pitia hii jamani

Skyblue

Senior Member
Joined
Jan 3, 2014
Posts
196
Reaction score
55
Wazo kwanini serikali ingepitisha sheria kwa makampuni kuajiri bili kuweka kigezo cha uzoefu. Kwani wanatutesa sana. Uzoefu mtu umetoka chuo utaupatia wapi. Mfano mtu mwaka watatu yupo kitaa anatafuta kazi hafu wasema uzoefu auto wap? Serikali badilikeni. Kwahilo mnataka wenye kazi wapewe kaz na fresh acpate kazi. Inaumaaaaaa
 
Serikali yetu Tukufu ni Sikivu sana. Kuna watu wao wanapita pita humu. Nadhani watalishughulikia.
 
Acha ujinga ww na gpa yako ya kutilia maji afu huna confidence kwenye kujieleza ukiwa unadodosolewa,huna CV yenye kumshawish mwajir akupe ajira?acha kulalamika mbona wenzako wanapata na n fresh?jiuliz n wapi umejikwaa ndugu
 
Ajira za kuanzia serikalini (entry level positions) haziitaji uzoefu kama kigezo cha kuajiriwa.
Kwenye makampuni binafsi, sidhani kama wataielewa serikali ikitaka kuwawekea mashrti hayo sana sana najua makampuni binafsi yanabanwa kuhusu kuajiri wageni tu.
Tembelea sana mtandao wa sekretariet ya ajira serikalini wanatangaza nafasi za kazi nyingi tu za kuanzia ambazo haziitaji mtu kuwa na experience.
Aidha taasisi nyingine za serikali mfano pccb walitangaza nafasi kazi ambazo hazikuwa na kigezo cha experience.
Kwa hiyi kijana usikate tamaa endelea kutafuta kazi kwa bidiii Mungu atakujalia utapata
 
Hi. ukisema hivo unakosea mkuu, kwahiyo wenye gpa ndogo wafanyaje? wafe njaa? mi nadhani suala sio gpa, nchi zinazojali watu wao watu hawafiki hata vyuo wanaishia seconday na wana ajira nzuri, serikali yetu haina msimamo. kuna watu wengi sana ambao sio watanzania wanafanya kazi kwenye kampuni tena kampuni binafsi nyingi na wengi wakuja sio raia, unafkiri kwenye nchi zao watakupa ajira ww kwanza kabla ya mtu wao? hapana, nchi zote zinazojali zinahakikisha wazawa wanapewa ajira kabla ya expatriate. sisemi watu wa nje wasiajiriwe nchi hapana, ila sio kwa kiwango kikubwa km hapa nchi kwetu. vijana wanahangaika mtaani masikini wengine wakuja kaja na cheti cha uongo, experience ya uongo, ana kiji experience kdg akijua kazi kdg tu bac ataandika ana experience ya miaka 7 na anaajiriwa, wa kwetu humu humu wanahangaika. Ifike kipindi serikali iwe adilifu, huruma na kujali watu wao. serikali ingeweka sharia na zifuatwe vijana wapate ajira, hata kama ni mishahara kidogo lakini ni fresher basi sio mbaya sn japo laki 4 tu watu wajikimu hata hela ya kula, huko mtaani ni njaa tupu, labda haijakufika bado ndugu, sisi wote ni watanzania, umoja na upendo ndo utakaotupeleka mbele daima.
 
Habari yako. unaongea kwa masikitiko sana hadi huruma imenijaa, sina cha kukusaidia zaidi ya kukuombea Mungu upate ajira mapema ww na walio wengi mtaani, usichoke kuvumilia, ipo siku riziki utaipata. ushauri wangu ni kua jaribu kuomba hata sehemu ya kujitolea ili upate sehemu kufanya kazi kuliko kukaa bure, usijali kuhusu mshahara, jail kujua kazi kwanza, utaiona faida yake mbeleni. Mola akutangulie na sote kwa pamoja.
 
Naona mze umepigika sana kitaa pole sana..sasa wakati ni huu jikusanyeni watu kama wewe kumi na tano andaeni andiko lolote la kitafiti au la mradi wowote pelekeni kwenye grants funders.., usiulize ziko wapi tafuta au uliza hata kwa walio karibu..hakika utafanikiwa na epuka kukaa vijiwe vinavokatisha tamaa....ideas zenu ndo zitawatoa kuna mashirika mengi yanatafuta hela pa kupeleka inawezekana mkawa kundi lenu..all the best..
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…