Pingamizi la CHADEMA juu ya Siyoi na uthibitisho kuwa Siyoi si Mtanzania

Sheria za Kenya hazituhusu hata punje, sisi tunafuatilia sheria za nchi yetu ambazo zinamtaka mtu aliyezaliwa katika mazingira kama ya sioi kuomba uraia wa Tanzania anapofikisha umri wa miaka 18.
Uraia wa tanzania hutokana na wazazi. Siyo tu kwamba umezaliwa Tanzania au kenya basi automatically wewe ni raia. Soma 1995 citizenship act ya Tanzania, pia usome katiba ya kenya.
Kwanini aombe wakati yeye siyo raia wa kenya?
Ndio maana ofisa uhamiaji amewaomba wadhibitishe uraia wa kenya ili hivyo vifungu viwe applied to Sioi.
Tuliza boli.... we got this!
 
Hivi ukizaliwa kenya ina maana kuwa wewe ni raia wa kenya?
Au ukizaliwa Tanzania basi wewe ni raia wa Tanzania? Mbona Bashe kazaliwa Tanzania?
Uraia wa nchi hizi mbili hutokana na wazazi.
Sioi ili awe raia wa kenya, ni lazima mzazi wake mmoja awe amezaliwa kenya.
Punguzeni ngonjera dah!

Hata wale maofisa wa balozi zetu nje ya nchi nao wakizaa watoto nje ya Tanzania nao wanakuwa sio raia wa Tanzania?

Kwanza nimegundua humu JF watu wengi sheria za uhamiaji zinawapiga chenga sana.

Sheria ya Uhamiaji namba 7 ya mwaka 1997, kuna uraia wa aina tatu, ambao ni wa kuzaliwa, kurithi na kuomba.

Sasa tujiulize Siyoi kazaliwa lini.
 
Wakuu,
Hii hapa chini ndio section ambayo inalalamikiwa kwamba Siyoi hajatimiza. Kwanza hii sections sio kwa ajili ya wale waliozaliwa nje ya nchi tu, badala yake ni kwa kila mtu ambaye ana uraia wa nchi nyingine. Inatakiwa akitimiza miaka 18 azingatie section hii. Huyo jamaa wa Uhamiaji ufafanuzi wake una walakini mkubwa.

Ili Siyao awe na matatizo hapa ni lazima Kenya iwe na uraia wa kuzaliwa. Yaani mtoto akizaliwa Kenya awe automatically anakuwa Mkenya (Kama ilivyo USA ambako ukizaliwa huko unakuwa automatically raia wa USA). Au awe na mmoja wa wazazi wake ambaye ni Mkenya kwahiyo awe anarithi huo uraia wa mzazi wake mmoja.

Kwa Siyoi hayo mambo yote mawili hayamhusu. Wazazi wake wote ni Watanzania na pia kule alikozaliwa hawana uraia wa kuzaliwa. Hivyo kuzaliwa kwake Kenya hakukumpa yeye uwezo wa kuwa raia wa Kenya kwa taratibu zozote zile za kisheria. Ni kama mtoto akizaliwa Tanzania na wazazi ambao sio Watanzania anakuwa sio Mtanzania. Kenya nao ni hivyo hivyo.

Uhamiaji huwa wanawashauri Watanzania waliozaliwa nje wajaze hizo forms za kuukana uraia wa nchi nyingine kama njia za kuwasaidia kwani kuna nchi nyingi ambazo mtu huwezi kujua una uraia wao au hapana. Ili kurahisisha ni vizuri ujaze hiyo form. Lakini sheria yetu iko wazi hapo, muhimu kwa Siyoi ni kuthibitisha hajawahi kuwa Mkenya kwa sheria yoyote ile ya Kenya.

Tafsiri ya sheria inatolewa na mahakama na kwa kuzingatia kifungu hiki sioni ni mahakama gani itasema Siyoi sio raia?

7. (1) Any person who, upon the attainment of the age of eighteen years, is a citizen of the United Republic or was a citizen of the former Republic of Tanganyika or of the former People's Republic of Zanzibar and also is or was a citizen of some country other than the United Republic or either the former Republic of Tanganyika or the former People's Republic of Zanzibar shall, subject to the provisions of subsection (8), be deemed to have ceased to be a citizen of the United Republic
upon the specified date unless he previously renounced his citizenship of that other country, taken tile oath of allegiance and, in the case of
a citizen by descent, made and registered the declaration prescribed by Parliament regarding his intention as to residence.
 
Swali la msing, je kipindi anazaliwa kenya je wazazi wake walikuwa wanafanya nini? maana kuna hicho kifungu cha "kama wazazi wapo na shughuli za kibalozi nchi husika..."
 
