(Tazama Gazeti la Mwananchi)Akijibu hoja hizo, Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa, Dk Hussein Mwinyi alisema Serikali ya Tanzania inalipa uzito mkubwa suala hilo na Waziri Mkuu Mizengo Pinda ataongoza jopo litakalokutana na wenzao wa Malawi Februari kuanza mazungumzo.
huyu ni mtoto wa Mkulima kama anavyojinadi mwenyewe na yeye ni mkulima...Huwezi kumlinganisha na Lowasa yeye amekaa ki-bizness zaidi.Si unajua wakulima siku zote hukandamizwa kwa kupangiwa bei duni ya mazao hawana sauti hawa wakulima alwayz.
Pinda ni mchapa kazi na yuko makini katika maamuzi yake huyo lowasa ni richmundHivi karibuni suala la mgogoro wa kimpaka kati ya Malawi na Tanzania limeibuka Bungeni na Waziri Mkuu Mizengo Pinda inasemekana ataongoza jopo kwenda Malawi ili kufanya mazungumzo. (Tazama Gazeti la Mwananchi)
Mimi sina imani kabisa na Waziri Mkuu huyu Mizengo Pinda ambaye huwa anaonesha udhaifu mkubwa hasa pale anapobanwa kuhusu hoja aliyoitoa mwenyewe. Kwa mfano kuhusu suala la mauaji ya albino huyu bwana alilia pale Bungeni! Suala la Zanzibar ni nchi au la alilianzisha mwenyewe lakini likamlipukia na kumrudi mwenyewe. Suala la Mahakama ya Kadhi, alidai kwamba kuleta mahakama hizi itakuwa ni kuleta fujo, lakini baada ya muda mchache akakimbia tena kwa mashekhe na kwenda kujisalimisha na kudai kwamba hakuna aliyezuia Mahakama hizi kuanzishwa!
Sasa hivi anataka kuanzisha mazungumzo na Malawi! Sijui ataibua nini huko maskini! This man is too weak for negotiation and I don't trust him! Afadhali hata ya Lowasa ambaye aliiambia Serikali ya Misri kwamba sisi tutaendelea kutumia maji ya Ziwa Victoria bila kujali Mkataba wa Mwaka 1929 kati ya Serikali ya Misri na Serikali ya Tanganyika ambao unataka ruhusa ya Serikali ya Misri kabla ya kutumia maji ya Ziwa Victoria na Mto Nile kwa ujumla. Sijui hapa Pinda wetu angesemaje?
Mimi naona huyu PM aachane na utatuzi wa migogoro kwa kuwa anaonekana ni mnyonge mno kutatua na watamkandamiza tu!
Pinda ni mchapa kazi na yuko makini katika maamuzi yake huyo lowasa ni richmund
Uko sawa kabisa mkuu kwa hii ishu jamaa atashindwa, he is too weak!
Kaaazi kweli kweli! Huyu bwana atawaambia kwamba "ili kudumisha amani" basi sisi hatuna tone hata moja la maji ya Ziwa Nyasa! Ni afadhali tuwe na mgogoro ambao unatuwezesha kutumia sehemu ya Ziwa Nyasa kuliko kutokuwa na mgogoro ambao utatuwezesha kukosa Ziwa hilo!
Sioni hoja yoyote ya msingi katika mjadala huu, badala yake naona ni chuki binafsi tu zinaelekezwa kwa PM wetu. Hoja kwamba aliwahi kutoa machozi Bungeni kuhusu mauaji ya Maalbino linahusiana vipi na negotiation katika suala la mpaka wa Malawi na Tz? Hata hizo hoja nyingine hazithibitishi kwamba PM wetu ni weak. Wengi wetu tumezoea kuongozwa na viongozi wenye mbwembwe na maneno mengi ya kutaka sifa, huku wakiliibia taifa kwa njia za ujanja ujanja. Tunataka viongozi waadilifu na Pinda ni mmoja wapo.
Mhe. PM ni m deplomasia mno kuliko Papa!..pengine shida ipo kwenye "negotiation skills" Liliongelewa hilo kwenye Taarifa ya Dr. Mwakyembe kuhusu Richmond kuwa watumishi wengi wa umma, hopeful PM inclusive, hawana taaluma ya "majadiliano". Aidha, uzoefu waonyesha kuwa wengi ya watumishi waliofanya kazi Ikulu huwa ni kama wafuasi wa YESU Mnazareti, wao kila kitu ni "YES, YES.." hata kama panasitaili "BIG NO.." nidhamu yao ni kama ya gheshi, hakuna kubishana na Afande!