Pitio la kitabu mimi, Umma Party na mapinduzi ya Zanzibar Mwandishi: Hashil Seif Hashil

Mohamed Said

JF-Expert Member
Nov 2, 2008
21,184
30,530

Kuandika historia ya ukombozi katika nchi za Kiafrika kunahitaji ujasiri mkubwa sana na sababu yake ni kuwa Afrika ina historia rasmi. Historia hii rasmi ni ile ambayo imepitishwa na kukubalika na watawala. Historia hii ikishaandikwa ndiyo mwisho kwani haitoi nafasi ya kuwapo kwa historia nyingine itakayokwenda kinyume na hiyo. Hii ni moja ya sifa ya siasa katika Afrika. Historia rasmi ndiyo hiyo itakayokuwa katika mitaala kuanzia shule ya msingi hadi chuo kikuu. Hatari yake ni kuwa inasababisha na pengine kwa miaka mingi sana kusomeshwa historia yenye upungufu hadi pale atakapotokea mtu jasiri akaandika ukweli. Wako watu bado wa hai na pengine wapo hapa ukumbini wanaijua historia ya mapinduzi ya Zanzibar kwa kuyaona mapinduzi yenyewe na kwa kushiriki lakini hawajanyanyua kalamu kuandika wala kufungua mdomo kuihadithia na watakwenda kaburini na watazikwa na historia zao ambazo laiti wangeliziandika nchi ingenufaika pakubwa.

Hashil Seif Hashil anastahili pongezi kwa ujasiri huu wa kutuandikia kitabu na kutueleza historia ya Zanzibar ambayo si wengi wanaijua khasa vijana waliozaliwa baada ya mapinduzi mwaka wa 1964 ambao kwa sasa ni watu wazima. Kuiandika historia ya mapinduzi ya Zanzibar ni kazi inayohitaji, ushujaa kwani si rahisi kuieleza na ukakosa kuwaudhi baadhi ya watu na wengine watu wako wa karibu sana. Afrika tuna utamaduni wa kuzifanya historia zetu kuwa kitu nyeti kwa hiyo iogopwe na isiguswe kwa kuigeuzageuza kutaka kujua undani wake. Hashil Seif ni mwandishi jasiri na mtu huwezi kustaajabu kwa huu ujasiri wake utakapoijua historia yake binafsi. Hashir Seif mwaka wa 1962 akiwa kijna mdogo kabisa wa umri wa miaka 26 alitoroka Zanzibar pamoja na wenzake wapatao 20 kwenda Cuba kupata mafunzo ya vita kwa nia ya kurejea Zanzibar na kupindua serikali na kuweka utawala wa Ki-Marxist. Hili la kwanza na kaeleza katika kumbukumbu hizi.

Pili, Hashir Seif hajasita hata mara moja katika kitabu hiki kueleza kuwa yeye alikuwa mwanachama wa ZNP, maarufu kwa jina la ‘’Hizbu.’’ Katika historia ya Zanzibar baada ya mapinduzi neno, ‘’Hizbu,’’ lilikuwa linatisha na kuna watu na si wadogo hadi leo bado wana hofu kubwa ya kunasibishwa na historia yao katika Hizbu. Katika kumbukumbu hizi Hashil Seif anaeleza historia yake ndani ya chama hiki na mchango wake kama kijana katika Youth Own Union (YOU) bila hofu wala wasiwasi wowote na hadi leo katika umri mkubwa wa miaka 80 bado ni komredi na hajabadili fikra zake za siasa za mrengo wa kushoto. Katika kitabu hiki Hashil Seif anaeleza fikra zake kama bado yuko katika Zanzibar ya miaka ya 1960 bila ya kuongeza wala kupunguza nukta. Hii ni moja ya mambo yanayokifanya kitabu hiki kiwe kiongozi katika kuijua historia ya mapinduzi na wanasiasa wake wa nyakati zile.

Ili kitabu kiwe kitabu ni lazima kiwe kina elimu mpya ambayo kabla haikuwa inajulikana. Wazanzibari wengi, ukimtoa Dr. Harith Ghassany: ‘’Kwaheri Ukoloni Kwaheri Uhuru,’’ (2010), walioandika historia ya mapinduzi wote wamepita mle mle katika historia rasmi. Msomaji hapati jipya isipokuwa tofauti ya jalada, jina la kitabu na la mwandishi. Unapoanza kumsoma Hashil Seif mwanzoni tu unakuwa mfano wa mtu aliyekuwa kalala usingizi fofofo na ghafla anatokea mtu akammwagia maji baridi usoni na kwa maji yale akashtuka kutoka usingizini na pengine kwenye ndoto akawa karejea katika dunia ya kweli. Hashil Seif anakifungua kitabu kwa majina ambayo hutayakuta katika historia tuliyoizoea ya mapinduzi ya Zanzibar. Hashil Seif katika kitabu hiki kataja majina ambayo yalifutika katika historia ya Zanzibar na kama utayakuta basi yatakuwa yemetajwa, ‘’in passing,’’ kama Waingereza wasemavyo, yaani majina hayo yatakuwa yametajwa kijuujuu. Nitatoa mfano kwa uchache.

Hashil anawataja mara kadhaa katika kitabu Abdulrahman Babu, Khamisi Abdallah Ameir, Ali Sultan Issa na Badawi Qullatein katika siasa za kupigania uhuru wa Zanzibar. Ahmed Rajab mmoja wa makomredi, ambae kaupitia mswada wa kitabu hiki ameniandikia na kunifahamisha kuwa Khamis Abdallah Ameir kama ‘’Theoretician,’’ sifa hii hutaisoma katika kitabu lakini katika mawasiliano yangu na Ahmed Rajab hili kanieleza na akasema kuwa Khamis Abdallah Ameir hakuwa mwanachama wa kawaida katika harakati zile. Hili lilidhihirika baada ya mapinduzi kwa Khamis Abdallah Ameir kuwa memba wa Baraza la Kwanza la Mapinduzi. Khamis Abdallah Ameir sikupatapo kumsikia kabla mpaka nilipomuona hapa katika ukumbi huu katika muhadhara wa Abdallah Kassim Hanga na sasa kaletwa tena na Hashil Seif. Babu, Ali Sultan na Badawi Qullatein hawahitaji maelezo. Bahati mbaya sana kuwa kitabu hakikuwekwa faharasha yaani ‘’index,’’ lakini laiti ingekuwapo faharasha msomaji angeweza kuona umihumu wa wazalendo hawa waliotajwa katika kitabu hiki kwa kuangalia ni mara ngapi majina yao yametajwa katika historia hii.

Huu ni mfano mmoja tu katika majina mengi ambayo hayajatajwa katika historia ya Zanzibar lakini Hashil Seif ameyarejesha na kueleza historia za watu hao katika kupigania uhuru wa Zanzibar. Msomaji atamsoma Ali Sultan Issa aliyekuwa Mkomunisti ndani ya ZNP, Badawi Qulattein, Salim Rashid aliyekuwa katibu wa kwanza wa Baraza la Mapinduzi. Wazalendo hawa historia zao zina mvuto wa pekee kabla na baada ya mapinduzi. Ali Sultan ndiye aliyetengezeza mpango mzima wa kuwapeleka vijana wa ZNP, Cuba kwa mafunzo ya kijeshi kujitayarisha kwa mapinduzi. Haya ndiyo msomaji atakutananayo katika kitabu hiki na ikiwa ni hivi ndivyo hali ilivyokuwa wakati wa kupigani uhuru wa Zanzibar haiwi tabu kuelewa sifa za makomredi katika uongozi na mchango wao katika mapinduzi.

Hashil Seif ameifanyia hisani kubwa sana historia ya Zanzibar kwa kueleza uongozi wa Abdulrahmani Babu katika kupigania uhuru wa Zanzibar na katika kuweka msingi wa mapinduzi. Hashil Seif anasema Babu alimuathir zaidi katika maisha yake ya kutafuta kuleta mabadiliko visiwani na akamaliza kwa kusema kuwa hapajatokea kiongozi Zanzibar ambae anaweza akalinganishwa na uwezo aliokuwanao Babu. Hashil anamsifia Babu kw akusema kuwa ‘’bongo,’’ lake halikuwa la kawaida. Nilipokianza kukisoma kitabu hiki hata kabla sijafika mbali ikawa imeshanidhihirikia kuwa mikononi mwangu nimeshika kitabu kinachofungua mengi katika historia ya mapinduzi ya Zanzibar na kwa ile harara yangu sikuweza kustahamili mara moja niliandika patio fupi kwa kile nilichokisoma na kukiweka katika mtandao na nikawaahidi wasomaji wangu In Shaa Allah nitarejea nitakapokimaliza kitabu. Huenda ni hili patio langu ndilo lililosababisha hii leo mimi kuwa hapa mbele yenu kwani haikuchukua muda baada ya kukiweka kitabu mtandaoni ikawa ghafla kitabu kikafahamika, kikapata umaarufu na kikawa kinaulizwa; na kama kawaida linapokuja suala la Zanzibar malumbano yakaanza na mjadala ukawa unakwenda kwa kasi lakini bila ya wanaojadiliana kuwa wamekisoma kitabu. Wengi walibakia na zile zile rejea zao za kale ambazo zingine ni shida kutambua ipi ni ‘’fact,’’ na ipi, ni ‘’fictio,’’ yaani upi ukweli na upi uongo.

Moto ukawaka. Katikati ya mjadala nikaletewa mtandaoni picha ya Hashil Seif na wenzake wawili, Amour Dugheshi na Mussa Maisara wamebeba bunduki. Yawezekana kwa baadhi picha hii ilinogesha kumbukumbu za mapinduzi na mchango wa makomredi na jinsi Hashil Seif na Amour Dugheshi walivyomshughulikia Field Marshall John Okello na kumfurusha visiwani. Haukupita muda nikaletewa picha nyingine akiwamo Khamis Abdallah Ameir, Badawi Qullatein na Hashil Seif. Kwangu mimi hizi picha zikaongeza mengi katika kukielewa kitabu cha Hashil Seif na nafasi ya Umma Party katika historia ya mapinduzi kwani picha husema maneno elfu.

Nilipoangalia picha ya Hashil Seif amebeba silaha na kusoma kuhusu mafunzo ambayo vijana wa Umma Party waliyapata Cuba wakati wa kupigania uhuru nilielewa kwa nini siku za mwanzoni za mapinduzi hawa vijana ndiyo walikuwa walinzi wa mapinduzi na wangejenga uti wa mgongo wa Jeshi la Zanzibar ingekuwa hapangekuwa na muungano na Tanganyika. Hashil Seif ameeleza toka mwanzo nia ya makomredi kupindua serikali yoyote Zanzibar isiyokuwa yao na kuweka utawala utakaofuata siasa za ki-Marxist. Haiwezekani kuwa na serikali kama hii bila ya jeshi madhubuti. Sijui kwa nini Hashil Seif katika kitabu kizima hili hakugusia ingawa kaeleza mengi juu ya masikitiko yake kwa kuona mapinduzi hayakwenda kama walivyotegemea ingawa kaeleza kuwa laiti ushauri wa Babu kwa viongozi wenzake katika ZNP ungelifuatwa, basi mapinduzi yasingelitokea. Hashil Seif ameeleza mgongano uliokuwapo ndani ya ZNP kati ya Babu na Ali Muhsin uliopelekea Babu kujitoa ZNP na kuunda Umma Party. Hashil katika sintofahamu hii anaeleza kile anachokiita njama baina ya Waingereza na viongozi wahafidhina ndani ya ZNP kumfunga Babu jela kitu ambacho walifanikiwa. Hashil Seif anaeleza karoti aliyowekewa farasi mdomoni kummaliza Babu. Hakika katika simulizi hii Hashil Seif kaeleza mengi ya kufikirisha. Hashil katika kurasa za mwisho wa kitabu kwa masikitiko kasema kuwa mapinduzi yaliyofanyika Zanzibar si mapinduzi ambayo Umma Party walikuwa wakiyafikiria na walijitayarisha kwa hilo, wala si mapinduzi ambayo Abdallah Kassim Hanga wa ASP alitaka yatokee.

Nahitimisha kwa kusema kuwa hili somo la mapinduzi kama alivyoeleza Hashil Seif bila shaka litawastaajabisha wasomaji na wanafunzi wa historia ya mapinduzi ya Zanzibar kwani mapinduzi yalifanyika na ASP wamesema kuwa ni wao ndiyo waliopindua na kuja na kauli mbiu ya, ‘’Mapinduzi Daima.’’ Wengi bila shaka wataguswa na maelezo ya Hashil Seif na vijana wenzake wa Umma Party kwa kazi waliyofanya ya kukamilisha mapinduzi kwa kuzuia umwagaji damu uliokuwa si wa lazima baada ya serikali kuanguka na jinsi walivyorejesha nidhamu kwa wale wanamapinduzi waliokuwa na mapanga mikononi. Wapo wanaoamini kuwa bila ya uongozi wa Umma Party na watu kama Badawi Qulatein na vijana kama Hashil Seif Hashil damu nyingi zaidi ingelimwagika na Mji Mkongwe pengine ungechomwa moto.

Mohamed Said

1 March, 2019.
 
1551554575000.png

Kushoto Badawo Qullatein, Hashir Seif aliyekaa na
Khamis Abdallah Ameir

1 March, 2019.[/QUOTE]
 
Leo tarehe 12 January ni Sikukuu ya Mapinduzi ya Zanzibar, nachukua nafasi hii kuwatakia nyote heri na fanaka za Mapinduzi na kukutakieni maadhimisho mema ya sherehe ya kumbukumbu ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar kwa watakao shereheka kwa wale wenye kumbukumbu njema, na kwa vile Mapinduzi Matukufu yale pia yaliandamana na umwagaji damu, natoa pole kwa wenye kumbukumbu chungu.
P
 
View attachment 1036339

Katika tembea tembea zangu JF ni ajabu huu uzi sijapatapo kuuona kabla, kwanza umenivutia kuwa na vitu vipya katika historia ya mapinduzi halafu AlhamduliLlah nimebahatika kuwafahamu, katika uhai wao, Badawi Qullatain, Abdulrahman Babu, Kanal Mahafuz na "Tony", kati ya hao makomred. Allah awarehem waliotutangulia aturehem na sisi tunaowafatia.

In shaa Allah ntakitafuta kitabu.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom