PIUS Msekwa Amvaa Nape

PIUS Msekwa Amvaa Nape

Atakuwa mnafiki huyu Msekwa, hivi hajiulizi kwanini Watanzania wamefikia hatua mpaka ya kuamua kulinda kura zao katika majimbo mbali mbali nchini?

Haiwezekeni mchezaji makini aliejindaa kwa mechi afunge bao kwa mkono. Goli kama hilo litafutwa na refa. Naomba wananchi wapuuzie maneno ya upuuzi kama hayo.

kufunga goli la mkono ni faul na moja kwa moja litakataliwa na refa ambayo ni tume ya uchaguzi. Kauli mbaya kama hizo zinaweza kufanya wananchi kukosa imani na serikali na kuleta machafuko na ninaamini haya ninayoyasema ndio msimamo wa chama changu... Pius Msekwa.... 2.07.2015 (ITV, kipindi cha Mzelendo)....
 
Magoli ya mkono ndiyo yanayoifanya ccm iendelee kubaki madarakani. Nape yuko sahihi.

Zanzibar, CCM magori ya mkono kama hayo ni kawaida, kila mechi wanazidiwa wanaokolewa na magori ya mkono. Pius aache Nape aendelee kuropoka point.
 
Nape ndo msemaji wa ccm mwaka huu ccm mtaruana hata kuuana kila mwaka huu lazima muondoke madarakani
 
Tunaweza kumlaumu nape lakini goli la mkono ndiyo uwezo wa c.c ulipofikia
 
Habari ya mjini ni lowasa. ...ccm wakmptsha lowasa kura za vijana wanazo tunataka fursa lowasa kashba hatutak rais njaa wa kutuletea ma dc njaa kama kna makonda

pole sana nani kakwambia kuna kijana wapenda rushwa wewe peke yako tu
 
Narudia tena asiyetaka basi ahamie nchi nyingine kwani H.E EDWARD LOWASA ndo next Presida of die U.R.T 2015-2020.
 
mzee msekwa hana chochote aliwai kutoa ushauri wa hovyo kabisa anasema watoe mchunjo waache wajumbe wawapie kula bila kumchuja hata mmoja ,nilimshaangaa nikamuona kumbe ndo walewale wakina kingunge,
 
Hata huyu Mzee amepima haliya hewa akaona asawazishe ki style.Ni kweli Mzee Msekwa hajui kama Chama chake ni mabingwa wa magori hayo?.Team yake haijawahi kufunga gori lahivyo nayeye akiwemo kwenye team?,aache kutuhadaa na ajue tunatambua kauli hiyo ya Nape ndi kauli ya Chama chao

Unafahamu wakati mwingine nasi wananchi tusipende kulala sana kama alivyotuambia kiongozi mmoja kuwa watz hulala usiku na mashine/vitendea kazi/mitambo nayo inaachwa kulala. Wakati mwingine haya matamko makubwa hivi na yasiyochukuliwa hatua ni maagizo toka kwa viongozi wa juu kuwa waelezeni hivyo kuwakatisha tamaa wapinzani. Kwani kule Bagamoyo mtoto wa kigogo alipotamka hadharani kuwa kiongozi wa nchi hii hatatoka kaskazini na hayupo alieikana kauli hiyo kuwa sio msimamo wa chama wala serikali mlishasahau?
 
Nape ni mropokaji,Hotuba ya bosi wake Kinana pale Mwanza ilikuwa ya kupigiwa mfano ingawa imekuja siku za mwisho za utawala wa CCM! yeye kazi yake ni kuropoka tu,

Ameshindwa kuyavua magamba mpaka yanataka kuingia ikulu,atavuliwa yeye ingawa magamba ni ngumu kuingia ikulu.
 
Nape alichokieleza ndicho kinachofanyika, nadhani nape siyo mnafiki kaamua kusema ukweli. Hata msekwa anaujua ukweli huu, lakini haya mambo hayadumu hata kidogo!
Kwa lugha nyingine, hata watu wanaolala vituoni wakisubiri kujiandikisha wanajisumbua tu kwa sababu kura zao ni insignificant! Fucken nape
 
Mungu kawaumbua mumeanza kuwekana peupe wenyewe kwani nina asiyejua kuwa CCM ni wezi?,kabla ya hapo Mungu alikuwa ana tumia vinywa vya watu wengine kuusema wizi wa CCM safari hii amewaumbua kwa kutumia vinywa vyao wenyewe.
 
Mzee Msekwa unakumbuka wakerewe walivyokunyoa ulivyotoa kauli kama hiyo ya Nape? Lakini ni kweli sasa unaonyesha Uzee dawa maana yalishakukuta.
 
Back
Top Bottom