PlayStation 4 Neo: Ujio wa toleo jipya la PS4 mbioni..

RASHEEDMTOI

Member
Apr 13, 2015
85
68
Kwa miezi kadhaa sasa watumiaji wa intaneti wamekuwa wakiongelea toleo jipya la PS4 ambayo inasemekana itakuwa ndogo zaidi kuliko toleo la hivi sasa iliyopewa jina la “Sony PlayStation 4 Neo”.

Toleo hilo jipya la PS4 litakuwa na muenekano wa picha bora zaidi na pia itakuwa na CPU ambayo itakuwa na kasi zaidi (2.16GHz) kutoka 1.16GHz kwenye toleo la sasa la PS4 pia inasemekana itakuwa na uwezo wa kusupport “Ultra HD Blu-ray playback (4K)”.

Aidha Microsoft nao wanasubiriwa watatoa nini baada ya toleo jipya la PS4 kutoka. “Xbox One” ni toleo lililo chini ya Microsoft ambayo bado haina nguvu ukilinganisha na toleo la hivi sasa la PS4 ambapo Microsoft wanashauriwa kuifanyia maboresho Xbox One.

Kwa habari za hivi karibuni zinasema Microsoft watatoa kifaa cha kucheza game mwakani ambacho kitasupport kifaa cha kuvaa kwenye macho kiitwacho “Oculus Rift” huku Sony wakisema kuwa tutaona ujio watoleo jipya la PS4 baadae mwaka huu ambazo zitakuwa na ukubwa wa kutunza data mpaka 2TB.

Pia, itakuwa ni ndogo, nyembamba zaidi kuliko toleo la sasa hivi na pia kuna uwezekano PS4 Neo itauzwa pamoja na kifaa cha kuvaa kwa ajili ya kuongeza uhalisia cha PVR (Virtual Reality). Kwa muda mrefu Sony wamekuwa wakitengeneza kifaa hicho kwa ajili ya kifaa chake cha magemu cha PlayStation.

Source TEKNOKONA
 

Attachments

  • 1464687072295.jpg
    1464687072295.jpg
    15.4 KB · Views: 84
usitegemee hio power itumike kwenye gaming itakuwa tu ni mambo mengine kama kuplay video za 4k. sony hawawezi kujichimbia shimo kwa kutoa ps4 yenye nguvu sababu games mpya hazitacheza kwenye ps4 za zamani na kuleta malalamiko mengi
 
Xbox One Scorpio duh!! Ni balaa slim kuliko ile ya kwanza alafu nasikia eti round hii PS4 inaweza kupigwa K.O na Xbox One Scorpion kwenye Spec
 
nimeshangaa eti pc gaming zina bei kuliko hizo play station n xbox. yan gaming pc ni million kwenda mbele.
 
nimeshangaa eti pc gaming zina bei kuliko hizo play station n xbox. yan gaming pc ni million kwenda mbele.
mkuu hizi playstation na xbox ni low end gaming kwa watu wasio na hela, kama ps3 karibia games zote hazifiki 720p (hd ya kawaida) nyingi ni 540p ambayo ni ndogo sana na ps4 na xbox one games nyingi ni 720p chache zinafika 900p na zinazofika 1080p zinahesabika. Pc yenyewe ni mnyama mwengine inaenda hadi 4k, kuna watu gpu ghali na highend kama gtx 1080 haziwatoshi inabidi wazieke mbili kwa pamoja ili wacheze games kwa 4k, bado hapo hajaanza kugame na VR headset atahitaji power zaidi.

kifupi pc gaming ipo advanced sana kulinganisha na hizo console.
 
Back
Top Bottom