The Finest
JF-Expert Member
- Jul 14, 2010
- 21,605
- 6,080
Mwanakijiji mpe pole Nyonda mwambie atulize moyo na agange yajayo.
Pendo ninakupa pole
Kwa yote yalokusibu
Nakupa haya na yale
Ni miye wako habibu
Pole nyonda pole, kutoka kwa pendo pole!
Yamenitoka machozi
Mawazo yajaa tele
Nimeshindwa fanya kazi,
Nikiyawaza ya yule
Pole nyonda pole, kutoka kwa pendo pole!
Jalali tumuachie
Tugange yaliyo mbele
Moyo wako utulie
Upate ya kheri tele
Pole nyonda pole, kutoka kwa pendo pole!
Moyoni mwangu tulia
Ewe nyonda wa milele
Tulia binti tulia
Nakusubiria kule
Pole nyonda Pole, kutoka kwa pendo pole
Na. M. M. Mwanakijiiji (Sauti ya Kijiji) BGM.
* Rafiki yangu mmoja mpenzi amenisimulia simulizi la huzuni na kunifanya niandike hiki kama sehemu ya faraja yangu kwake. Dedicated kwake huyo.
Wanaume wakati mwingine tunaweza kujipatia vipointi hivihivi
Bembeleza
Sema pole
Jibaraguze
And say sorry!
Mambo yanajiweka sawa tu..
CAmerederie.. nimepigiwa simu na nyonda fasta fasta.. "ooh unaibiwa!" nikasema nini? "Ati kuna waasi wanajaribu kuja Tripoli"!! Nikaambiwa naweza kujikuta nabakia kuimba "zenga zenga"!
Kwi kwi kwiiii....:lol::lol:...niko na KIDAWA wa KIPAWA wangu
Mwanakijiji,
Nyonda anaendeleaje?....mwambie KIDAWA wa KIPAWA anampa pole pia