PINDA - Nitatoa Maamuzi yote Jumatatu

GHOST RYDER

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
1,025
475
Muda Mfupi uliopita Waziri Mkuu Mheshimiwa Mizengo Pinda kamaliza mazungumzo na Waandihi wa Habari wa Vyombo mbalimbali na kusisitiza kuwa Taarifa kamili kuhusu Mawaziri wanaodaiwa kujiuzuru atazitoa rasmi Jumatatu atakapokuwa akiahirisha kikao cha Bunge.

Maswali ni mengi kwa kila nayeisikia kauli hii:

  1. Nini kimejitokeza hapa
  2. Kuna aliyezuia maamuzi haya yasipate baraka?
  3. PM kashikwa na kigugumizi gani?
  4. Mbona kila jambo katika kiako cha jana yalishafahamika mpaka maazimio?
  5. Kikao cha leo kilikuwa na Agenda gani?
  6. Ni kweli anasubiri baraka za Rais?
  7. Ilikuwa sanaa?
  8. Au ni mchezo gani unataka kufanyika hapa?
  9. Kwanini Spika kaahirisha Bunge bila kuusoma Muongozo uliohusu ufafanuzi wa Serikali juu ya suala hili?
  10. Kwanini wameiacha nchi katika sintofahamu kiasi hiki?

Ahadi yake ni Jumatatu

Tunaendelea kusubiri


ADIOS


Akihojiwa na waandishi wa habari amedai kwamba hajapokea barua toka kwa waziri yeyote
 
Hapa wanangoja nini badala ya kutoa maamuzi?
Huyu jamaa hana meno wacha wamtoe tu kazidi ukilaza
 
Ulitegemea Pinda huyu atoe maamuzi yoyote? Pinda kwa kawaida huwa ni speaker ya JK. Hivyo anasubiri JK azungumze kupitia mdomoni mwake hiyo Jumatatu.
 
JK kaumbuka maana anamsubili Rose Migiro,waziri mkuu wa Tanzania hana meno ndiyo maana JK alimpa anjua hana maamuzi yeye ni mwoga
 
Lowasa alishasema serikali ya ccm ni legelege haiwezi kufanya maamuzi magumu anachosubiri mpaka jumatatu ni nini wakati kila kitu kiko wazi
 
hii nchi ndio maana iko nyuma siku zote.kufanya maamuzi ni swala gumu sana.
anyways!!waamue wasiamue kwa upande wa wananchi washaamua!
 
hata kama mimi ningekuwa Pinda ningeacha bora liende. Dharau za Kikwete ziko juu sana. Siamini mpaka leo kama rais anapenda kufanya kazi na Pinda.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom