Pinda ni zaidi ya Cleopa David Msuya

Wakati ule Waziri Mkuu wa zamani Msuya anasimamia kwa nguvu zake zote kuanzishwa kwa wilaya mpya ya Mwanga wengi tulimwona ni mkabila, mtu anayependelea kwao.

Waziri Mkuu wa sasa, Mizengo KP Pinda ni zaidi ya Msuya. Katika kipindi hiki kifupi tu cha uwaziri mkuu wake kaanzisha mkoa wake, KATAVI, kaanzisha na wilaya yake, MLELE, na anataka wilaya hii iwe na halmashauri mbili!

Yote haya kwa gharama ya kodi zetu WATANZANIA. Kuna wa kumzuia?

Na wewe anzisha yako.
 
sasa unashaanga nini? alinza msuya, kaja Sumaye na mkoa wake, sasa pinda si anaendelza tu utaratibu uliokuwepo
 
Mbona hamsemi juu ya mikoa mengine iliyoanzishwa wakati wake kama Njombe, Geita nk. Je huko nako ni kwake? Acheni majungu.Watu wengine kazi yao ni kulaumu tu. Na si ajabu wengi wenu mkipewa nafasi kama hizo matafanya mabaya kuliko hata hayo mnayopigia kelele. Kama ni lawama basi iwe kwa serikali yote, kwasababau maamuzi ya kuanzisha mikoa na wilya hayafanywi na mtu mmoja.
Njombe nayo ina wafadhili wake akina Anna Makinda na Philemon Luhanjo. Hiyo mingine imewekwa kama wasindikizaji ili WATANZANIA muone "haki" inatendeka au ionekane inatendeka! Hivi kweli kwa hali hii tuliomo ambako watoto wanasomea chini ya miti wewe unaongeza mikoa na wilaya? Kwa nini hasa!
 
Mtu kwao hata ningekuwa mie, tumuache ili akumbukwe kwa mengi si ajabu miaka 50 ijayo hatatoka mtu kipande hicho si mnapafahamu palivyo!
 
sasa unashaanga nini? alinza msuya, kaja Sumaye na mkoa wake, sasa pinda si anaendelza tu utaratibu uliokuwepo
Tusiwalaumu Wachagga, Wahaya, Wanyakyusa kwamba wao ndio wanaujua ukabila. Haya mambo yapo kwa makabila yote. Wengine ni nafasi tu hatujapata. Nimpongeze kidogo Mkapa. Alikuwa na kila sababu kuifanya MASASI kuwa mkoa. Ni moja kati ya wilaya kongwe sana nchi hii.
 
huyu jamaa kwa maoni yangu hana kabisa uwezo wa kuwa waziri mkuu! Sijawahi kuona waziri mkuu dhaifu kama pinda ktk historia ya nchi hii!
 
huyu jamaa kwa maoni yangu hana kabisa uwezo wa kuwa waziri mkuu! Sijawahi kuona waziri mkuu dhaifu kama pinda ktk historia ya nchi hii!

Wewe unaijuwa historia ya nchi hii au unajisemea tu?
 
Mhhh, katiba itamke pia kushtakiwa kwa waziri mkuu,, maana kwa jinsi Pinda alivyopindisha mambo sijui kama after 2015 atanusurika kushtakiwa. Yaani ni dhahiri upendeleo wa viongozi kwa maeneo wanayotoka umezidi nchi hii. Leo Bagamoyo ni kila kitu, kina Mrisho serikalini usiseme.. Uwanja wa Ndege wa kutisha upo katavi (kazi ya Pinda). Je, Nyerere (RIP) angekuwa na Kasumba hii, watu wa maeneo tofauti na Mara wangefika walipo leo (la hasha, labda kwa bunduki)? Leo hii Mara ingekuwa ndo kila kitu kinapatikana kwa hapa TZ. Ama hakika walikaa naye, wakacheza, kula, kuongea na kulala naye (kama wayahudi na Yesu) lakini hawakumuelewa (Julius K Nyerere). Na sasa wanatumia maneno, hotuba na ukaribu waliokuwa nao kwake kuhalalisha matendo waliyoyaficha wakati wakiwa naye. Katiba itawahukumu.
 
