Pole sana dada

Pole sana dada

Eiyer

JF-Expert Member
Joined
Apr 17, 2011
Posts
28,259
Reaction score
20,914
Tukio lililotokea siku sio nyingi huko Uganda na kusambaa kutokana na maendeleo ya mawasiliano limewastua wengi hasa wanawake kwakuwa ni wazazi,lakini hata wanaume nao limewastua sana na kupelekea kuanza kuwa na hofu kuhusu usalama wa watoto wao ambao wanalelewa na hawa ma housegirl.

Tukio hili kwa bahati mbaya sana watu wamelitazama kwa upande mmoja tu na hii inasababishwa na tabia ya kibinadamu ya umimi,nasema hivyo kwasababu kwa sasa najua kuna namba kubwa sana ya watu ambayo in amuona yule dada kama mnyama na hastahili kabisa kuishi na wengine wanatamani hata angekuwa tayari ameshauwawa kwasababu ya kitendo ambacho amemfan yia yule mtoto,huu ni unafiki.

Nasema ni unafiki kwasababu kwenye tukio hili na matukio mengine binadamu tumejipachika utakatifu na kujiondoa kwenye madhambi pengine makubwa zaidi kuliko hata alilofanya huyu dada,lakini kikubwa zaidi dada yule ameonekana kama yeye tu ndio mwenye tatizo.

Kimsingi binadamu ambae amekamilika kiakili hawezi kufanya jambo kama lile na kama atafanya ni lazima kutakuwa na sababu nyuma ya alichokifanya.leo hii ni vigumu kukutana na mtu ambae hajui kabisa madhila ambayo wanakutana nayo hawa wadada wa kazi huko kwenye majumba wanamoishi,kuna dada mmoja ambae niliwahi kukutana nae na kuniambia maswahibu ambayo anakutana nayo huko anakofanya kazi hadi nililengwa na machozi.

Dada huyu anasema hajawahi kununuliwa nguo bali zile nguo ambazo zinachakaa za watoto wa mwajiri wake ndio anapewa kuvaa,zile ambazo zinawabana watoto hao na zinakuwa bado ni nzuri hapewi na hutafutwa namna nyingine ya kufanywa na hata wakati mwingine kupelekwa kwa watoto wa ndugu zao,binti huyu anasema kuwa hajawahi kukaa mezani kula pamoja na mwajiri wake na kila siku yeye huwa wa mwisho kula na wakati mwingine hulazimika kula makombo kwani kuna wakati chakula huisha na kwakuwa haruhusiwi kula pamoja na wanafamilia na c hakula kinapokuwa ni kidogo hulazimika kula makombo ya mabosi wake.

Dada huyu anasema kuwa pamoja na wakati mwingine kutokula chakula ambacho anakinunua mwenyewe na kukipika anasema siku akichelewesha chakula basi huambulia kufokewa na wakati mwingine ananyimwa chakula na kuna wakati hata hulala nje ya nyumba kwani mama mwenye nyumba humfungia nyumba kwa sababu ya kosa fulani tu.Dada huyu akaniambia kuwa kuna siku aliunguzwa mkono wake kwasababu tu alipoteza sh 500 ambayo alirudishiwa sokoni baada ya kyhemea vitu vya nyumbani.

Hayo ni kwa ufupi tu,yapo makubwa zaidi ya hayo na wengine hufikia kudhalilishwa kabisa na waajiri wao,kwasababu hawa watu wanaishi kwenye majumba na hakuna ambae wanaweza kumuambia angalau kupu nguza hasira ambazo wanakuwa nazo wameishia kutukutia ndani kwa ndani na kilichotokea Uganda ni mfano wa hili.Hakuna mtu ambae nimemsikia akijaribu kutazama upande wa pili wa shilingi ili kuona hasa tatizo limeanzia wapi.

Siungi mkono kile ambacho dada yule amekifanya na kinahitaji adhabu,lakini kumuona dada yule kama shetani wakati kuna shetani mwingine anadunda tu na ndie huenda amesababisha yote hayo sio jambo na kibinadamu.Kama nilivyosema hapo juu, ni vigumu sana kwa binadamu ambae yuko timamu kabisa kufanya kitendo kama kile lakini kama akifanya ni lazima kunakuwa na sababu nyuma ya hilo,kwanini hatuangalii kile ambacho kinaweza kluwa kimemsababisha huyu binti kufanya alichokifanya?

Binti yule sio kichaa,nasema hivyo kwasababu kama angekuwa na tatizo hilo sidhani kama hao waajiri wake wangekuwa wameishi nae kwamuda wote ambao wameishi nae,kwasababu hiyo sasa huyu binti ni mzima kabisa kiakili,sasa je ni kwasababu gani amefanya vile? Hili ni swali ambalo mtu yoyote yule mwenye utimamu wa akili na ubinadamu anatakiwa ajiulize lakini kwasababu sisi ni wanafiki hatujiulizi kwasababu tunayaogopa majibu ambayo yatakuja na kutuumbua.

Hivi ni nani anajua kama huyu binti amekuwa akipata mateso maku bwa sana hapo kwenye hiyo nyumba? Sisemi kuwa kama alipata mateso bali ni halali kwake kufanya hivyo lakini kujua hili angalau tunaweza kuona kuwa mwenye kuonwa ni shetani sio huyu binti pekee bali kuna mwingine au wengine.

Mateso ambayo wamekuwa wakikumbana nayo hawa wadada wa kazi ni ya kutisha na kama tunavyojua kuwa binadamu anapoteswa hutafuta namna ya kulipiza kisasi na pale ambapo anakuja kuona kuwa mhusika anaemtesa hawezi kumlipizia kisasi kwasababu huenda akawa ni tajiri basi mhusika hutafuta wanyonge wake ambao mara nyingi kwa hawa wadada wa kazi huwa ni wale wanaowalea na haya yaliyotokea ni matokeo ya haya.

Huyu dada hajapewa kabisa nafasi ya kujitetea na sidhani kama atapata,hili nalisema kwakuwa nasikia kwanza amepewa kipigo kikali sana na mwajiri wake na polisi walipokuja kumkamata huyu mwajiri aliwaonesha video na walimuachia,tatizo ambalo hata hawa mapolisi wa Uganda nao walishiondwa kufikiri kwa namna ya kibinadamu [kama kweli walimkamata na kumuachia] na wao waliona huyu mwajiri ana haki ya kumuadhibu huyu dada kwa kitendo kile,kitu ambacho sio sahihi kabisa.

Ifikie mahali tuwe na utu hata angalau kidogo,watu kama huyu dada hawana mtu wa kuwaambia madhila wanayokutana nayo na hiyo imewasababisha kufanya mambo ya ajabu kama haya,kwa wenzetu kuna vitengo vya kufatilia matukio kama haya na inafikia mahali uchunguzi hufanyika na hatimae kila mtu kubeba adhabu stahiki,kama mwajiri wake anahusika na kumnyanyasa huyo dada na kuna wakati hufikia hawa wadada kubakwa na waajiri wao,ni nani atawawajibisha hawa waajiri wa huyo dada wakati hawampi nafasi hata ya kujitetea?

Kama huyu dada ni shetani,hawa waajiri ambao wanawanyanyasa hawa wasaidizi wao wa ndani hadi wanawaathiri kisaikolojia watakuwa nani? Nani anawapa kipaza sauti hawa wadada na kuwapa nafasi ya kusema kile ambacho wanakutana na cho huko majumbani mwetu?

Binadamu tuna safari ndefu sana hadi kufikia kujitambua na kuacha unafiki huu,najua huyo dada yupo kwenye wakati mguu sana sasa,lakini naamini Mungu atam saidia,kitendo alichomfanyia yule mtoto hakikubaliki na sheria ichukue mkondo wake lakini kama hawa waajiri wake ambao naamini watakuwa wamehusika na madhila yaliyompata mtoto wao nao wana chao cha kujibu mbele ya sheria,haiwezekani tukio hili liachwe hivi hivi tu na mnyonge aadhibiwe peke yake

Haikubaliki
 
Okey, umejitahidi kuelezea kwa pande zote lakini hata hivyo bado haitoshi kumuona yule dada ni mtu wa kawaida.
Hata kama alifanya vile kutokana na madhira anayopata toka kwa wazazi wa yule mtoto, bado ni shetani pekee anayeweza kulipiza kisasi cha aina ile.
Kuna mtu alisema pamoja na adhabu za kisheria atakazopata yule binti, wanaume wote mpaka huko magerezani tungeonesha umoja wetu na hasira za jambo hilo kwa kususia kufanya nae tendo la ndoa ili asizae milele kwani hata mtoto wake yawezekana akamfanya hivohivo.
 
Ndo maana mimi sitaki, sijawahi, na sitakuja kuwa na msaidizi wa ndani.

Kwa upande wangu huwa naona ni kama 'slave labor' kuwa na huyo msaidizi.

Hao wadada huwa wananyanyaswa sana.

Kwanza tu hata ile kuwapa majina kama 'beki tatu' au 'house-girl' naona ni dharau.

Na sioni ambacho huyo msaidizi anafanya ambacho mimi siwezi kukifanya.

Mpaka sasa nimefanya vizuri tu na nimekuza mdada mzuri, mwenye kujielewa, mwenye heshima, na mwenye bidii shuleni.

Unamkuta msichana wa watu anaambiwa kauli chafu chafu na zenye dharau na hao mabosi wake hususan akina mama.

Mtu hata kumwongelesha kwa kauli nzuri na ya kistaarabu huwezi, sasa unategemea nini?

Nawahurumia sana hao wadada.

Ningekuwa na uwezo ningehakikisha walau kunakuwa na utaratibu mzuri wa kuajiri hao wasaidizi - yaani kunakuwepo na sheria zinazolinda haki zao na wapi pa kwenda iwapo inatokea wamedhulumiwa au kutendewa vibaya.
 
"mabosi" wengi huwa ni wakatili kuliko tunavyodhani. Hawa hawa wanaolaani kitendo cha huyu dada kumfanyia unyama malaika huyu, wengi ni wakatili tena kupitiliza kwa wasaidizi wao majumbani huku wakiwalipa as low as 20,000tsh kwa mwezi, huku wakifanyishwa kazi kuliko punda. Hayo nimewahi kuyashihudia.

Alichokifanya hakina justification yoyote coz angeamua kuondoka kama mateso yamezidi, lakini nae aliona hana pa kumaliza hasira zake isipokuwa kwa malaika.

Huwa nafikiria jinsi mwanangu atakavyoishi, maisha ya kitanzania bila wasaidizi WA nyumbani sijui kama yanawezekana. Japo nazidi kufikiria na najua upinzani mkubwa utakuja toka kwa mke lakini lazima ipatikane mbinu aisee..
 
chochote kile haki-justify kitendo alichofanya yule dada.....kama aliona mateso yamezidi angeondoka,wapo madada wengi tu wanateswa mwisho wanatoroka au wanaomba kuondoka.....kitendo alichofanya ni cha kinyama na anastahili adhabu kali.
 
Kulaani kitendo alichofanyiwa innocent victim ni reaction ya kibinadamu.

kujiuliza how na why inakuja baadaye sana. Na kama wewe ambavyo umeamua kubase upande wa msichana wa kazi mimi na wengine wengi tumeamua kujikita kwanza kwa innocent victim.

Tunazo facts mezani ambazo ni mtoto kateswa kwa vipigo ambavyo ni vya kuua. Na pia reaction ya mzazi baada ya kukutana na hiyo fact, kweli mzazi aligeuka mnyama pia lkn nani asingegeuka mnyama kwa hali ilivyokuwa?

speculation ni kuwa binti ameteswa sana na kuamua kumalizia hasira zake kwa mnyonge (innocent victim ). Je ni njia sahihi kufanya aliyoyafanya?

wanaokutwa na hali kama hiyo hufanya nini? Kwanini asiondoke au asiende police?

Suala la kumalizia hasira waliodhaifu kuliko wewev sio jema kabisa. Nakumbuka mama alishanipiga sana kisa ameudhiwa na mama mkwe wake na wifi zake, of recent nilimkumbushaa au umeudhiwa kazini unakuja mpiga mkeo sio fair.
Anger management inahitajika kwa watu wengi. Yes binadamu anaweza kuwa shetani inahitaji trigger ndogo tu. So yule binti jwa wakati ule alikuwa shetani, na baba mtoto alikuwa shetani pia.
 
