Pius Msekwa akoshwa na uongozi wa Rais Samia

benzemah

JF-Expert Member
Nov 19, 2014
1,503
2,980
Spika mstaafu wa Bunge, Mzee. Pius Msekwa, amesema maridhiano ya kisiasa vya yaliyofanywa na serikali dhidi ya vyama upinzani, yamedumisha utulivu na kuondoa migogoro ya kisiasa huku akisisitiza njia sahihi ya kutatua kero za muungano ni njia ya mazungumzo.

Msekwa alitoa kauli hiyo nyumbani kwake Mtaa wa Bomani wilayani Ukerewe mkoani Mwanza wakati alipokuwa akizungumzia miaka 59 ya Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.

"Kiongozi tuliye naye wa Awamu ya Sita amekuja na staili yake nzuri ya kujitahidi kuondoa migogoro ya kisiasa ambayo ingeweza kutukwamisha. Ilikuwa inaleta malalamiko kutoka kwa vyama vingine vya siasa kuzuwa kufanya shughuli za siasa ambayo ni kazi yao," alieleza.

Mbunge huyo wa zamani wa Ukerewe na Katibu Mkuu wa TANU na CCM kwa nyakati tofauti, Rais Dk. Samia Suluhu Hassan, amelenga kuhakikisha wananchi wanaishi kwa amani na utulivu na ndio sababu ya kuja na maridhiano ya kisiasa.

"Kwa hiyo tutazamie kwamba huko tunakokwenda angalau katika kipindi hiki tutakuwa tunaishi katika nchi ya asali na maziwa,"alisema Spika huyo mstaafu.

Akizungumzia kuhusu muungano wa Tanganyika na Zanzibar, alisema kero zipo lakini zimeendelea kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo.

"Bado kuna matatizo madogo, nadhani mnayasikia yanaitwa kero za muungano lakini zimeendelea kutatuliwa kwa mazungumza ya kirafiki na kidugu baina ya pande zote mbili, "alieleza.

"Nimekuwa Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu, ambayo inahusika na mambo ya utawala wa kiserikali, najua kulikuwa na kamati, muda wote kumekuwa na kamati za Serikall ya Muungano wa Tanzania baina ya Serikali ya Zanzibar, ikitokea kuna jambo wanalizungumza, wanazungumza namna ya kuliondoa hilo tatizo, alisema.

Kwa mujibu wa spika huyo mstaafu, alisema maridhiano yamesababisha kuwepo amani na kutokuwepo migogoro ambayo ingetuletea matatizo katika uendeshaji wa nchi huku akimwagia sifa Rais Dk. Samia kwa mtindo bora wa uongozi wake.
 
kero za muungano lakini zimeendelea kutatuliwa kwa mazungumza ya kirafiki na kidugu baina ya pande zote mbili, "alieleza
Neno hili lna nikwaza '' pande zote mbili,''
Hivi Pande mbili alikusudia nini? Zanzibar na nani ?
Ikiwa upande wa pili ni Tanganyika unawakilishwa na nani?
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom