toa bei acha longo longo
Habari wandugu
Kuna kiwanja kinauzwa Mtwara Mjini Kipo mtaa wa kilimahewa, kiwanja hiki kinukubwa wa eneo la mita za mraba zaidi 2300 ( kama nusu heka), Sehemu yote ya maeneo haya imepimwa ila hapajaanza kujengwa.
hicho kiwanja,kipo kwenye mwinuko bahari unaiyona kwa mbali na mikoko ya baharini ipo umbali wa nusu km kutoka kwenye kiwanja hicho.
Kwa yeyote anayetaka kukiona hicho kiwanja au kupata maelezo zaidi piga simu na. 0784 707789
huyu hayuko serious, halafu hawa madalali siku hizi asilimia 90% yao ni matapeli hawana hata kiwanja cha kukanyagia miguu yao iliyopinda. NB: lakini kwa huyu sina uhakika, pengine ni mtu mwema,...ila tunaomba atoe bei, kama hatoi bei ameleta cha nini hapa? unataka namba zetu za simu tukupigie ili uzifanyie nini? uzitumie kututapeli au kutapeli ndugu zetu?/
Jamani ehe!
Nimegoogle earth hilieneo la viwanja, kwa maana ya kwamba bara bara kuu kuelekea mikindani/Lindi/Dar inaonekana pamoja na bahari inaonekana.Kwa hiyo hii picha inatoa ufafanuzi mzuri kuhusu hiki kiwanja, na wale wenye pesa zao wataweza kutathmini thamani ya hii asset/kiwanja. Sasa naomba mnielekeze wanajamii jinsi ya kuattach hii picha/ramani mimi sijui
Asante
Unatumia kompyuta au simu?
Kama unatumia computa save picha kwenye kompyuta the ukiwa unapost JF angali juu ya message box kuna tools panel, ukiweka arrow yako kwenye hizo tools utaona moja imeandikwa insert image (hii ni ya saba toka kulia mstari wa chini), click hiyo then fuata maelekezo...
Nashukuru kwa maelekezo ZeMarcopolo
Kama nimekuelewa vizuri, Kwa hiyo inabidi nipost upwa.
Nafanya hivyo sasa hivi