimo kikikua na mengine mengi.
Tunataka kuona nidhamu ya Serikali inakuwepo na Watanzania wanapata huduma muhimu na sio kuwatukuza watu wachache wanaojiona wao ndio vigogo wa nchi na wana uwezo wa kufanya chochote.
Tunataka kuona chama kilichoachwa na Hayati Mwl. Nyerere, chama cha Watanzania wote, chama cha wafanyakazi na wakulima kinatekeleza hasa malengo yaliyokusudiwa na sio kuwa chama cha wapiga dili na kuwaomumiza wanyonge.
Mwisho niwatakie jioni njema.
Ni mimi Mzee Yusuf Makali Jumbe,
Naishi Kinondoni Dar es salaam
Leo tarehe 19.07.2019
. Hakuna kipya ulicho andika, sana umeongeza pumba.
 
Akina Kinana,Nape na Membe tuwaiteje sasa mkuu.

Hawa ndiyo wasaliti wakuu, kwani wao ndiyo walifunga lile la mkono mpaka jiwe akajikuta kapata ushindi feki, ushindi feki wa mtawala lazima utawala wake uambatane na laana ama majanga kama unavyoona hali ilivyo kwa sasa
 
Halafu mkiitwa washamba mnakuwa wakali!
 
Umesahau kuweka namba yako ya simu
 
Weka na namba ya simu hapo chini unaweza ukateuliwa mzee wangu
 
Hivi wewe na akili unamsifia mwizi wa matilioni ,mfunga watu kwenye viroba ,anayedhuluma wakulima wa korosho ,mbaazi .Anayedhulumu haki za wafanyakazi ,anayefungulia watu kesi za visasi za kubambika za uhujumu uchumi ,anayeteua vilaza kuwa wakuu wa wilaya na mikoa .
 
Back
Top Bottom