Pingamizi la CHADEMA juu ya Siyoi na uthibitisho kuwa Siyoi si Mtanzania

Ahhhh Mary Chatanda... Damu au dhambi ile ya mauaji Arusha itachana hadi chu...yako mwaka huu! pole sana mama!
 
Amezaliwa Thika,Kenya.Baba yake Mmeru wa Tanzania,mama yake sijui.Huyo Sumari alipomzaa Sioi alikuwa anafanya nini huko Kenya?EAC ilikuwa ina miaka miwili tangu ife,hivyo haukuwepo ubalozi wa TZ pale.
ANGALIZO:
EAC haikuwepo kisiasa ila ilikuwa haijafa rasmi.Mfilisi alikua hajaanza kazi.Uraia wa eac/commonwealth unalongaje wanasheria?CCM ni chama chenye macho mengi sana,haiwezekani kimteuwe mtu mwenye utata wa uraia!!
 
Mkuu wa mkoa anaitaka Uhamiaji impe taarifa za uraia wa mgombea wa CCM?

Nlifikiri Mkuu wa Mkoa anafanya kazi za serikali na si za kisiasa!

Anyway ngoja tukae kimya tuone.
Babu, Unataka kukaakimya wakati katiba inataka kuchakachuliwa...
 
Nilitamani sana tukishinde CCM hiki kwa kura uwanjani sasa huyu paka mweusi kwa jina la Sioi naye katokea wapi mbona anatuharibia mechi hivi, aggghhh!!!!!!!!!

Mambo mengine bana, mpaka kero; ina maana hata huyu Meneja Kampeni wa kukodi, hili li-rugaruga kwa upande wa CCM Lowassa naye hakulifahamu hilo mpaka wanamvuna baba wa watu mahela meeengi kupitia kwa 'Askofu wa Tanzanite' wakati CCM Orijino ilishasema kuwa huyo mtu hapan???????

Mwigulu Nchemba naye bana, huu si utapeli kweli huu kwa Mhe Lowassa mchana kweupe hivi hivi mpaka CHADEMA bao la kisigino hivi??????

Big up sana Vicent Nyerere na Makamanda wote mliokua mnasaidiana huko ila mturudishie japo NUSU VIINGILIO maana wengine bado tulikua bado tuko kwenye foleni huku nje ya uwanja hivo mechi hatujaona kitu mara tunasikia eti ni KO zile za ki-Mike Tysoni tu daahh!!.


Sio uungwana kumtukana mwenzio Paka mweusi.... Kwa kosa lipi alilokutendea yeye kama Sioi ? Watu wengine mnapendaga sana ban za kujitakia.
 
Hivi topic ni kuhusu Crashwise au uraia wa SIOI.....?....kama crashwise ni mchicha mwiba basi wewe mchicha

Mkuu achana nao hao wameshachanganyikiwa baada ya siri kuvuja. nyoka ukimumwagia mafuta ya taa anahangaika hadi anatamani kuvua gamba. hakika gamba litavuka.
Tuachane na hayo, mkuu leo tunahitaji maombi yako kwenye mechi ya leo. Hakikisha unatupa updates.
 
Mimi ni Crashwise (Mtu mwenye fikra chache kuzidi hata punje ya mchanga) ...kawaulize (wakina nani ww? mie ntakuja muuliza mwenza wako) Uhamiaji nimeupataje (sio kiswahili sahihi, waonyesha ww si mtanzania) barua zao siyo mimi.....yaani CCM (Chama Dume) Arumeru mmechanganyikiwa (Sio ww ? kwa nn uweke mapingamizi) na bado (na kweli na bado lazima mwaka huu nikufanye mchicha)

Kama kawaida yako habari zako sio zakuaminika humu JF , JITOE !


Unapobishana, ukishindwa kwa hoja anza kukosoa/kusahihisha "grammar" hehehehe! DM jibu hoja!
 
Huyu Afisa Uhamiaji naye haelewi jambo la kuwa siri. Kutoa ufafanunuzi wa kisheria kuhusu uraia, iweje siri. Matumizi mabaya ya 'classification'
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Kwa hili CDM msijisumbue kabisaaa! Maana nyie mmeshika mpini wenzenu wameshika makali.
Hawa CCM Mahakama ni yao na Tume ya uchaguzi ni yao'So mwisho wa siku hili pingamizi lita
tupiliwa ya mbali. So ni kheri mjikite kwenye kampeni kuliko kupoteza mda kwa swala hili....
Huu ni mtizamo wangu binafsi na si lazima kuufata. All the best makamanda.
 
Radhia Sweety,
Fikiria yaliyomkuta Siyoi ndio yangekuwa yamemkuta Kamanda Nassari unadhani Magamba nao wangemuacha hivi hivi? Hii ndio siasa bana. One mistake, one gool. Tayari Jimbo tumeshalichukua!

Haya HAYA MNADA UMEANZA HUO!!!!!!!!!!!!!!

JIMBO LA ARUMERU LINAUZWA, KURA 200, KURA 500, KURA 5000, KURA 15,000; TOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOOP

UPINZANI WAMECHUKUAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAAA
 
Hahaha kumbe Chadema wanaiogopa CCM dah sikutegemea kutoka kwa Chadema. Mambo ya pingamizi bora mshinde mkishindwa ina cost sana.
 
CHADEMA imemwekea pingamizi mgombea wa ccm Siyoi kwa madai kuwa si raia wa Tanzania.CHADEMA imenasa barua ya siri yenye Kumb no.AR/C/32/VOL1/85 ya Feb 29/2/2012,kutoka kwa Afisa mfawidhi wa uhamiaji mkoa wa Arusha kwenda kwa Mkuu wa mkoa wa Arusha,ikifafanua uraia wa Sioyi na katika ufafanuzi huo Ofisi ya uhamiaji inakiri kuwa kwa yeyote aliyezaliwa nje ya nchi,ukomo wa uraia wake ni pale anapofikisha miaka 18 na baada ya hapo anapaswa kuukana uraia wa nchi alipozaliwa na Sioi Sumari alizaliwa Kenya,na hakuwahi kuomba uraia wa Tanzania.

View attachment 48967
View attachment 48968
View attachment 48969
View attachment 48970


Nimekukubali mzee,
Uko makini sana kutupatia update. Arumeru ni kwetu ila wewe umeingia hadi mvunguni. - Ninda - NENDA kanywe soda bili kwangu.
 
Marehemu Jeremia Sumari[JERRY SOLOMON kwa wakati huo] baba yake Siyoi alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni iitwayo Shell Chemical Company of Eastern Africa nchini Kenya. Hakuwa ubalozini.

Kwenye red: What a disaster? Kama baba yake alikuwa anafanya kazi kwenye kampuni binafsi basi Sioi Mkenya! Hivi Sioi na wapambe wake hakushtukia hili mapema?
 
Hivi ukizaliwa kenya ina maana kuwa wewe ni raia wa kenya?
Au ukizaliwa Tanzania basi wewe ni raia wa Tanzania? Mbona Bashe kazaliwa Tanzania?
Uraia wa nchi hizi mbili hutokana na wazazi.
Sioi ili awe raia wa kenya, ni lazima mzazi wake mmoja awe amezaliwa kenya.
Punguzeni ngonjera dah!
 
Hili ni rahisi sana kwa siyoi kulitupilia mbali - kuonesha kuwa hakuzaliwa Kenya na b. kama alizaliwa Kenya aliukana uraia wa Kenya alipofikisha miaka 18.

na hizo passport mbili za kusafiria kazipataje wakati kenya na tanzania hawana uraia wa nchi mbili?
 
Hivi wewe ni Pro-Chadema au msemaji wa ofisi ya Uhamiaji Arusha? Wewe basi kifungu cha sheria kinacho thibitisha Sioyi sio raia wa Tanzania, weka na uthibitisho wa Siyoi ni raia wa Kenya..

Kweli huyu dogo kiboko kila mkipiga hesabu zenu kwenye box la kura atashinda kwa mbali sana, mmeamua kuja na mbinu za kitoto.

Kama Chadema mnakubalika Arumeru kwa nini mnaangaika hivyo mpaka mnatia huruma.

Vipi Safari hii? Umeshawaahidi ile zawadi yao ya siku zote?
Namaanisha safari hii utavua ngu na kutembea mtupu?
 
Hivi ukizaliwa kenya ina maana kuwa wewe ni raia wa kenya?
Au ukizaliwa Tanzania basi wewe ni raia wa Tanzania? Mbona Bashe kazaliwa Tanzania?
Uraia wa nchi hizi mbili hutokana na wazazi.
Sioi ili awe raia wa kenya, ni lazima mzazi wake mmoja awe amezaliwa kenya.
Punguzeni ngonjera dah!

Sheria za Kenya hazituhusu hata punje, sisi tunafuatilia sheria za nchi yetu ambazo zinamtaka mtu aliyezaliwa katika mazingira kama ya sioi kuomba uraia wa Tanzania anapofikisha umri wa miaka 18.
 
  • Thanks
Reactions: FJM
Back
Top Bottom