Pitia hapa ushauri wako muhimu

Pitia hapa ushauri wako muhimu

love peace

Senior Member
Joined
Sep 10, 2013
Posts
130
Reaction score
37
Hope mko salama wakuu...

Mi nina mpenzi wangu tulikuwa tunapendana sana but kwa sasa nahisi hanifai na hii yote ni kutokana hiki.

Nilipanga chumba somewhere, but kabla sijamaliza mwezi nikapata kazi Morogoro, ikabidi chumba tutafute mtu aingie aturudishie kodi iliyobaki mi nkaja kazini nikiamini mpenzi wangu atafuatilia.

Nikamuunganisha na dalali wangu anayentafutia mtu wa kuingia pale mda kidogo wakampata mtu, kumbe yule mtu alitoa hela yote lakini mpenzi wangu akaniambia katoa elfu tisini na ishirini imebidi ampe dalali mi nkachukua sabini.

Mwezi umepita nikaja kuongea na dalali akasema yule mpangaj katoa hela yote laki na nusu, nikaongea na mpangaji akasema ndio katoa yote. Nikampigia simu mpenzi wangu anasema dalali alimshawishi afanye hivyo nimsamehe sana.

Kiukwel mpenzi wanug kupanga njama ya kunidhulum naona maajab nimechanganykiwa sana. Wakuu hivi huyu mwanaume atanifaa kweli au nimwache?
 
mkiliwa hela huwa mnakuwa wapole.... komaa nae tu lakini serengeti boys ndo walivyo
 
Hivi nyumba ya mtu una haki ya kumpangisha mwingine? Hii imekaaje?
 
Acha ubahili binti,sh ngapi hiyo ya kulialia na mpenzi wako?Wanawake wengine bwana!!bahili sana.
 
Yaani buku themanini tu ndio inakufanya uanzishe sredi...

Hebu acha umaskini bi mkubwa, mwenzako kama kaomba msamaha ni jukumu lako kusamehe au kutosamehe...
 
Hi sled imenfurahisha sana......ushauri wangu tafta mtu mzima viserengeti boy ckiz vinapenda majimama yanayohonga
 
Hyo c sbb ya kumuacha bt ungemwambia ukweli kuwa hilo jambo limekukasirisha sn na umuonyeshe kwa vitendo kabsa kua hukupendezewa na jambo hilo,hopeful atabadilika na ck nyingine hatorudi tena,usimuache hilo ni suala dogo sn ktk mahusiano.
 
hilo suala linazungumzika kaa muelewane kama bado mwapendana sidhani kama unaweza kuvunja mahusiano na mtu ambae una malengo nae kwa jambo kama hili. Kuna watu wamekutana na changamoto kubwa zaid ya hii lakin bado wako wote na upendo ndo umekolea
 
Pole sana najua inaumiza unapomwamini mtu halafu akakuangusha imani huwa inapotea kiasi fulan,hilo ni jambo linalozungumzika,funguka vile ulivyoumia na ambavyo hujapendezwa na hilo,kisha msamehe na maisha yaendelee,na kumbuka tu upendo wa kweli hauhesabu mabaya.
 
Acha ubahili binti,sh ngapi hiyo ya kulialia na mpenzi wako?Wanawake wengine bwana!!bahili sana.

cjaumia na hela hata kdog.but amewezaje kupangana na mtu kunifanyia hvyo.means anaweza hata kupanga kuniibia au hata kunidhulu ksa hela huko badae lyk kweny ndoa.
 
hilo suala linazungumzika kaa muelewane kama bado mwapendana sidhani kama unaweza kuvunja mahusiano na mtu ambae una malengo nae kwa jambo kama hili. Kuna watu wamekutana na changamoto kubwa zaid ya hii lakin bado wako wote na upendo ndo umekolea

hv mkuu unaweza kupanpga njama ya kumfanyia unyama mtu umpendae?kama kaweza kwa kdog how about kikubwa?
 
Yaani buku themanini tu ndio inakufanya uanzishe sredi...

Hebu acha umaskini bi mkubwa, mwenzako kama kaomba msamaha ni jukumu lako kusamehe au kutosamehe...

sina mawazo ya hela,but future life.
 
cjaumia na hela hata kdog.but amewezaje kupangana na mtu kunifanyia hvyo.means anaweza hata kupanga kuniibia au hata kunidhulu ksa hela huko badae lyk kweny ndoa.
Kawaida sana wanaume kuwapiga kazi madem/wake zao.
 
yee binandam amekosea na kma kakubali makosa msamehe hakuna alie kamilika hilo lisiwe la kutengana nae fikiria zaidi
 
Yaani buku themanini tu ndio inakufanya uanzishe sredi...

Hebu acha umaskini bi mkubwa, mwenzako kama kaomba msamaha ni jukumu lako kusamehe au kutosamehe...

Kwa wengine hii ni pesa ndefu sana mkuu...
 
Acha ubahili binti,sh ngapi hiyo ya kulialia na mpenzi wako?Wanawake wengine bwana!!bahili sana.

mwisho wa akili yako ndo mwanzo wa matatizo usimlaumu binafsi, Mtu akinichakachua najisikia vibaya sana bora nisijue.
 
Kwa wengine hii ni pesa ndefu sana mkuu...

Ishu hapa si hela ila ukweli na uaminifu; kwa maana mpaka hapo hakuna mkataba wa ndoa, sasa je, kwa tabia hii atafaa kuwa mwenza wa kudumu?

Mi naona sema naye, akikiri kosa na kuomba msamaha panga kipindi cha mpito usome tabia yake zaidi. Huenda sisi tuliosalia tukawa na matatizo zaidi ya hayo!
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom