Pitia Hizi Hadithi, Leo Unaweza Badilisha Mtazamo wako wa Fikra na Maisha pia

Nyamsusa JB

JF-Expert Member
Jul 9, 2015
568
1,562
Habarini wanajanvi.
Poleni na majukumu ya kila siku.

Leo ningependa kukushirikisha katika hizi Inspiration Story ambazo zimenisaidia sana katika kunijenga na kunihamasisha kwenda mbele na pia kuniongezea Uvumilivu.
Ni Story ambazo zimekuwepo kwa Karne nyingi zikifurahisha lakini zikiwa na ujumbe Mzito ndani yake, ukizipitia naamini Utaburudika lakini mwisho wa siku utapata ujumbe wakati ukiendelea kupambana na Maisha ya kila siku. Karibuni

1. Thamani Yako

Kuna Mhamasishaji moja maarufu aliianza Hotuba yake kwa kutoa Noti ya Dola 20 mbele ya Umati wa watu wapatao 200 waliokusanyika kumsikiliza. Akawauliza nani angependa apewe Noti ile?”

Mikono 200 ikanyooshwa.

Akasema nitampa hii noti ya dola 20 mmoja kati yenu lakini kwanza, ngoja nifanye hiki.” Akaikunjakunja vibaya ile noti.

Na akauliza tena,” Ni nani bado anaitaka?

Mikono yote 200 bado ilinyooshwa.

Akasema haina mbaya,” Vipi kama Nikiifanya hivi?” Akaitupa ile Noti chini na akaikanyaga na viatu vyake.

Akaichukua ile Noti, akaionyesha kwa Umati. Noti ilikua imejikunjakunja na kuchafuka sana.

“Nani bado anaitaka?”

Bado mikono yote ikanyooshwa juu.

Akawaambia Rafiki zangu leo nimewafundisha somo Muhimu sana. Haikujalisha niliifanya nini ile Pesa, uliendelea kuitaka kwa sababu thamani yake haikupungua, bado iliendelea kua na thamani ya $20.

Mara nyingi katika Maisha yetu, Maisha yanatupiga Yanatutaabisha na Uchafu mwingi, tunafanya maamuzi mabaya, tunajihisi hatuna thamani tena. Lakini nataka kusema Haijalishi nini Kimetokea au Kitatokea, Bado Hujapoteza Thamani kwani Wewe ni wa Kipekee – Usisahau Hili.


2. Misaada Inayodumaza

Mtu mmoja alipata kuona kipepeo mdogo akinga’ng’niza kujitoa katika yai.

Alikaa na kutazama kipepeo huyo kwa masaa kadhaa wakati akijitahidi kulazimisha mwili wake kupita upenyo mdogo katika yai.

Hadi alipoacha ghafla kufanya maendeleo yoyote na ilionekana kama Kipepeo huyo mdogo amekwama.

Kwa hivyo mtu huyo aliamua kumsaidia kipepeo huyo mchanga. Alitwaa mkasi na akachukua lile yai na kuliongezea upenyo . Kisha kipepeo iliibuka kwa urahisi, ingawa alikuwa na mwili wenye kuvimba na mabawa madogo, yaliyofungwa.

Mtu huyo hakufikiria kitu chochote na alikaa hapo akingoja mabawa ya Kipepeo Yule mchanga yapanuke ili kumsaidia kipepeo Yule mchanga. Lakini hiyo haikutokea. Kipepeo alitumia maisha yake yote kukosa kuruka, akitambaa pande zote na mabawa madogo na mwili wenye kuvimba.

Licha ya moyo huruma wa mtu huyo, hakuelewa kwamba upenyo mdogo wa yai la Kipepeo ni kizuizi kinachohitajika kwa kipepeo huyo mchanga, ili apambane ajilazimishe kupita na ilikuwa njia ya Mungu ya kulazimisha maji kutoka kwa mwili wa kipepeo na kwenda kwenye mabawa yake Ili yakue na kujitayarisha kwa kuruka mara tu akitoka nje ya yai lake..



Funzo la hadithi:

Mapambano yetu maishani huendeleza nguvu zetu. Bila mapambano, hatukui na kamwe hatutakua na nguvu, kwa hivyo ni muhimu kwetu kushughulikia changamoto peke yetu, na sio kutegemea msaada kwa kila jambo kutoka kwa wengine.



3. Vizuizi Katika Maisha Yetu ni Fursa

Katika nyakati za zamani, Mfalme aliweka mwamba wa jiwe barabarani. Kisha yeye akajificha na kutazama kuona kama kuna mtu atauondoa mwamba wa jiwe nje ya njia. Wauzaji na wafanyabiashara tajiri zaidi wa mfalme walikuja na kutembea karibu na mwamba huo lakini hakuondoa mwamba huo.

Watu wengi walimlaumu sana Mfalme kwa kutoondosha mwamba ule barabarani, lakini hakuna hata mmoja wao aliyefanya chochote juu ya kuliondoa jiwe lile.

Kisha mfanyabiashara mdogo akaja akiwa amebeba mzigo wa mboga. Alipokaribia mwamba, huyo mkulima aliweka mzigo wake na kujaribu kusukuma jiwe na kuliondosha barabarani. Baada ya kusukuma na kujitahidi sana, hatimaye alifanikiwa.

Baada ya kurudi nyuma kuchukua mboga zake, akaona begi likiwa barabarani mahali palipokuwa na mwamba.

Begi hilo lilikuwa na sarafu nyingi za dhahabu na barua kutoka kwa Mfalme akielezea kwamba dhahabu hiyo ilikuwa ya mtu ambaye ameondoa mwambai huo barabarani.



Funzo la hadithi:
Kila kizuizi kinachokuja maishani kinatupa fursa ya kuboresha hali zetu, na wakati wavivu wanalalamika, wengine wanaunda fursa kupitia mioyo yao ya fadhili, ukarimu, na utayari wa kufanya mambo.


Asanteni

Tutaendelea tena wakati mwingine Siku njema



 
Funzo la hadithi:
Kila kizuizi tunachokuja maishani kinatupa fursa ya kuboresha hali zetu, na wakati wavivu wanalalamika, wengine wanaunda fursa kupitia mioyo yao ya fadhili, ukarimu, na utayari wa kufanya mambo.
Ahsante kwa ku_share nasi.
 
Ahsante kwa chakula ya akili.
Siku zote jitahidi kuwa mtu wa matumaini, ukiweza kaa mbali tena jitenge na wanaopenda kulalamika muda wote.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom