Pole mwenyekiti wetu Mbowe, sikufundishi kazi ila ujue kazi hii ni yetu wote

Chadema siku zote ina watu makini Sana, Ila watu makini hawapewi nafasi kutumia umakini wao kukisaidia Chama

Mwandishi najua utapewa matusi Sana, lkin umeandika ukweli mwingi Sana

Chama makini hujibu hoja Kwa makini na sio matusi

Chadema ilikuwa zamani, unapigwa hoja za nguvu, zinamfanya mtetezi wa hoja akasirike yeye, ndivyo ilivyokuwa Chadema yangu ya zamani

Hi ya leo ya kutukana viongozi wa Dini!!!

Iko kazi kuitoa hapo na kuirudisha tena ulingoni
 
Hata uwe mwanasiasa mwenye kipaji gani..
Mradi jiwe ndo Rais basi hakuna siasa ya kufanya..

Mtaji wa Chadema wala haikuwa Dr Slaa wala nani..mtaji ulikuwa Kikwete..now hayupo..
AKILI..! Unapokuwa Kiongozi lazima Uwaza both Ndani na Nje ya Box. Ukiwaza tu Ndani ya Box na Kuzipa Kipaumbele Njia zilezile kwenye Vita Ileile Kwa Jamii ile ile lazima Ufeli. Ona Jamaa Hawa waliwahi kuwaza Jambo Kwa mapana Yake..!

Mark2:
3 Wakaja watu wakimletea mtu mwenye kupooza, anachukuliwa na watu wanne.

4 Na walipokuwa hawawezi kumkaribia kwa sababu ya makutano, waliitoboa dari pale alipokuwapo; na wakiisha kuivunja wakalitelemsha godoro alilolilalia yule mwenye kupooza.

5 Naye Yesu, alipoiona imani yao, akamwambia yule mwenye kupooza, Mwanangu, umesamehewa dhambi zako.

6 Na baadhi ya waandishi walikuwako huko, wameketi, wakifikiri mioyoni mwao,

7 Mbona huyu anasema hivi? Anakufuru. Ni nani awezaye kusamehe dhambi isipokuwa mmoja, ndiye Mungu?

8 Mara Yesu akafahamu rohoni mwake kwamba wanafikiri hivyo nafsini mwao, akawaambia, Mbona mnafikiri hivi mioyoni mwenu?

9 Vyepesi ni vipi, kumwambia mwenye kupooza, Umesamehewa dhambi zako, au kusema, Ondoka, ujitwike godoro lako, uende?

10 Lakini mpate kujua ya kwamba Mwana wa Adamu anayo amri duniani ya kusamehe dhambi, (hapo amwambia yule mwenye kupooza),

11 Nakuambia, Ondoka, ujitwike godoro lako uende nyumbani kwako.

12 Mara akaondoka, akajitwika godoro lake, akatoka mbele yao wote; hata wakastaajabu wote, wakamtukuza Mungu, wakisema, Namna hii hatujapata kuiona kamwe.
*********************

Hawa Walipo leta Mgonjwa walikutana na wagonjwa wengine Njiani ambao nao walitaka Huduma. Hivyo walipo taka Kutumia Njia zilezile Kwa watu walewale Kwa Huduma ile ile zikishindikana. Wakafeli, ila jamaa wakafikiria in a broad way. Wakapitia juu ya Paa imargine.

Kiongozi aliye Feli kuwaza husema Ah! HATUWEZI LOLOTE, IMESHINDIKANA! Na mara Nyingi huanza Kutukana hovyo hovyo na lawama Kila Siku Kumbe Ubongo wake Umegota. Lakini Kiongozi Anaye IJUA KAZI YAKE lazima AWAZE ZAIDI , Magumu ni Changamoto ya Kuwaza zaidi.

Mkulima Mjinga Hutegemea Mvua, Siku Mvua Ikiacha kunyesha lazima Afe Njaa. Atasema “Sasa Nitafanyaje, mvua Hakuna, Mvua lazima Ije ili tulime sasa Haipo Hatuna Cha Kufanya” Lakini mkulima Mwerevu Huwaza zaidi Ili asife Njaa.

AKILI inayo Tumika Chadema ni Ile ile Kwa namna ile ile! Mbaya zaidi Hakuna anaye Taka Kubadilika Hata Humu Akili za watu wengi wanao Comment ni zile zile Za Kusukuma bahari isogee iwapishe wakae. Na wakiona andiko lenye changamoto ya kweli Wanaumia hawalitaki, mioyo yao ishafeli.

Mjinga mmoja anasema Kwani Lini MAJERAHA HAYO tuliyafanya “washauri wa CHAMA” wapi MU zao. Hizi akili mfu kabisa. werevu hutazama mwenendo wa mtu sambamba na matamshi ya watu wengine. Ukiona mtu anawapigia kelele wengine “kojoeni barabarani, kojoeni barabarani..” na kweli Sauti Yake Ikabamba wakakojoa huhitaji kamusi au miwani kukufahamisha kwamba mshauri wa wakojoaji ni nani.
 
Naona unafikiri kwa kutumia masaburi, CCM hatuna ubavu wa kushindana na CDM kwenye uwanja huru. Ebu tujaribu tuone, watoke ma DED, Watendaji, Polisi, Nec na wengine wawe huru, tunapigwa asubuhi saa mbili.
Salaam Mwenyekiti wangu.. Leo Tarehe 5April Najaribu Kuvaa kiatu chako Kwa mtazamo wa Kila kitu Najua Uko kwenye wakati Mgumu Unajipa Mtima wa kusonga Mbele Labda maisha Yatapata Direction.

Nimepitia mitandaoni, majukwaa mengi ya Kijamii NIMESOMA Comments kwenye posts mbalimbali hasa zinazo husiana na Chama chetu, Kwa Upande wa Hasi na Chanya vyote, Na wakati NASOMA Natengeneza Picha na wewe ukisoma Najua HAKUNA ZINAZO KUFURAHISHA. Si Za wana CDM au CCM au Wapinzani WOTE WANACHEFUA TU. Hakuna mwenye True Solution ya Nini sasa Kifanyike Kwenye Sintofahamu hii.

Wewe ni MWENYEKITI wa Chama Kikuu hapa TZ. Lazima Uwe imara kuhakikisha Unakinasua kisogee Tena Mbele. Mimi Nina Ushauri kama Utaupokea Sawa kama Hauta upokea pia sawa. Ushauri ni Ushauri tu. Kabla ya Kushauri kidogo niweke Kumbukumbu..

Unakumbuka 2005, Tuanzie hapo, ulipata kura laki Sita, Sio mbaya. ilikuwa Duru la pili. Upepo wa kisiasa ulipwaya kutokana na historia ya mrema 1995 unakumbuka sina haja ya Kurudia huko. Nataka nifinyilie hapa karibuni.

Upepo mzito Kwa Chama Chetu Ulivuma ulipo muibua Dr Slaa 2010. Kishindo Cha Dr Slaa kilitokana na Kweli kadhaa na Ujasiri wake Bungeni wa Kuibua Kashfa mbalimbali. Ghafla watanzania Wakaibuka Kwa Nguvu kumshabikia sana. Kura zikakwea hadi milioni mbili Za Urais. Chama Kimetembea Kwa Nguvu Za Hoja, Bungeni na Nje ya Bunge. Hoja ambazo Wananchi walizielewa na zilikuwa Za kweli. Matarajio Hayo yakaja 2015. Lakini Mgombea wetu akawa na kasoro Kubwa kwenye masuala ya Ndoa Yake. Hali iliyofanya chama kuminyika sana. Matarajio ya Wananchi wote Yakahamia CCM Hasa Mechi ya UCHAGUZI ndani ya Chama hivyo. Ng’atana ng’atana ile WANANCHI wote matarajio yao na Macho yao yalikuwa Edward Lowassa. Chadema Tukafifia sana. Mawimbi ya Redio ya CCM Ndio yalisikika Kila KONA EDO! Lakini Tumaini la Watu wote EDO, Jamaa wakampiga Chini.. Mungu akasaidia Edo Akaja CDM.

Unakumbuka Edo alirudisha Form Kwa mbwembwe ambazo hazijawahi tokea. Mtaji Wa EDO ulitupatia Kura karibia milioni tano..achilia Mbali Wabunge 116 na madiwani. Mbali na mashambulizi mawili la Dr Slaa na Lipumba Ndani ya Ukawa Lakini Mtaji wa Mzee Yule Uliiweka CDM juu mno.

2020 Sasa Iko mbele Yetu.. imekaribia sana. NAJUA HATUNA KETE MKONONI. Tulisusia Uchaguzi wa Serikali ya mitaa Tukapigwa Jumla, Leo Dalili zinaonyesha rangirangi tena. HAPO LAZIMA TUJITATHIMINI.

Kabla ya Kujitathimini Tuna PEPO Tatu, Tuzijue

1: CHAMA HAKINA MSEMAJI:- Kwa sasa Mwana Chadema Yeyote ni msemaji kwenye Jambo Lolote. Kiongozi wa Chama anakurupuka tu kupost Majibu anayo waza Yeye mtandaoni Bila kufikiri kwamba wasomaji Wataelewa Ndio msimamo wa Chama. Viongozi wa Chama hawajui kwamba Hata post ya mtandaoni inayo Husu Chama ni Usemaji. Hii imeleta mkanganyiko mkubwa sana. Najua Inakuchanganya sana. Labda ni Utoto au Ulimbukeni wa kutumia Mitandao.

2: Tokea Mashambulizi ya Ndugu Yetu Lissu (MB) , kuna Upepo ulivuma kiasi Chama Kikapata wafadhiri MAJERAHA YA CCM. Wale Wafadhili ambao ni MAJERAHA ya CCM Ndio Chama Kimewabeba Jumla na wamekuwa Watetezi wa Chama Mitandaoni. Taratibu Chama kimewafanya miungu watu na hakina Ubavu wa Kuwakemea Hata wakikosea. Chama kimejivika Mavi na Hakiwezi kujivua mavi Hayo. Sikutaka kutaja Majina Lakini hapa naongelea watu kama Maria/Mange/shangazi n.k Nadhani Unaelewa. Hawa sio wabaya, ni wanachama Lakini MAJERAHA! Kila mmoja Ana JERAHA Ambalo hawezi kuwaza positive, Najua hamta penda lakini tunaongea kama kweli Tuna dhamira ya Kujenga Chama UPYA.

3: MA-PROPAGANDIST.. katikati ya Hawa MAJERAHA, kuna Kikundi kibaya Sana Kimeibuka, hiki Ndivyo kimeua kabisa Siasa Za Elite society Mitandaoni. Propagandist Hawa ambao Chama Kimekuwa kikiwafuatilia tena Kwa Karibu kama watetezi lakini wameshakipaka matope, Chama Kimeingizwa kwenye Shimo la mavi Bila Kujua. Propagandist Hawa kama KIGOGO, Wamejaribu kutunga Taarifa Za Uzushi kuaminisha Jamii kwamba wao ni antenas.. receiving informations Kila kona. Sometime wanarushiwa taarifa Flan na kuzifanyia kazi. Akili za Chama zote zimeshikwa na Kigogo na Hawa ni zaidi ya miungu watu hawaguswi!

Mzee Mwenyekiti CHAMA HAPO HAKIPO.. Tujitathimini..!

1: Kwanza Tujue Mitandao ipo, Hatuwezi kuwazuia watu Kupost watakayo na watakavyo. Lakini kama mwenyekiti kamata Usukani wa Gari lirudishe Barabarani Hao watu sio Muhimu kama Jamii Kubwa ya Watanzania wanao Taka Mageuzi. Raha ya Nchi ni Vyama Vingi yenye Nguvu. Sio dhaifu au Mfu.

2: Rudisha Chama Back to 2015 ambapo Tulikuwa Tukiongelea Matatizo ya Wananchi na Utatuzi wake Kuliko siku hizi ambazo Chama kimejikita kwenye personal attacks. Tukiendekeza hao MAJERAHA YA CCM Chama kitakuwa kama inzi kikishambulia watu Kila siku na mwisho Tutapotea. Wananchi hawako na Interest na Hayo.