Ndo maana mimi sitaki, sijawahi, na sitakuja kuwa na msaidizi wa ndani.

Kwa upande wangu huwa naona ni kama 'slave labor' kuwa na huyo msaidizi.

Hao wadada huwa wananyanyaswa sana.

Kwanza tu hata ile kuwapa majina kama 'beki tatu' au 'house-girl' naona ni dharau.

Na sioni ambacho huyo msaidizi anafanya ambacho mimi siwezi kukifanya.

Mpaka sasa nimefanya vizuri tu na nimekuza mdada mzuri, mwenye kujielewa, mwenye heshima, na mwenye bidii shuleni.

Unamkuta msichana wa watu anaambiwa kauli chafu chafu na zenye dharau na hao mabosi wake hususan akina mama.

Mtu hata kumwongelesha kwa kauli nzuri na ya kistaarabu huwezi, sasa unategemea nini?

Nawahurumia sana hao wadada.

Ningekuwa na uwezo ningehakikisha walau kunakuwa na utaratibu mzuri wa kuajiri hao wasaidizi - yaani kunakuwepo na sheria zinazolinda haki zao na wapi pa kwenda iwapo inatokea wamedhulumiwa au kutendewa vibaya.
How do you manage without a house helper? Mie naona ngumu sana kwa maisha ya kitanzania, labda huko ughaibuni
 
hivi yule alieunguzwa na PASI hapa BONGO ishu yake iliishaje
Hakuna wa kuwasemea hawa wadada masikini,ila pale wanaposhindwa kuvumilia na kuonesha wanavyoteseka wanaonekana sio binadamu .....

Binadamu sijui lini tutaacha unafiki .....!!
 
umemtazama dada kwa jicho ulilomtazama yule aliyekupa kisa chake. Pole anatakiwa kupewa mtoto na si kuhalalisha ukatili kwa mtoto, ila si vibaya kutoa angalizo kwa namna tunavyowafanya wafanyakazi wa ndani. Dada wa kazi anaweza kuwa na ugonjwa wa akili ukalipuka siku isiyojulikana. Wapo wadada wa kazi wanaoteswa lakini hawawakatili watoto. Wapo ambao hawateswi na waajiri ila wana visirani vinavyotokana na sababu nyingi zikiwamo za kimapenzi - kaachwa na bwana basi hasira kwa mtoto. Wengine wanafanya hizi kazi kwa sababu hawana namna, wamefungashwa na wazazi kuja mjini. Hata uwape nini bado wananuna tu na kazi wanafanya wanavyotaka. Unabembeleza housegirl mpaka unajishtukia. Nimeshakutana nao. Kwa hiyo sababu za ukatili wa wadada wa kazi nyingi.

Nimewahi kuwa na housegirl mkatili kwa mtoto. Hakuwahi kuonyesha kuwa na roho mbaya. kwa miezi mitatu aliyokaa nilijitahidi kumpa mahitaji yote muhimu. Anakula ninachokula mimi jioni, mchana anakula anachotaka yeye maana sipo. Analala kwenye chumba chake mwenyewe na malazi ni masafi. Jumapili anaenda anakojua yeye kwa mapunziko. Jumapili moja akanirudia saa 5 usiku. Nikauliza kulikoni nikadanganywa nilivyodanganywa maisha yakaendelea.

Mtoto wangu wakati huo akiwa na mwaka na miezi 3 alikuwa mbishi wa kula na kulala. Yule dada akawa ananiambia wewe anakusumbua sana. Mimi wala hanisumbui. Nikachukulia watoto wote hudeka wakiwa na mama zao. Kuna kipindi nikawa nikirudi home mtoto anaenda jikoni ananiletea kiboko usawa wa rula hivi. Wakati huo hawezi kuongea vizuri. Ananionyesha kile kiboko lakini nilivyokuwa mpuuzi hata sikufikiria kama kilikuwa kinamhusu. Siku moja nikiwa namnyonyesha akawa anapeleka sana mkono makalioni. Wakati nambadilisha diaper nakuta kuna mstari umevimba. Nikashangaa, nikamwita dada kumuonyesha akaniambia labda mdudu. Nikajiuliza huyu mdudu gani anapita kama rula. Kwa umri wa mtoto na upole wa dada sikuwaza habari ya kuchapwa. Siku ya siku jirani akaniita na kunipa habari kuwa mtoto wangu anachapwa sana na msichana wa kazi. Sikuwa na sababu ya kubisha maana dalili nilishaziona nikapuuza. Nikarudi nyumbani nikamtimua yule binti.

