Chrismoris
JF-Expert Member
- Oct 27, 2017
- 14,234
- 17,828
Habari ya jumapili mabibi na mabwana. Leo ni siku nyingine ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima.
Napenda kuchukua wasaa huu kuwashirikisha ujumbe wa leo kutoka katika maandiko matakatifu.
Katika masomo ya leo tunakumbushwa kuhusu kuishi maisha yenye uwiano. Uwiano huu tunauzungumzia katika suala zima la kuhakikisha matendo yetu yaendane na maneno tunayoyaongea.
Katika Injili tumepewa mfano wa makuhani ambao walikuwa wanawabebesha waamini wao mizigo mizito ambayo wao wenyewe hawawezi kuibeba. Hivyo basi Bwana Yesu anatuambia tujiepushe na maisha yaliyojaa unafki, tuache tabia ya kuwahubiria wenzetu mambo ambayo sisi wenyewe hatuwezi kuyatenda.
Tunapofanya jambo lolote tuhakikishe dhamira zetu ni safi na zinasadifu yale tunayoyaongea.
Kwa leo ni hayo, aksanteni sana.
Muwe na jumapili njema.