3: Acha Maamuzi ya KIIMLA. Chama Cha Demokrasia Basi Hubiri Demokrasia. Ukiendekeza maamuzi ya Hulka, Mihemko na Imla Chama Kitakufia. See Hiki ni Chama Cha Demokrasia -hubiri Demokrasia Kwa Vitendo. Unakumbuka Baada ya Uchaguzi “UKUTA” ikafeli.. acha Ukuta Ukaamuru Maamuzi Mabaya Kabisa Yasiyo ya Kidemokrasia kukikataza Chama Kisishiriki Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa, ULIKOSEA MZEE, Watu walijiandaa wakaacha! Labda Ulikuwa na Plab “B” Kumbe Huna lolote ilikuwa munkari tu sasa Watu Hawana viongozi wa Msingi kabisa. Ungekuwa wa Kidemokrasia Ungesema Nduguzangu kutokana na Mapungufu haya ya Uchaguzi, na Tumefanya bidii hizi kurekebisha imeshindikana uongozi umeamua Kutoshiriki ila Kwa Sababu ya Demokrasia Mtu atakaye penda kushiriki Hazuiliwi hapo unge-exercise Democracy, Lakini pia UNGETOA PLAN “B” sio Kusema Hushiriki na Huna Plan B.

Makosa Hayo naona yanaendelea kwa kasi, Juzi UMETAMKA Wabunge watoke Bungeni kwamba pamejaa Corona. Ni Sawa Sipingi Lakini Unge-exercise Democracy Ukawaambia madhara ya Kuendelea na Bunge na Uamuzi we Chama kuwalinda wabunge wake kisha ukawapa Demokrasia na wao kuchagua atakaye endelea na asiye taka Kuendelea Ndio maana ya Demokrasia. Lakini PIA MAAMUZI Hayo Yanaonekana kukosa Hadhi ya Uongozi, Kama madaktari/manesi wako mstari wa mbele kupambana na pandemic wewe unajifungia ndani? Hii mzee Imeonyesha Udhaifu Mkubwa sana. Kiongozi anaye jijali mwenyewe na Mbinafsi. Contradiction Kubwa zaidi ni Pale Viongozi ambao Wamejiwekea karantini wanaonekana ofisini wakifanya Kazi Za Chama unajua ni KUJIVURUGA SANA.

4: THAMINI Walio Tufikisha Hapo. Mtu yeyote aliye Ipaisha au kuishika mkono CDM lazima aheshimiwe na sio KUFUATWA. Ni Vema Kuwa na Utu, 2015 Wana CCM wengi walikuja CDM. Lakini wengi wamerudi CCM, Tumewatukana, Tumewachamba, Tumewachora HUU SIO UTU. Mzee EDO Aliondoka Ukiwa Gerezani kweli Lakini hotuba yako ulipo toka Gerezani kuhusu Yeye Sikupenda Hata kidogo. Kiongozi asiye thamini Watu walio mshika mkono Wakati wa taabu Yake HAFAI. Ungempa Heshima Yake Ukamwacha. Viongozi wako wamemsema mitandanoni Ndio maana Nasema Chadema Kila mtu Msemaji. Mzee Gwajima Mzee Kakobe Hawa Walitutoa wapi, Kweli ni watu wa kuwashambulia leo!. Shukrani Gani. Hata kama hawapo Kwetu Tuna Yetu ya Kuyafanya ya Msingi.

5: Maisha Ya Chama Cha siasa ni ku-win citizens mind. CDM Kazi hiyo haifanyiki kabisa. mnadeal na Personal Atack! Kitu ambacho hakijawahi kusaidia! Baadae Wananchi watatuuliza mlitusaidia nini Wakati wa Corona majibu ni “tulikuwa tukimshambulia raisi” HAYA NDIO MAJIBU Ya kuwapa Wananchi Wakati wa Kampeni Kweli? .

Mwananchi mmoja wa Kijijini nilimsikia akisema “Chadema imekufa kweli yaani Gonjwa limeanzia China wao wanalifanya mtaji wa kisiasa” maneno yao yana Ukweli au Hayana Ukweli ila Result inayo patikana ni kwamba Tumefeli ku-win mindset zao.

Mwenyekiti Mbowe Sikufundishi Kazi Ila Ujue Kazi hii ni Yetu Wote. Kama Chama Kitakufa, 2020 wakawepo wabunge wa CCM Bungeni, sio kwamba Hali Itakuwa shwari Upinzani wa CCM Kwa CCM ni Mkali zaidi. Hivyo kama Chama kisipo jirekebisha Mapema Wenye akili wengi Watakimbilia CCM. Ndani wana mageuzi ila Nje CCM. Wakipata Nafasi BUNGE LA 2020 litakuwa CCM tu na Litakuwa HOT ZAIDI, maana Hakuna wakumwambia Ndio mzee Wala sio mzee Bali wote watoto wa nyumba moja ni Mnyukano zaidi.

ASANTENI.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Uchaguzi ulioisha hawakuwepo hao uliowataja?

Mbona huwa mnasema kwamba CCM waliponea NEC?

Leo kumeongezwa kitu gani?

Fikicheni Akili sio kulialia hapa
 
Mbowe ataibuka shujaa miaka michache ijayo, huu upepo utapita, kama ambavyo yesu ilibidi afe ili kuleta ukombozi.

Mh. Mbowe usikate tamaa tupo wengi nyuma yako
 
Jana usiku kaka yake Joseph Selasini amekufa kwa korona.

Korona ni hatari jamani tuache mzaa.
Hiyo ndo hoja iliyopo hapa mkuu? Au ndo Yale aloyasema mleta hoja?

Badala ya kujenga hoja mnakimbilia kuhoji mambo ambayo hayana msingi!

Ndugu yake huyo hajaanza yeye kufa naamini hata kwenu kifo kilishagafanya yake, na hata wewe si wa milele, siku usiyoijua, saa na dakika usizozijua na wewe utakwenda, utakwepa kifo wewe utaweza? Alikufa Babu yako sembuse wewe uliyekuja janajana
 
Pungaza jazba za kike alafu usinipangie cha kuandika.
 
Hili jambo la Corona ni zito. Kila mmoja amepanic kivyake kujinasua. Mh. Rais wetu amejaribu kutuondoa hofu sawa na Kinjekitile na vita ya Majimaji au Al-Sayaf na Sadam Husein kwa vita na Wamarekani.
Kati ya Mbowe,Mh Rais na Spika,hakuna mwenye actual fact ya gonjwa hili na mwisho wake!!!! Hata China, USA nk hawana!

Issue ya kupata watu wengi kama mtaji wa Kisiasa au kukubalika Chama ni wrong perception kwa Tanzania yetu. Kinachoangaliwa zaidi, ni umemuweka mgombea wa sifa gani na bila kusahau "nguvu" ya umma katika usimamizi wa uchaguzi; hili kina Mch. Mtikila waliliona ck nyingi lilipelekea hata kufungua Kesi ya Mgombea Binafsi!
Hujajibu hoja ,umekurupuka

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Salaam Mwenyekiti wangu.. Leo Tarehe 5April Najaribu Kuvaa kiatu chako Kwa mtazamo wa Kila kitu Najua Uko kwenye wakati Mgumu Unajipa Mtima wa kusonga Mbele Labda maisha Yatapata Direction.

Nimepitia mitandaoni, majukwaa mengi ya Kijamii NIMESOMA Comments kwenye posts mbalimbali hasa zinazo husiana na Chama chetu, Kwa Upande wa Hasi na Chanya vyote, Na wakati NASOMA Natengeneza Picha na wewe ukisoma Najua HAKUNA ZINAZO KUFURAHISHA. Si Za wana CDM au CCM au Wapinzani WOTE WANACHEFUA TU. Hakuna mwenye True Solution ya Nini sasa Kifanyike Kwenye Sintofahamu hii.