Kutokana na huo uzoefu wangu siwezi kusema moja kwa moja kuwa mayaya wanakatili watoto kwa sababu nao wakakatiliwa na waajiri. Mwajiri anaweza kumlamba miguu yaya na bado yaya akafanya vituko. Ukatili hutokana na "frustration" inayotokana na mtu kutofikia malengo yake fulani. Tuliangalie hili swala kwa upana zaidi. Ila kama mnataka tuangalie sababu moja ya waajiri, sawa.
 
Okey, umejitahidi kuelezea kwa pande zote lakini hata hivyo bado haitoshi kumuona yule dada ni mtu wa kawaida.
Hata kama alifanya vile kutokana na madhira anayopata toka kwa wazazi wa yule mtoto, bado ni shetani pekee anayeweza kulipiza kisasi cha aina ile.
Kuna mtu alisema pamoja na adhabu za kisheria atakazopata yule binti, wanaume wote mpaka huko magerezani tungeonesha umoja wetu na hasira za jambo hilo kwa kususia kufanya nae tendo la ndoa ili asizae milele kwani hata mtoto wake yawezekana akamfanya hivohivo.

Yaani wewe unaona ni sawa binadamu mmoja kufanyiwa unyama [hakika ni unyama] lakini unaona sio sawa binadamu mwingine kufanyiwa unyama ule ule .....

Akili yako ni lazima itakuwa ina matatizo mahali ....!!
 
Hakuna wa kuwasemea hawa wadada masikini,ila pale wanaposhindwa kuvumilia na kuonesha wanavyoteseka wanaonekana sio binadamu .....

Binadamu sijui lini tutaacha unafiki .....!!

siku zote shida kubwa huja kwa njia tunayotumia kutatua tatizo, maana hiyo huwa tatizo kubwa kuliko la awali
 
How do you manage without a house helper? Mie naona ngumu sana kwa maisha ya kitanzania, labda huko ughaibuni

I have a can-do attitude. I can cook, clean, run errands and then some.

Bongo kwa mtazamo wangu watu wengi wala hawahitaji maid.

Babysitters sawa, sikatai. Lakini hadi kupikiwa na kufuliwa nguo?

Unakuta familia nzima ipo nyumbani lakini wanapikiwa na msaidizi.

I shake my head in mystification.

*Na unasema ni ngumu sana kwa maisha ya Kitanzania? Mbona mimi sikulelewa na msaidizi wa kazi za ndani na leo hii nipo nina mji wangu na najitegemea mwenyewe? Wazazi wangu waliwezaji ilhali wote walikuwa ni wafanyakazi?*

I tell you a 'can-do attitude' goes a long way.
 
Ndo maana mimi sitaki, sijawahi, na sitakuja kuwa na msaidizi wa ndani.

Kwa upande wangu huwa naona ni kama 'slave labor' kuwa na huyo msaidizi.

Hao wadada huwa wananyanyaswa sana.

Kwanza tu hata ile kuwapa majina kama 'beki tatu' au 'house-girl' naona ni dharau.

Na sioni ambacho huyo msaidizi anafanya ambacho mimi siwezi kukifanya.

Mpaka sasa nimefanya vizuri tu na nimekuza mdada mzuri, mwenye kujielewa, mwenye heshima, na mwenye bidii shuleni.

Unamkuta msichana wa watu anaambiwa kauli chafu chafu na zenye dharau na hao mabosi wake hususan akina mama.

Mtu hata kumwongelesha kwa kauli nzuri na ya kistaarabu huwezi, sasa unategemea nini?

Nawahurumia sana hao wadada.

Ningekuwa na uwezo ningehakikisha walau kunakuwa na utaratibu mzuri wa kuajiri hao wasaidizi - yaani kunakuwepo na sheria zinazolinda haki zao na wapi pa kwenda iwapo inatokea wamedhulumiwa au kutendewa vibaya.

Mkuu hii kitu inaniuma sana

Binadamu tumefikia kiwango cha hatari sana cha kuona kama sisi ni binadamu lakini wengine asio binadamu .....

Aaaaaaahhhhh ......!!
 
Umenena Eiyer! Nilipo ona hile video kwa Mara ya kwanza nilisikitika sana na ni video ambayo siwezi kurudi kuangalia maana inasukitisha sana mtoto kufanyiwa vile!

Lakini baadae nilianza kujenga picha juu ya hili tukio!
Kwanza ningekuwa Mimi cha kwanza ninge hitaji apimwe akili yule binti Maana nilijenga picha ya mtu mwenye tatizo la akili!

Pili nilijenga picha ya binti wa kazi anaye teswa sana na wenye nyumba hivyo analipiza kisasi kwa mtoto wa wanao mtesa na kumnyanyasa!

Pia nilijenga picha yakuwa huyu binti huteswa sana na Mama mwenye nyumba kiasi kwamba amepata tatizo la kisaikolojia na la kiakili maana tumezoea ni kawaida Wamama walio wengi kuwanyanyasa wafanyakazi!

Kwakweli nilikosa jibu nilipo pata taarifa kuwa huyu mtoto alikuwa anaishi na baba yake pamoja na housegirl tuu!

Bado niliendelea kujiuliza ni lini Mama mwenye nyumba aliachana na Mumewe kama walishawai kuishi pamoja?

Mama mwenye nyumba hakuwai kuishi na huyu binti wa kazi kabla ya kuondoka?

Nini hufanyiwa huyu mfanyakazi na Baba mwenye nyumba na wana maahusiano gani na mfanyakazi?

Nilijiuliza hayo Maswali kwakuwa asilimia 99% ya mateso ya wadada wa kazi huyapata kwa wa Mama wenye nyumba!
Na kuhakikishia kabisa kati ya wanawake 100 ni wanawake 3 wanaweza ishi na wafanyakazi wa ndani kama watu muhimu kwao!

Katika hili ni wazi kabisa kuna sababu za msingi kabisa yule mfanyakazi kufanya yale kama itathibitika hana tatizo la kisaikolojia au la kiakili! Wafanyakazi wandani wananyanyaswa sana tena uzuri Mimi nimeshuhudia sana hili lakini ukisema unaonekana una interest!

Yani unakuta hawapewi muda wa kupumzika na mshahara bado mdogo na wengine wana kopwa kabisa hadi mshahara!

Wafanyakazi hawa wanateswa sana na wanao watesa ndio hao hao huwa wakwanza kusema wana uchungu sana na huruma sana kumbe ni unafiki tuu!

Kwakweli kitendo alicho mfanyia mtoto hakikubaliki lakini kwa upande mwingine hawa watu nao hupata mateso sana kwa sisi wenyewe tunao laani kitendo chake!
 
Last edited by a moderator:
"mabosi" wengi huwa ni wakatili kuliko tunavyodhani. Hawa hawa wanaolaani kitendo cha huyu dada kumfanyia unyama malaika huyu, wengi ni wakatili tena kupitiliza kwa wasaidizi wao majumbani huku wakiwalipa as low as 20,000tsh kwa mwezi, huku wakifanyishwa kazi kuliko punda. Hayo nimewahi kuyashihudia.

Alichokifanya hakina justification yoyote coz angeamua kuondoka kama mateso yamezidi, lakini nae aliona hana pa kumaliza hasira zake isipokuwa kwa malaika.

Huwa nafikiria jinsi mwanangu atakavyoishi, maisha ya kitanzania bila wasaidizi WA nyumbani sijui kama yanawezekana. Japo nazidi kufikiria na najua upinzani mkubwa utakuja toka kwa mke lakini lazima ipatikane mbinu aisee..

Mkuu we acha tu .....

Kuna mdada mmoja aliamua kumuambukiza Ukimwi kwasababu za kuteswa na waajiri wake namna hii hii,yule dada alilaumiwa sana na alionekana kama hana utu lakini wale waliokuwa wanamtesa wakaonekana ni watu ...

Pambaf .......!
 
Back
Top Bottom