Sheria za Kenya hazituhusu hata punje, sisi tunafuatilia sheria za nchi yetu ambazo zinamtaka mtu aliyezaliwa katika mazingira kama ya sioi kuomba uraia wa Tanzania anapofikisha umri wa miaka 18.

Mwita Maranya,
Ni sheria ipi ya Tanzania (naomba kifungu) ambayo inamtaka mtu aliyezaliwa kama Siyoi kuomba uraia wa Tanzania inapofika miaka 18?

Sheria ya uraia ni hii hapa chini:
http://www.bunge.go.tz/Polis/PAMS/Docs/6-1995.pdf

Sheria yetu inatoa haki sawa kwa Watanzania walio zaliwa ndani ya nchi na wale wa nje ya nchi na wazazi Watanzania. Lakini kwasababu kuna nchi nyingi mtoto akizaliwa huko anapata uraia wa alikozaliwa ndio maana haja ya kuweka hicho kifungu cha kuukana uraia wa nchi nyingine.
 
Siku zote huwa nasema Crashwise ni mchicha mwiba mnanibishia, haya angalieni sasa !

Hao ndio wazee wa kujivua gamba, kama wanavyoshambulia humu ndivyo watavyoipiga tik tak issue ya uraia, hukuna linalowashinda hata kumfufua mtu wanaweza hawa majambazi.
 
Mmeshindwa kushindana kwa sera sasa mnaingia kwenye personal life?
Hii inanikumbusha ya 2010 ya Slaa kuiba mke wa mtu!!

Mkuu mifano yako always uwa haiko relevant,sijui ni ushabiki wa kitoto au uelewa mdogo au kutokua na elimu kabisa,hv kwa akili yako wewe,ni lipi hatari kwa taifa(si Tanzania tu bali taifa lolote duniani) kumpa uongozi mtu ambae uraia wake haueleweki kwa taifa husika au yule ambae uraia wake uko wazi ila hana mke na ana mchumba tu?jaribu kutumia kichwa kujenga hoja
 
Hili ni rahisi sana kwa siyoi kulitupilia mbali - kuonesha kuwa hakuzaliwa Kenya na b. kama alizaliwa Kenya aliukana uraia wa Kenya alipofikisha miaka 18.

a. Yeye mwenyewe kwenye fomu kaandika kazaliwa Thika-Kenya "ataonesha" vipi kuwa hakuzaliwa Kenya?
b. Kama alizaliwa Kenya na akaukana uraia wa kenya iko wapi "renunciation certificate" ambayo ofisi ya Uhamiaji hawana?
 
Hivi humu JF hakuna wanasheria wa kutufafanulia issue ya Siyoi? Mbona kila mtu ni kama mbumbumbu tu na tafsiri nyepesi nyepesi kama karatasi za choo?
 
Wakuu,
Hii hapa chini ndio section ambayo inalalamikiwa kwamba Siyoi hajatimiza. Kwanza hii sections sio kwa ajili ya wale waliozaliwa nje ya nchi tu, badala yake ni kwa kila mtu ambaye ana uraia wa nchi nyingine. Inatakiwa akitimiza miaka 18 azingatie section hii. Huyo jamaa wa Uhamiaji ufafanuzi wake una walakini mkubwa.

Ili Siyao awe na matatizo hapa ni lazima Kenya iwe na uraia wa kuzaliwa. Yaani mtoto akizaliwa Kenya awe automatically anakuwa Mkenya (Kama ilivyo USA ambako ukizaliwa huko unakuwa automatically raia wa USA). Au awe na mmoja wa wazazi wake ambaye ni Mkenya kwahiyo awe anarithi huo uraia wa mzazi wake mmoja.

Kwa Siyoi hayo mambo yote mawili hayamhusu. Wazazi wake wote ni Watanzania na pia kule alikozaliwa hawana uraia wa kuzaliwa. Hivyo kuzaliwa kwake Kenya hakukumpa yeye uwezo wa kuwa raia wa Kenya kwa taratibu zozote zile za kisheria. Ni kama mtoto akizaliwa Tanzania na wazazi ambao sio Watanzania anakuwa sio Mtanzania. Kenya nao ni hivyo hivyo.

Uhamiaji huwa wanawashauri Watanzania waliozaliwa nje wajaze hizo forms za kuukana uraia wa nchi nyingine kama njia za kuwasaidia kwani kuna nchi nyingi ambazo mtu huwezi kujua una uraia wao au hapana. Ili kurahisisha ni vizuri ujaze hiyo form. Lakini sheria yetu iko wazi hapo, muhimu kwa Siyoi ni kuthibitisha hajawahi kuwa Mkenya kwa sheria yoyote ile ya Kenya.

Tafsiri ya sheria inatolewa na mahakama na kwa kuzingatia kifungu hiki sioni ni mahakama gani itasema Siyoi sio raia?

7. (1) Any person who, upon the attainment of the age of eighteen years, is a citizen of the United Republic or was a citizen of the former Republic of Tanganyika or of the former People's Republic of Zanzibar and also is or was a citizen of some country other than the United Republic or either the former Republic of Tanganyika or the former People's Republic of Zanzibar shall, subject to the provisions of subsection (8), be deemed to have ceased to be a citizen of the United Republic
upon the specified date unless he previously renounced his citizenship of that other country, taken tile oath of allegiance and, in the case of
a citizen by descent, made and registered the declaration prescribed by Parliament regarding his intention as to residence.

Mkuu, tunashukuru kwa ufafanuzi wako murua, lakini kuna mapungufu katika bandiko lako ungeweka wazi hiyo sheria ya uhamiaji ni ya mwaka gani? Na kabla ya hiyo sheria Uhamiaji walikuwa wanatumia sheria gani.
 
Na vipi kama Mzazi/wazazi wake walienda huko kwa kazi za kibalozi?

Mkuu Saharavoice,
Kama ingekuwa hivyo unadhani Wanasheria wa CDM wangehangaika nae. Ukweli ni kwamba Marehemu Jeremia Solomon Sumari (Baba yake Sioi) wakati anamzaa Sioi alikuwa anafaya Kibarua kwenye kampuni iitwayo Shell Chemical Company of East Africa nchini Kenya. Kwa mazingira hayo Sioi alipofikisha miaka 18 alitakiwa aukane uraia wa KENYA, lakini yeye hakuwai kufanya hivyo.
 
Nashindwa kuisoma hiyo nyaraka kwa kuwa natumia kamchina kangu.
Kama katika pingamizi lao, CDM watadai Sioi ni raia wa Kenya basi waandike maumivu wani itabidi waaambatanishe vielelezo ili kuthibitisha hilo, ieleweke kuwa ni jukumu la mlalamikaji kuthibitisha.
Ilitosha sana kuwasilisha wasiwasi wao juu ya uraia wa mlalamikiwa kutokana na mazingira ya kuzaliwa kwake hapo angelazimika kuleta vielelezo vinavyomthibitisha kuwa ni raia
 
Hakuna kitu hapo, zaidi yakupoteza muda wote. Yote haya kamati kuu ya CCM ilipelekewa na kuona hayana athari. Na mwenyekiti wa kamati kuu ni RAIS WA NCHI. Na hizi barua kabla ya kamati kuu kukaa zilipitiwa na usalama wa Taifa na Uhamiaji na ndipo wakamshauri Rais kuwa hoja hazina msingi. Hii ni wazi kabisa SIOI NI TISHIO ARUMERU, CDM WANA WEWESEKA KILA UPANDE

Ni ujinga ku quote barua ndefu kama ile aliyotoa muanzisha thread
 
CDM kama Barca unalinda goli huku unatuma mashambulizi mbele na nyuma, wakishangaa tu unatupa kitu nyavuni, Jamaa nasikia wanamwaga sumu mbaya huko, magamba wanaangaka wamkabe yupi wamuache yupi
 
Wakuu,
Hii hapa chini ndio section ambayo inalalamikiwa kwamba Siyoi hajatimiza. Kwanza hii sections sio kwa ajili ya wale waliozaliwa nje ya nchi tu, badala yake ni kwa kila mtu ambaye ana uraia wa nchi nyingine. Inatakiwa akitimiza miaka 18 azingatie section hii. Huyo jamaa wa Uhamiaji ufafanuzi wake una walakini mkubwa.

Ili Siyao awe na matatizo hapa ni lazima Kenya iwe na uraia wa kuzaliwa. Yaani mtoto akizaliwa Kenya awe automatically anakuwa Mkenya (Kama ilivyo USA ambako ukizaliwa huko unakuwa automatically raia wa USA). Au awe na mmoja wa wazazi wake ambaye ni Mkenya kwahiyo awe anarithi huo uraia wa mzazi wake mmoja.

Kwa Siyoi hayo mambo yote mawili hayamhusu. Wazazi wake wote ni Watanzania na pia kule alikozaliwa hawana uraia wa kuzaliwa. Hivyo kuzaliwa kwake Kenya hakukumpa yeye uwezo wa kuwa raia wa Kenya kwa taratibu zozote zile za kisheria. Ni kama mtoto akizaliwa Tanzania na wazazi ambao sio Watanzania anakuwa sio Mtanzania. Kenya nao ni hivyo hivyo.

Uhamiaji huwa wanawashauri Watanzania waliozaliwa nje wajaze hizo forms za kuukana uraia wa nchi nyingine kama njia za kuwasaidia kwani kuna nchi nyingi ambazo mtu huwezi kujua una uraia wao au hapana. Ili kurahisisha ni vizuri ujaze hiyo form. Lakini sheria yetu iko wazi hapo, muhimu kwa Siyoi ni kuthibitisha hajawahi kuwa Mkenya kwa sheria yoyote ile ya Kenya.

Tafsiri ya sheria inatolewa na mahakama na kwa kuzingatia kifungu hiki sioni ni mahakama gani itasema Siyoi sio raia?

7. (1) Any person who, upon the attainment of the age of eighteen years, is a citizen of the United Republic or was a citizen of the former Republic of Tanganyika or of the former People's Republic of Zanzibar and also is or was a citizen of some country other than the United Republic or either the former Republic of Tanganyika or the former People's Republic of Zanzibar shall, subject to the provisions of subsection (8), be deemed to have ceased to be a citizen of the United Republic
upon the specified date unless he previously renounced his citizenship of that other country, taken tile oath of allegiance and, in the case of
a citizen by descent, made and registered the declaration prescribed by Parliament regarding his intention as to residence.
You said it all Broda..... unless kama mmoja wa wazazi wake ni Mkenya
 
Hivi ukizaliwa kenya ina maana kuwa wewe ni raia wa kenya?
Au ukizaliwa Tanzania basi wewe ni raia wa Tanzania? Mbona Bashe kazaliwa Tanzania?
Uraia wa nchi hizi mbili hutokana na wazazi.
Sioi ili awe raia wa kenya, ni lazima mzazi wake mmoja awe amezaliwa kenya.
Punguzeni ngonjera dah!

Uraia uko wa aina mbili:

1. Wa kuzaliwa: ambapo kama umezaliwa Tanzania, bila kujali uraia wa wazazi wako, unakuwa raia wa TZ hadi hapo utakapofikisha umri wa miaka 18 na kuamua kuukana uraia wa nchi uliyozaliwa.

2. Uraia wa kupewa kwa mujibu wa katiba ya nchi. Hapa kuna kigezo cha mtu kuwa ameishi Tz kwa miaka kadhaa na ameomba uraia na kutimiza masharti ya kikatiba na sheria.

Kwa Sioi kama hakuukana uraia wa nchi alikozaliwa (ndivyo ilivyothibitishwa na uhamiaji) ina maana bado ni raia wa nchi husika. Tukumbuke kuwa sheria za Tanzania haziruhusu uraia wa nchi mbili.
 
Mkuu siokweli usemacho
1. Inamaana mume na mke wa kimarekani wakija bongo na kujifungua mtoto atakuwa raia wa kuzalia? HAPANA
2. Unamueleko wa kuwa sahihi lakini inahitaji ufafanuzi
Nimekundua watu wengu hawajui DUAL CITIZENSHIP inakuwaje
 
Mkuu, tunashukuru kwa ufafanuzi wako murua, lakini kuna mapungufu katika bandiko lako ungeweka wazi hiyo sheria ya uhamiaji ni ya mwaka gani? Na kabla ya hiyo sheria Uhamiaji walikuwa wanatumia sheria gani.

Ritz,

Hiyo ni citizen act ya mwaka 1995 ambayo ndio inatumika mpaka sasa kwa Tanzania. Sheria zote zilizokuwa zinatumika kabla ya hapo zimezingatiwa kwenye hii sheria ya uraia ya 1995.

Kinachochanganya watu ni hizi guidelines ambazo idara za serikali hutoa kama njia ya kutafsiri sheria. Kuna jamaa yangu wa Uhamiaji aliwahi kuniambia kwamba Watanzania wengi hawaelewi sheria ya uhamiaji. Sehemu kubwa hawaelewi kwamba kule walikozaliwa au wazazi wao walikokaa wanaweza kujikuta ni raia bila kujijua. Ili kuwasaidia, alisema, tunawaambia yeyote aliyezaliwa nje ya nchi aukane uraia wa nchi kule alikozaliwa. Hii ni tahadhari, kama ulikuwa raia basi unakuwa umejilinda. kama hukuwa raia linakuwa halijaharibika neno. Hizo ni guideliness sio sheria. Sheria ni hiyo hiyo ambayo iko kwenye citizen act ya 1995.

Ikienda mahakamani hawaangalii tena guidelines bali act yenyewe.
 
Back
Top Bottom