Wewe ni MWENYEKITI wa Chama Kikuu hapa TZ. Lazima Uwe imara kuhakikisha Unakinasua kisogee Tena Mbele. Mimi Nina Ushauri kama Utaupokea Sawa kama Hauta upokea pia sawa. Ushauri ni Ushauri tu. Kabla ya Kushauri kidogo niweke Kumbukumbu..

Unakumbuka 2005, Tuanzie hapo, ulipata kura laki Sita, Sio mbaya. ilikuwa Duru la pili. Upepo wa kisiasa ulipwaya kutokana na historia ya mrema 1995 unakumbuka sina haja ya Kurudia huko. Nataka nifinyilie hapa karibuni.

Upepo mzito Kwa Chama Chetu Ulivuma ulipo muibua Dr Slaa 2010. Kishindo Cha Dr Slaa kilitokana na Kweli kadhaa na Ujasiri wake Bungeni wa Kuibua Kashfa mbalimbali. Ghafla watanzania Wakaibuka Kwa Nguvu kumshabikia sana. Kura zikakwea hadi milioni mbili Za Urais. Chama Kimetembea Kwa Nguvu Za Hoja, Bungeni na Nje ya Bunge. Hoja ambazo Wananchi walizielewa na zilikuwa Za kweli. Matarajio Hayo yakaja 2015. Lakini Mgombea wetu akawa na kasoro Kubwa kwenye masuala ya Ndoa Yake. Hali iliyofanya chama kuminyika sana. Matarajio ya Wananchi wote Yakahamia CCM Hasa Mechi ya UCHAGUZI ndani ya Chama hivyo. Ng’atana ng’atana ile WANANCHI wote matarajio yao na Macho yao yalikuwa Edward Lowassa. Chadema Tukafifia sana. Mawimbi ya Redio ya CCM Ndio yalisikika Kila KONA EDO! Lakini Tumaini la Watu wote EDO, Jamaa wakampiga Chini.. Mungu akasaidia Edo Akaja CDM.

Unakumbuka Edo alirudisha Form Kwa mbwembwe ambazo hazijawahi tokea. Mtaji Wa EDO ulitupatia Kura karibia milioni tano..achilia Mbali Wabunge 116 na madiwani. Mbali na mashambulizi mawili la Dr Slaa na Lipumba Ndani ya Ukawa Lakini Mtaji wa Mzee Yule Uliiweka CDM juu mno.

2020 Sasa Iko mbele Yetu.. imekaribia sana. NAJUA HATUNA KETE MKONONI. Tulisusia Uchaguzi wa Serikali ya mitaa Tukapigwa Jumla, Leo Dalili zinaonyesha rangirangi tena. HAPO LAZIMA TUJITATHIMINI.

Kabla ya Kujitathimini Tuna PEPO Tatu, Tuzijue

1: CHAMA HAKINA MSEMAJI:- Kwa sasa Mwana Chadema Yeyote ni msemaji kwenye Jambo Lolote. Kiongozi wa Chama anakurupuka tu kupost Majibu anayo waza Yeye mtandaoni Bila kufikiri kwamba wasomaji Wataelewa Ndio msimamo wa Chama. Viongozi wa Chama hawajui kwamba Hata post ya mtandaoni inayo Husu Chama ni Usemaji. Hii imeleta mkanganyiko mkubwa sana. Najua Inakuchanganya sana. Labda ni Utoto au Ulimbukeni wa kutumia Mitandao.

2: Tokea Mashambulizi ya Ndugu Yetu Lissu (MB) , kuna Upepo ulivuma kiasi Chama Kikapata wafadhiri MAJERAHA YA CCM. Wale Wafadhili ambao ni MAJERAHA ya CCM Ndio Chama Kimewabeba Jumla na wamekuwa Watetezi wa Chama Mitandaoni. Taratibu Chama kimewafanya miungu watu na hakina Ubavu wa Kuwakemea Hata wakikosea. Chama kimejivika Mavi na Hakiwezi kujivua mavi Hayo. Sikutaka kutaja Majina Lakini hapa naongelea watu kama Maria/Mange/shangazi n.k Nadhani Unaelewa. Hawa sio wabaya, ni wanachama Lakini MAJERAHA! Kila mmoja Ana JERAHA Ambalo hawezi kuwaza positive, Najua hamta penda lakini tunaongea kama kweli Tuna dhamira ya Kujenga Chama UPYA.

3: MA-PROPAGANDIST.. katikati ya Hawa MAJERAHA, kuna Kikundi kibaya Sana Kimeibuka, hiki Ndivyo kimeua kabisa Siasa Za Elite society Mitandaoni. Propagandist Hawa ambao Chama Kimekuwa kikiwafuatilia tena Kwa Karibu kama watetezi lakini wameshakipaka matope, Chama Kimeingizwa kwenye Shimo la mavi Bila Kujua. Propagandist Hawa kama KIGOGO, Wamejaribu kutunga Taarifa Za Uzushi kuaminisha Jamii kwamba wao ni antenas.. receiving informations Kila kona. Sometime wanarushiwa taarifa Flan na kuzifanyia kazi. Akili za Chama zote zimeshikwa na Kigogo na Hawa ni zaidi ya miungu watu hawaguswi!

Mzee Mwenyekiti CHAMA HAPO HAKIPO.. Tujitathimini..!

1: Kwanza Tujue Mitandao ipo, Hatuwezi kuwazuia watu Kupost watakayo na watakavyo. Lakini kama mwenyekiti kamata Usukani wa Gari lirudishe Barabarani Hao watu sio Muhimu kama Jamii Kubwa ya Watanzania wanao Taka Mageuzi. Raha ya Nchi ni Vyama Vingi yenye Nguvu. Sio dhaifu au Mfu.

2: Rudisha Chama Back to 2015 ambapo Tulikuwa Tukiongelea Matatizo ya Wananchi na Utatuzi wake Kuliko siku hizi ambazo Chama kimejikita kwenye personal attacks. Tukiendekeza hao MAJERAHA YA CCM Chama kitakuwa kama inzi kikishambulia watu Kila siku na mwisho Tutapotea. Wananchi hawako na Interest na Hayo.

3: Acha Maamuzi ya KIIMLA. Chama Cha Demokrasia Basi Hubiri Demokrasia. Ukiendekeza maamuzi ya Hulka, Mihemko na Imla Chama Kitakufia. See Hiki ni Chama Cha Demokrasia -hubiri Demokrasia Kwa Vitendo. Unakumbuka Baada ya Uchaguzi “UKUTA” ikafeli.. acha Ukuta Ukaamuru Maamuzi Mabaya Kabisa Yasiyo ya Kidemokrasia kukikataza Chama Kisishiriki Uchaguzi wa Serikali Za Mitaa, ULIKOSEA MZEE, Watu walijiandaa wakaacha! Labda Ulikuwa na Plab “B” Kumbe Huna lolote ilikuwa munkari tu sasa Watu Hawana viongozi wa Msingi kabisa. Ungekuwa wa Kidemokrasia Ungesema Nduguzangu kutokana na Mapungufu haya ya Uchaguzi, na Tumefanya bidii hizi kurekebisha imeshindikana uongozi umeamua Kutoshiriki ila Kwa Sababu ya Demokrasia Mtu atakaye penda kushiriki Hazuiliwi hapo unge-exercise Democracy, Lakini pia UNGETOA PLAN “B” sio Kusema Hushiriki na Huna Plan B.

Makosa Hayo naona yanaendelea kwa kasi, Juzi UMETAMKA Wabunge watoke Bungeni kwamba pamejaa Corona. Ni Sawa Sipingi Lakini Unge-exercise Democracy Ukawaambia madhara ya Kuendelea na Bunge na Uamuzi we Chama kuwalinda wabunge wake kisha ukawapa Demokrasia na wao kuchagua atakaye endelea na asiye taka Kuendelea Ndio maana ya Demokrasia. Lakini PIA MAAMUZI Hayo Yanaonekana kukosa Hadhi ya Uongozi, Kama madaktari/manesi wako mstari wa mbele kupambana na pandemic wewe unajifungia ndani? Hii mzee Imeonyesha Udhaifu Mkubwa sana. Kiongozi anaye jijali mwenyewe na Mbinafsi. Contradiction Kubwa zaidi ni Pale Viongozi ambao Wamejiwekea karantini wanaonekana ofisini wakifanya Kazi Za Chama unajua ni KUJIVURUGA SANA.

4: THAMINI Walio Tufikisha Hapo. Mtu yeyote aliye Ipaisha au kuishika mkono CDM lazima aheshimiwe na sio KUFUATWA. Ni Vema Kuwa na Utu, 2015 Wana CCM wengi walikuja CDM. Lakini wengi wamerudi CCM, Tumewatukana, Tumewachamba, Tumewachora HUU SIO UTU. Mzee EDO Aliondoka Ukiwa Gerezani kweli Lakini hotuba yako ulipo toka Gerezani kuhusu Yeye Sikupenda Hata kidogo. Kiongozi asiye thamini Watu walio mshika mkono Wakati wa taabu Yake HAFAI. Ungempa Heshima Yake Ukamwacha. Viongozi wako wamemsema mitandanoni Ndio maana Nasema Chadema Kila mtu Msemaji. Mzee Gwajima Mzee Kakobe Hawa Walitutoa wapi, Kweli ni watu wa kuwashambulia leo!. Shukrani Gani. Hata kama hawapo Kwetu Tuna Yetu ya Kuyafanya ya Msingi.

5: Maisha Ya Chama Cha siasa ni ku-win citizens mind. CDM Kazi hiyo haifanyiki kabisa. mnadeal na Personal Atack! Kitu ambacho hakijawahi kusaidia! Baadae Wananchi watatuuliza mlitusaidia nini Wakati wa Corona majibu ni “tulikuwa tukimshambulia raisi” HAYA NDIO MAJIBU Ya kuwapa Wananchi Wakati wa Kampeni Kweli? .

Mwananchi mmoja wa Kijijini nilimsikia akisema “Chadema imekufa kweli yaani Gonjwa limeanzia China wao wanalifanya mtaji wa kisiasa” maneno yao yana Ukweli au Hayana Ukweli ila Result inayo patikana ni kwamba Tumefeli ku-win mindset zao.

Mwenyekiti Mbowe Sikufundishi Kazi Ila Ujue Kazi hii ni Yetu Wote. Kama Chama Kitakufa, 2020 wakawepo wabunge wa CCM Bungeni, sio kwamba Hali Itakuwa shwari Upinzani wa CCM Kwa CCM ni Mkali zaidi. Hivyo kama Chama kisipo jirekebisha Mapema Wenye akili wengi Watakimbilia CCM. Ndani wana mageuzi ila Nje CCM. Wakipata Nafasi BUNGE LA 2020 litakuwa CCM tu na Litakuwa HOT ZAIDI, maana Hakuna wakumwambia Ndio mzee Wala sio mzee Bali wote watoto wa nyumba moja ni Mnyukano zaidi.

ASANTENI.
Kinachonitia imani ni kwamba CDM ni chama cha umma na kwamba hata wakihama akina Mbowe chama kinakuwepo tu, tusonge mbele. Mimi nilifikiri chama kingekufa alipoondoka Slaa, akaja Lowasa na hata Sumaye na wengine wengi tu bado chama ni kile kile CDM na nyota yake inang'aa sana.
 
Chadema siku zote ina watu makini Sana, Ila watu makini hawapewi nafasi kutumia umakini wao kukisaidia Chama

Mwandishi najua utapewa matusi Sana, lkin umeandika ukweli mwingi Sana

Chama makini hujibu hoja Kwa makini na sio matusi

Chadema ilikuwa zamani, unapigwa hoja za nguvu, zinamfanya mtetezi wa hoja akasirike yeye, ndivyo ilivyokuwa Chadema yangu ya zamani

Hi ya leo ya kutukana viongozi wa Dini!!!

Iko kazi kuitoa hapo na kuirudisha tena ulingoni
Umeongea ukweli mtupu mkuu, watu makini hawana nafasi ndani ya chama, chama kwa sasa hakina watu kabisa wa kupambana.
 
Back
Top Bottom