Pole mwenyekiti wetu Mbowe, sikufundishi kazi ila ujue kazi hii ni yetu wote

TAMKO

JF-Expert Member
Oct 11, 2011
1,090
762
Salaam Mwenyekiti wangu.. Leo Tarehe 5April Najaribu Kuvaa kiatu chako Kwa mtazamo wa Kila kitu Najua Uko kwenye wakati Mgumu Unajipa Mtima wa kusonga Mbele Labda maisha Yatapata Direction.

Nimepitia mitandaoni, majukwaa mengi ya Kijamii NIMESOMA Comments kwenye posts mbalimbali hasa zinazo husiana na Chama chetu, Kwa Upande wa Hasi na Chanya vyote, Na wakati NASOMA Natengeneza Picha na wewe ukisoma Najua HAKUNA ZINAZO KUFURAHISHA. Si Za wana CDM au CCM au Wapinzani WOTE WANACHEFUA TU. Hakuna mwenye True Solution ya Nini sasa Kifanyike Kwenye Sintofahamu hii.

Wewe ni MWENYEKITI wa Chama Kikuu hapa TZ. Lazima Uwe imara kuhakikisha Unakinasua kisogee Tena Mbele. Mimi Nina Ushauri kama Utaupokea Sawa kama Hauta upokea pia sawa. Ushauri ni Ushauri tu. Kabla ya Kushauri kidogo niweke Kumbukumbu..

Unakumbuka 2005, Tuanzie hapo, ulipata kura laki Sita, Sio mbaya. ilikuwa Duru la pili. Upepo wa kisiasa ulipwaya kutokana na historia ya mrema 1995 unakumbuka sina haja ya Kurudia huko. Nataka nifinyilie hapa karibuni.

Upepo mzito Kwa Chama Chetu Ulivuma ulipo muibua Dr Slaa 2010. Kishindo Cha Dr Slaa kilitokana na Kweli kadhaa na Ujasiri wake Bungeni wa Kuibua Kashfa mbalimbali. Ghafla watanzania Wakaibuka Kwa Nguvu kumshabikia sana. Kura zikakwea hadi milioni mbili Za Urais. Chama Kimetembea Kwa Nguvu Za Hoja, Bungeni na Nje ya Bunge. Hoja ambazo Wananchi walizielewa na zilikuwa Za kweli. Matarajio Hayo yakaja 2015. Lakini Mgombea wetu akawa na kasoro Kubwa kwenye masuala ya Ndoa Yake. Hali iliyofanya chama kuminyika sana. Matarajio ya Wananchi wote Yakahamia CCM Hasa Mechi ya UCHAGUZI ndani ya Chama hivyo. Ng’atana ng’atana ile WANANCHI wote matarajio yao na Macho yao yalikuwa Edward Lowassa. Chadema Tukafifia sana. Mawimbi ya Redio ya CCM Ndio yalisikika Kila KONA EDO! Lakini Tumaini la Watu wote EDO, Jamaa wakampiga Chini.. Mungu akasaidia Edo Akaja CDM.

Unakumbuka Edo alirudisha Form Kwa mbwembwe ambazo hazijawahi tokea. Mtaji Wa EDO ulitupatia Kura karibia milioni tano..achilia Mbali Wabunge 116 na madiwani. Mbali na mashambulizi mawili la Dr Slaa na Lipumba Ndani ya Ukawa Lakini Mtaji wa Mzee Yule Uliiweka CDM juu mno.

2020 Sasa Iko mbele Yetu.. imekaribia sana. NAJUA HATUNA KETE MKONONI. Tulisusia Uchaguzi wa Serikali ya mitaa Tukapigwa Jumla, Leo Dalili zinaonyesha rangirangi tena. HAPO LAZIMA TUJITATHIMINI.

Kabla ya Kujitathimini Tuna PEPO Tatu, Tuzijue

1: CHAMA HAKINA MSEMAJI:- Kwa sasa Mwana Chadema Yeyote ni msemaji kwenye Jambo Lolote. Kiongozi wa Chama anakurupuka tu kupost Majibu anayo waza Yeye mtandaoni Bila kufikiri kwamba wasomaji Wataelewa Ndio msimamo wa Chama. Viongozi wa Chama hawajui kwamba Hata post ya mtandaoni inayo Husu Chama ni Usemaji. Hii imeleta mkanganyiko mkubwa sana. Najua Inakuchanganya sana. Labda ni Utoto au Ulimbukeni wa kutumia Mitandao.

2: Tokea Mashambulizi ya Ndugu Yetu Lissu (MB) , kuna Upepo ulivuma kiasi Chama Kikapata wafadhiri MAJERAHA YA CCM. Wale Wafadhili ambao ni MAJERAHA ya CCM Ndio Chama Kimewabeba Jumla na wamekuwa Watetezi wa Chama Mitandaoni. Taratibu Chama kimewafanya miungu watu na hakina Ubavu wa Kuwakemea Hata wakikosea. Chama kimejivika Mavi na Hakiwezi kujivua mavi Hayo. Sikutaka kutaja Majina Lakini hapa naongelea watu kama Maria/Mange/shangazi n.k Nadhani Unaelewa. Hawa sio wabaya, ni wanachama Lakini MAJERAHA! Kila mmoja Ana JERAHA Ambalo hawezi kuwaza positive, Najua hamta penda lakini tunaongea kama kweli Tuna dhamira ya Kujenga Chama UPYA.

3: MA-PROPAGANDIST.. katikati ya Hawa MAJERAHA, kuna Kikundi kibaya Sana Kimeibuka, hiki Ndivyo kimeua kabisa Siasa Za Elite society Mitandaoni. Propagandist Hawa ambao Chama Kimekuwa kikiwafuatilia tena Kwa Karibu kama watetezi lakini wameshakipaka matope, Chama Kimeingizwa kwenye Shimo la mavi Bila Kujua. Propagandist Hawa kama KIGOGO, Wamejaribu kutunga Taarifa Za Uzushi kuaminisha Jamii kwamba wao ni antenas.. receiving informations Kila kona. Sometime wanarushiwa taarifa Flan na kuzifanyia kazi. Akili za Chama zote zimeshikwa na Kigogo na Hawa ni zaidi ya miungu watu hawaguswi!

Mzee Mwenyekiti CHAMA HAPO HAKIPO.. Tujitathimini..!

1: Kwanza Tujue Mitandao ipo, Hatuwezi kuwazuia watu Kupost watakayo na watakavyo. Lakini kama mwenyekiti kamata Usukani wa Gari lirudishe Barabarani Hao watu sio Muhimu kama Jamii Kubwa ya Watanzania wanao Taka Mageuzi. Raha ya Nchi ni Vyama Vingi yenye Nguvu. Sio dhaifu au Mfu.

2: Rudisha Chama Back to 2015 ambapo Tulikuwa Tukiongelea Matatizo ya Wananchi na Utatuzi wake Kuliko siku hizi ambazo Chama kimejikita kwenye personal attacks. Tukiendekeza hao MAJERAHA YA CCM Chama kitakuwa kama inzi kikishambulia watu Kila siku na mwisho Tutapotea. Wananchi hawako na Interest na Hayo.

3: Acha Maamuzi ya KIIMLA. Chama Cha Demokrasia Basi Hubiri Demokrasia. Ukiendekeza maamuzi ya Hulka, Mihemko na Imla Chama Kitakufia. See Hiki ni Chama Cha Demokrasia -hubiri Demokrasia Kwa Vitendo. Unakumbuka Baada ya Uchaguzi “UKUTA” ikafeli.. acha Ukuta Ukaamuru Maamuzi Mabaya Kabisa Yasiyo ya Kidemokrasia kukikataza Chama Kisishiriki Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa, ULIKOSEA MZEE, Watu walijiandaa wakaacha! Labda Ulikuwa na Plab “B” Kumbe Huna lolote ilikuwa munkari tu sasa Watu Hawana viongozi wa Msingi kabisa. Ungekuwa wa Kidemokrasia Ungesema Nduguzangu kutokana na Mapungufu haya ya Uchaguzi, na Tumefanya bidii hizi kurekebisha imeshindikana uongozi umeamua Kutoshiriki ila Kwa Sababu ya Demokrasia Mtu atakaye penda kushiriki Hazuiliwi hapo unge-exercise Democracy, Lakini pia UNGETOA PLAN “B” sio Kusema Hushiriki na Huna Plan B.

Makosa Hayo naona yanaendelea kwa kasi, Juzi UMETAMKA Wabunge watoke Bungeni kwamba pamejaa Corona. Ni Sawa Sipingi Lakini Unge-exercise Democracy Ukawaambia madhara ya Kuendelea na Bunge na Uamuzi we Chama kuwalinda wabunge wake kisha ukawapa Demokrasia na wao kuchagua atakaye endelea na asiye taka Kuendelea Ndio maana ya Demokrasia. Lakini PIA MAAMUZI Hayo Yanaonekana kukosa Hadhi ya Uongozi, Kama madaktari/manesi wako mstari wa mbele kupambana na pandemic wewe unajifungia ndani? Hii mzee Imeonyesha Udhaifu Mkubwa sana. Kiongozi anaye jijali mwenyewe na Mbinafsi. Contradiction Kubwa zaidi ni Pale Viongozi ambao Wamejiwekea karantini wanaonekana ofisini wakifanya Kazi Za Chama unajua ni KUJIVURUGA SANA.

4: THAMINI Walio Tufikisha Hapo. Mtu yeyote aliye Ipaisha au kuishika mkono CDM lazima aheshimiwe na sio KUFUATWA. Ni Vema Kuwa na Utu, 2015 Wana CCM wengi walikuja CDM. Lakini wengi wamerudi CCM, Tumewatukana, Tumewachamba, Tumewachora HUU SIO UTU. Mzee EDO Aliondoka Ukiwa Gerezani kweli Lakini hotuba yako ulipo toka Gerezani kuhusu Yeye Sikupenda Hata kidogo. Kiongozi asiye thamini Watu walio mshika mkono Wakati wa taabu Yake HAFAI. Ungempa Heshima Yake Ukamwacha. Viongozi wako wamemsema mitandanoni Ndio maana Nasema Chadema Kila mtu Msemaji. Mzee Gwajima Mzee Kakobe Hawa Walitutoa wapi, Kweli ni watu wa kuwashambulia leo!. Shukrani Gani. Hata kama hawapo Kwetu Tuna Yetu ya Kuyafanya ya Msingi.

5: Maisha Ya Chama Cha siasa ni ku-win citizens mind. CDM Kazi hiyo haifanyiki kabisa. mnadeal na Personal Atack! Kitu ambacho hakijawahi kusaidia! Baadae Wananchi watatuuliza mlitusaidia nini Wakati wa Corona majibu ni “tulikuwa tukimshambulia raisi” HAYA NDIO MAJIBU Ya kuwapa Wananchi Wakati wa Kampeni Kweli? .

Mwananchi mmoja wa Kijijini nilimsikia akisema “Chadema imekufa kweli yaani Gonjwa limeanzia China wao wanalifanya mtaji wa kisiasa” maneno yao yana Ukweli au Hayana Ukweli ila Result inayo patikana ni kwamba Tumefeli ku-win mindset zao.

Mwenyekiti Mbowe Sikufundishi Kazi Ila Ujue Kazi hii ni Yetu Wote. Kama Chama Kitakufa, 2020 wakawepo wabunge wa CCM Bungeni, sio kwamba Hali Itakuwa shwari Upinzani wa CCM Kwa CCM ni Mkali zaidi. Hivyo kama Chama kisipo jirekebisha Mapema Wenye akili wengi Watakimbilia CCM. Ndani wana mageuzi ila Nje CCM. Wakipata Nafasi BUNGE LA 2020 litakuwa CCM tu na Litakuwa HOT ZAIDI, maana Hakuna wakumwambia Ndio mzee Wala sio mzee Bali wote watoto wa nyumba moja ni Mnyukano zaidi.

ASANTENI.
 
Unavyomwambia Mbowe aachane na propagandist kina Kigogo 2014 ni lini uliwaona wakisaini mkataba wa ushirikiano?!

Unataka chama kiachane na watetezi kina Maria Sarungi na wenzake, again ni lini uliwaona wakisaini mkataba wa ushirikiano? au unaposema chama kuwabeba una maana gani?!.
Unadai kutaka demokrasia lakini hutaki wengine waseme.. why!

Hujui kuna wakati watu hufanana maoni/mawazo hasa wakati huu tulionao wa "sampuli za papai" kupelekwa maabara kupimwa Corona?

Hapo kwenye "personal attack" tuambie CDM wanamuattack nani ili tujue huyo mtu anastahili hizo attacks au anaonewa?

Mbowe kuamua Wabunge wa CDM kujiweka karantini siku 14 ni kulingana na maelekezo ya wataalamu wa Afya, sio yake binafsi; unapoona Wabunge "wanaondoka" kwa ile spidi ulitaka waendelee kukaa bungeni tu kama viazi? na hiyo demokrasia inayokupa uhuru wa kuchagua kifo ni ya kipuuzi. Wabunge wa CDM waliorudi bungeni kabla ya siku 14 ni njaa zao tu,sio demokrasia.

Huo mtazamo wa "mwananchi kijijini" ndio umeutumia ku- conclude kwamba CDM imeshindwa ku-win people's mind, sijui kama umewahi kufanya research toka uzaliwe.

All in all, umejitahidi kutoa mawazo yako, but umeacha gap nyingi sana kwenye hoja zako.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unavyomwambia Mbowe aachane na propagandist kina Kigogo 2014 ni lini uliwaona wakisaini mkataba wa ushirikiano?!

Unataka chama kiachane na watetezi kina Maria Sarungi na wenzake ni lini uliwaona wakisaini mkataba wa ushirikiano? au unaposema chama kuwabeba una maana gani?!. Unadai kutaka demokrasia lakini hutaki wengine waseme.. why!

Hujui kuna wakati watu hufanana maoni/mawazo hasa wakati huu tulionao wa sampuli za papai kupelekwa maabara kupimwa Corona?

Hapo kwenye "personal attack" tuambie CDM wanamuattack nani ili tujue huyo mtu anastahili hizo attacks awe anaonewa?

Mbowe kuamua Wabunge wa CDM kujiweka karantini siku 14 ni kulingana na maelekezo ya wataalamu wa Afya, sio yake binafsi; unapoona Wabunge "wanaondoka" kwa ike spidi ulitaka na waendelee kukaa bungeni tu kama viazi? na hiyo demokrasia inayokupa uhuru wa kuchagua kifo ni ya kipuuzi. Wabunge wa CDM waliorudi bungeni kbl ya siku 14 ni njaa zao tu,sio demokrasia.

Sent using Jamii Forums mobile app
Idea like this’s what kill CDM.. period
 
Hili jambo la Corona ni zito. Kila mmoja amepanic kivyake kujinasua. Mh. Rais wetu amejaribu kutuondoa hofu sawa na Kinjekitile na vita ya Majimaji au Al-Sayaf na Sadam Husein kwa vita na Wamarekani.
Kati ya Mbowe,Mh Rais na Spika,hakuna mwenye actual fact ya gonjwa hili na mwisho wake!!!! Hata China, USA nk hawana!

Issue ya kupata watu wengi kama mtaji wa Kisiasa au kukubalika Chama ni wrong perception kwa Tanzania yetu. Kinachoangaliwa zaidi, ni umemuweka mgombea wa sifa gani na bila kusahau "nguvu" ya umma katika usimamizi wa uchaguzi; hili kina Mch. Mtikila waliliona ck nyingi lilipelekea hata kufungua Kesi ya Mgombea Binafsi!
 
Unavyomwambia Mbowe aachane na propagandist kina Kigogo 2014 ni lini uliwaona wakisaini mkataba wa ushirikiano?!

Unataka chama kiachane na watetezi kina Maria Sarungi na wenzake ni lini uliwaona wakisaini mkataba wa ushirikiano? au unaposema chama kuwabeba una maana gani?!. Unadai kutaka demokrasia lakini hutaki wengine waseme.. why!

Hujui kuna wakati watu hufanana maoni/mawazo hasa wakati huu tulionao wa sampuli za papai kupelekwa maabara kupimwa Corona?

Hapo kwenye "personal attack" tuambie CDM wanamuattack nani ili tujue huyo mtu anastahili hizo attacks awe anaonewa?

Mbowe kuamua Wabunge wa CDM kujiweka karantini siku 14 ni kulingana na maelekezo ya wataalamu wa Afya, sio yake binafsi; unapoona Wabunge "wanaondoka" kwa ike spidi ulitaka na waendelee kukaa bungeni tu kama viazi? na hiyo demokrasia inayokupa uhuru wa kuchagua kifo ni ya kipuuzi. Wabunge wa CDM waliorudi bungeni kbl ya siku 14 ni njaa zao tu,sio demokrasia.

Huo mtazamo wa "mwananchi kijijini" ndio umeutumia ku- conclude kwamba CDM imeshindwa ku-win people's mind, sijui kama umewahi kufanya research toka uzaliwe.

All in all, umejitahidi kutoa mawazo yako, but umeacha gap nyingi sana kwenye hoja zako.

Sent using Jamii Forums mobile app

Wafuasi wa CDM mnafeli hapo.
haya,mwandishi ameacha gap,wewe andika hizo gap kujazia.
 
Ondoeni hizi takataka hapa JF

Mwandishi umeandika pumba,Nenda kawalishe kuku wa kisasa
uamuzi wa kutoshiriki Uchaguzi wa serikali za mitaa ulikuwa wa kipumbavu,tulikkuwa na mgombea kupitia chadema ambae anakubalika sana hapa kijijini lakini amekosa nafasi hiyo kwasababu ya kutoshiriki
 
Mwanaccm akijifanya mwanachadema, binafsi siamini lowasa ndo aliinua zaidi chadema pekee 2015 Ni uwongo.Hats Dr.slaa aliwahi kulipinga hili.
 
Andika wewe point sasa
hapa ndipo wafuasi wa CDM wanapofeli
Mwandishi ametoa point tupu,wewe unaandika pumba hapa
Kuna point ipi? Kataja Mange Kimambi, Maria Sarungi, Fatma Karume kuwa wasemaji wa chadema. Ni lini aliambiwa kuwa hao ni wanachama wa chadema? Anataka kuzuia wasitoe maoni huku yeye akiwa na haki hiyo na ndio maana kaleta uharo wake hapa?
 
Unavyomwambia Mbowe aachane na propagandist kina Kigogo 2014 ni lini uliwaona wakisaini mkataba wa ushirikiano?!

Unataka chama kiachane na watetezi kina Maria Sarungi na wenzake, again ni lini uliwaona wakisaini mkataba wa ushirikiano? au unaposema chama kuwabeba una maana gani?!.
Unadai kutaka demokrasia lakini hutaki wengine waseme.. why!

Hujui kuna wakati watu hufanana maoni/mawazo hasa wakati huu tulionao wa "sampuli za papai" kupelekwa maabara kupimwa Corona?

Hapo kwenye "personal attack" tuambie CDM wanamuattack nani ili tujue huyo mtu anastahili hizo attacks au anaonewa?

Mbowe kuamua Wabunge wa CDM kujiweka karantini siku 14 ni kulingana na maelekezo ya wataalamu wa Afya, sio yake binafsi; unapoona Wabunge "wanaondoka" kwa ile spidi ulitaka waendelee kukaa bungeni tu kama viazi? na hiyo demokrasia inayokupa uhuru wa kuchagua kifo ni ya kipuuzi. Wabunge wa CDM waliorudi bungeni kabla ya siku 14 ni njaa zao tu,sio demokrasia.

Huo mtazamo wa "mwananchi kijijini" ndio umeutumia ku- conclude kwamba CDM imeshindwa ku-win people's mind, sijui kama umewahi kufanya research toka uzaliwe.

All in all, umejitahidi kutoa mawazo yako, but umeacha gap nyingi sana kwenye hoja zako.

Sent using Jamii Forums mobile app

Utetezi wa kitoto kabisa, tena mtoto asiyejua kitu
 
Back
Top Bottom