Unafikiri uwaziri mkuu unapewa tu? tazama mawaziri wakuu wote walianzia wapi halafu iga.
Nimuige yupi sasa kati ya hawa wote: Mwalimu, Rashid, Sokoine, Msuya, Salim, Malecela, Warioba, Sumaye, Lowasa na huyu Pinda?
 
waziri mkuu gani wa kariba ya pinda kimaamuzi amewahi tokea Tz?

Nyerere, maamuzi yake yote yalikuwa mabovu toka alipokuwa Waziri Mkuu mpaka alipokuwa Rais kwa miaka nenda rudi, hakuna la maana lolote aliloifanyia Tanzania zaidi ya kuiwacha masikini wa mwisho duniani. Kaweka rekodi ya Dunia kwa kuikuta nchi ilikuwa ikiwaa ya kwanza kwa kusafirisha mazaao ya kilimo katika Afrika mpaka kuifikisha kuwa omba-omba wa chakula.
 
Haoni AIBU wala SONI hata kidogo. Katiba ijayo ivunje mikoa na wilaya zote za sasa. Ugawaji wake usimamiwe na kuidhinishwa na BUNGE. Hizi gharama za kuiendesha serikali kubwa namna hii hazifai.

Walter Rodney aliandika kwenye How Europe Underdeveloped Africa,siko karibu na kitabu la ningetoa quotation kabisa,kuna paragraph anatoa mfano wa majimbo kwa nchi za Afrika,kwamba wanasiasa wanaongeza idadi ya majimbo na mikoa ili kupeana ulaji,akatoa mfano mbunge wa France anaweza kuwakilisha watu 100,000 lakini wa nchi kama Gambia anawakilisha watu 10,000,haya mambo ndo yameanza kuja kwetu Tanzania.

Sent from my BlackBerry 8520 using JamiiForums
 
WENZETU KENYA HAWANA MAMBO HAYA YA KIJINGA YA KUJENGA JENGA MIKOA NA KUPANUA WILAYA KIHOLELA. WAO HUJENGA MAJUMBA YA KISASA YANAYOPATIKANA NEY YRK NA KUJENGA MIUNDO MBINU BORA ITAKAYO VUTIA WATALII WENGI. viongozi wa tanzania hawana wivu wa maendeleo kabisaa. Kila kukicha wizi bungeni na katika halmashauri za wilaya. je tutafika? najiulizaga kila siku ni kiongozi gani hapa tanzania hafuati amri za shetani? yaliyo ya shetani viongozi wetu huyafanya kwa nidhamu sana na kwa bidii zote ila yale ya kumpendeza mungu hawayafanyi ipasavyo. Risco mond, rada, mabajeti hewa wizarani, mikataba ya madini, wizi bandarini, wizi tanesco,wizi ATCL,wizi tanzania bureau standard, haya yote ni ya kumpendeza shetani. sasa jiulize ni lini shule za kata zitapata maktaba za vitabu, lini zitapata laboratories, lini walimu wataajiliwa vijijini, huyaoni hata siku maana haya yanampendeza mungu.
 
Wakati ule Waziri Mkuu wa zamani Msuya anasimamia kwa nguvu zake zote kuanzishwa kwa wilaya mpya ya Mwanga wengi tulimwona ni mkabila, mtu anayependelea kwao.

Waziri Mkuu wa sasa, Mizengo KP Pinda ni zaidi ya Msuya. Katika kipindi hiki kifupi tu cha uwaziri mkuu wake kaanzisha mkoa wake, KATAVI, kaanzisha na wilaya yake, MLELE, na anataka wilaya hii iwe na halmashauri mbili!

Yote haya kwa gharama ya kodi zetu WATANZANIA. Kuna wa kumzuia?

Niliwahi kusema hapa pinda hafai kuwa waziri, angepewa ukuu wa wilaya sababu hata ukurugenzi hawezi anapenda siasa za kinafki na za kuogopa ogopa anawaitaga "wakubwa"
 
Back
Top Bottom