PM Majaliwa: Bwawa la umeme kukamilika Juni 2022

The Assassin

JF-Expert Member
Oct 30, 2018
4,355
17,320
Waziri mkuu wa Tanzania Bwana Majaliwa leo ametembelea mradi wa ujenzi wa bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere na kuangalia maendeleo ya ujenzi.

Majaliwa ameridhika na kasi ya ujenzi wa mradi huo na amesisitiza utakamilika kwa wakati mwaka 2022 mwezi wa 6 kama majubaliano yalivyo.

PM amesema mradi utakamilika kama ilivyopangwa kwani pesa zipo hakuna sababu ya kuchelewesha mradi.

PM amasema mradi huo utatoa faida kubwa kwa uchumi wa nchi yetu kwani mradi utaleta umeme wa bei nafuu sana kwa watanzania.

Kwa wasiojua.

Kuzalisha Unit moja ya umeme wa maji hua ni TZS 36, Nuclear TZS 66, Jua TZS 105, Joto Ardhi TZS 114.5, Gas 150 na Mafuta mazito 460.

Kwa kuangalia hizo unit price unaona wazi kabisa kua hakuna source yoyote ya nishati yenye gharama ndogo kama maji.

 
Tuombe Mungu iwe hivyo maana msimu huu maneno yamekuwa mengimengi.

Vv
Achana na waganga njaa kina mhongo, wale ni madalali wa makampuni ya mitambo ya gas kama kina General Electric ya Marekani ambao aliwapigania hadi kupata tenda ya kujenga ama kuleta engine zao pale Kinyerezi.

Sasa naona wanamlipa mhongo awapigie debe kwani ujio wa umeme wa maji utawaondolea network yao ya ulaji wa services and maintenance pale Kinyerezi ambapo wanakula 30 Billioni kwa mwezi kwa matengenezo. Hapo ni Kinyerezi tu.
 
Waziri mkuu wa Tanzania Bwana Majaliwa leo ametembelea mradi wa ujenzi wa bwawa la umeme la Mwalimu Nyerere na kuangalia maendeleo ya ujenzi...
Sina tatizo na hii project kabisa ila sina imani kabisa na wanasiasa wa ccm, hizi calculations tulishapigiwa sana lakini hakuna tulichoambulia.

Lakini pia tukipiga hesabu hizo lazima tujue kuwa Hydro inaonekana ina bei nafuu kwa sababu gharama za uharibifu wa mazingira haziingizwi kwenye hizo hesabu.

Ni kama vile mkaa unaonekana ni nafuu kuliko gesi kwa sababu gharama za deforestation haziingizwi kwenye bei. Tungekuwa tunajumuisha na gharama ya kupanda upya miti na athari katika tabia nchi, bei ya mkaa isingeshikika.
 
Achana na waganga njaa kina mhongo, wale ni madalali wa makampuni ya mitambo ya gas kama kina General Electric ya Marekani ambao aliwapigania hadi kupata tenda ya kujenga ama kuleta engine zao pale Kinyerezi

Sasa naona wanamlipa mhongo awapigie debe kwani ujio wa umeme wa maji utawaondolea network yao ya ulaji wa services and maintenance pale Kinyerezi ambapo wanakula 30 Billioni kwa mwaka kwa matengenezo. Hapo ni Kinyerezi tu.
Muhongo ni takataka kabisa
 
Back
Top Bottom