Pokea ujumbe ewe wakala

Goliath mfalamagoha

JF-Expert Member
Aug 3, 2012
602
2,505
Dear wakala wa chama,

Salamu sana.

Natumaini u mzima na umejiandaa vema kusimamia maamuzi yetu.

Najua una 'mchecheto' hivi, ile hali ambayo mtu hujisikia anapokuwa anatarajia kufunga ndoa na mpenziwe anayempenda sana. Presha si presha, kiwewe si kiwewe. Kwa ujumla utulivu unakuwa mdogo, kadri siku zinavyosogea. Moyo unakulipuka kila ukiiwaza siku ya tukio.. Itakwendaje, nk.

Nakuandikia kukutia moyo, kwamba wewe ni jiwe la msingi ambalo likitetereka, basi nyumba ipo mashakani. Wewe ni wa muhimu hivyo.

Leo nilipata muda wa kuzungumza na mshikaji wangu ninayemkubali kindakindaki. Tulikuwa tukikuteta wewe. Mshikaji akauliza, 'hivi kweli wakala apewe elfu kumi, haitoshi hata kidogo, si atanunuliwa huyo?'

Nikamjibu, 'Hivi ni fedha kiasi gani mtu akipewa atasema INATOSHA?, Wabunge na madiwani walionunuliwa walikuwa wanalipwa elfu kumi?'

Mpendwa wakala,
Si kwamba nakataa wewe kuongezewa dau, au naamini elfu 10 ni kubwa au ndogo, nataka nikueleze hoja yangu niliyompa mshikaji wangu.

Hoja yangu ni hii.
Kusema ukweli kabisa, HAKUNA kiasi chochote ambacho utampa wakala kitakacholingana na kazi anayoifanya. Ndio kusema, wakala anajitolea mwili, roho na akili yake kwa taifa. Yaani wakala ni sawa na askari aendaye vitani...

Askari hupewa bunduki na risasi (naipa thamani ya elfu 10). Je, ni kweli silaha ile ndio italinganishwa na thamani ya kujitoa kwake kwenda vitani? Hasha. Kinachompeleka ni UZALENDO... Na uwakala vile vile.

Mpendwa wakala,
Ni heshima kubwa kusimamia maamuzi ya wengine kwa uaminifu. Mpaka uaminiwe maana yake wewe ni wa pekee sana. Kinachotakiwa kutazamwa ni heshima na tunu ya uaminifu uliyopewa. Kwamba heshima hiyo itaambatana na nini (fedha nk.) hilo si la kuzingatia.

Ndio kusema, malipo makubwa ili usimamie maamuzi yatamaanisha kuwa imani ya wanaokutuma ni NDOGO kiasi kwamba wanadhani fedha ndiyo motisha. Wanaopewa fedha kidogo maana yake imani waliyo nayo wanaokutuma ni KUBWA kupindukia... Ni kama umejitolea bure halafu waliokutuma wakaona haya usiende mikono mitupu... Just a token of appeciation...

Najua mshikaji wangu atasoma, naamini naye atakutia moyo. Tunataka ujue kuwa tunu ya uaminifu imelala moyoni mwako, na kuwa sehemu ya kutunza maamuzi ni taji isiyosahaulika. Tunakuamini, tunajua hutanunulika hata wakija na meli ya fedha inayotambaa nchi kavu.

Mwisho kabisa, usiache kumwomba Mwenyezi Mungu akupe ujasiri, shetani ana mambo yaliyopakwa rangi za kifalme, anaweza kukuletea tope lililopakwa rangi ukadhani ni kipande cha embe. Sisi wenye maamuzi pia tunakuombea ili uitambue thamani ya heshima tuliyokupa katika kusimamia maamuzi yetu.

Wasalaam,
Mpenda amani, na haki.

#unaweza_kushare mawakala wapokee salamu
 
Back
Top Bottom