Pinda ni zaidi ya Cleopa David Msuya

WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,511
2,000
Wakati ule Waziri Mkuu wa zamani Msuya anasimamia kwa nguvu zake zote kuanzishwa kwa wilaya mpya ya Mwanga wengi tulimwona ni mkabila, mtu anayependelea kwao.

Waziri Mkuu wa sasa, Mizengo KP Pinda ni zaidi ya Msuya. Katika kipindi hiki kifupi tu cha uwaziri mkuu wake kaanzisha mkoa wake, KATAVI, kaanzisha na wilaya yake, MLELE, na anataka wilaya hii iwe na halmashauri mbili!

Yote haya kwa gharama ya kodi zetu WATANZANIA. Kuna wa kumzuia?
 
Mkwe21

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
2,265
2,000
WildCard

Hii ni aibu sana!! Ilifikia mahali nikatafakari nikaona huyu Mkuu tuliyenaye sijui tumwiteje? Kodi zetu kaenda kujenga Katavi, Huyu mkuu nadhan anafaa kuwa mkuu wa mkoa, na si mkoa mwingine ila wa nyumbani kwake!! Sasa kawa Kiranja mkuu wa nchi!!!!!
 
Last edited by a moderator:

Lupweko

JF-Expert Member
Mar 26, 2009
15,230
2,000
Na uwanja wa ndege, chuo kikuu cha kilimo na mengine mtayasikia kabla pazia halijafungwa 2015
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,511
2,000
Hii ni aibu sana!! Ilifikia mahali nikatafakari nikaona huyu Mkuu tuliyenaye sijui tumwiteje? Kodi zetu kaenda kujenga Katavi, Huyu mkuu nadhan anafaa kuwa mkuu wa mkoa, na si mkoa mwingine ila wa nyumbani kwake!! sasa kawa Karanja mkuu wa nchi!!!!!
Haoni AIBU wala SONI hata kidogo. Katiba ijayo ivunje mikoa na wilaya zote za sasa. Ugawaji wake usimamiwe na kuidhinishwa na BUNGE. Hizi gharama za kuiendesha serikali kubwa namna hii hazifai.
 
Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
3,548
1,225
Haoni AIBU wala SONI hata kidogo. Katiba ijayo ivunje mikoa na wilaya zote za sasa. Ugawaji wake usimamiwe na kuidhinishwa na BUNGE. Hizi gharama za kuiendesha serikali kubwa namna hii hazifai.

Kwani tatizo ni Katiba? Katiba ni karatasi tu, hata Katiba ya sasa hivi pia ina mambo mazuri tu na inakataza mambo mengi tu lakini kila siku yanavunjwavunjwa tu, kwa hiyo hata ile Katiba gani, maadamu watu ni wale wale hamna litakalobadilika!

Wile GAMBA

JF-Expert Member
Sep 13, 2011
1,809
0
wakati tunapanga Afrika kuungana watu wana gawa vijiwilaya ili kujipatia ulaji wakiona hawawezi kushinda ubunge, hii nchi iliisha laaniwa, upuuzi mtupu! mdogo watu wana kufa njaa watu wamekaa kufanya upuuzi.
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,511
2,000
Badala ya kumuunga mkono Maghufuli na Mwakyembe kujenga miundombinu mizuri na imara ili nchi ifikike kiurahisi wakati wote popote, wao wanaongeza gharama za kiutawala halafu wanazifanya kiukabila na nguvu za nafasi zao. Pinda hatuibii lakini maamuzi kama haya ni zaidi ya wizi.
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,511
2,000
Kwani tatizo ni Katiba? Katiba ni karatasi tu, hata Katiba ya sasa hivi pia ina mambo mazuri tu na inakataza mambo mengi tu lakini kila siku yanavunjwavunjwa tu, kwa hiyo hata ile Katiba gani, maadamu watu ni wale wale hamna litakalobadilika!

Sikumtarajia Pinda, mwanasheria wa siku nyingi, mtu aliyefanyakazi na Mwalimu kwa karibu, abadilike, afanye haya. Uliokuwa Mkoa wa Rukwa ulikuwa na ukubwa kiasi gani, ulikuwa na idadi gani ya watu. Hivi kweli shida ya mkoa ule ilikuwa ni kuongeza mkoa na wilaya nyingine?
 
FJM

JF-Expert Member
Apr 11, 2011
8,083
1,225
Waziri Mkuu wa sasa, Mizengo KP Pinda ni zaidi ya Msuya. Katika kipindi hiki kifupi tu cha uwaziri mkuu wake kaanzisha mkoa wake, KATAVI, kaanzisha na wilaya yake, MLELE, na anataka wilaya hii iwe na halmashauri mbili!

Yote haya kwa gharama ya kodi zetu WATANZANIA. Kuna wa kumzuia?

Waziri mkuu wa Katavi! Hivi huo si ndio ule mkoa wenye Wilaya mbili tu? Kweli, ukitaka kumjua mtu mpe cheo!
 
Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
8,810
2,000
Kwani pinda kaanzisha mkoa na wilaya kwake tu? Je?alitakiwa aanzishe kwengine lakini kwake asianzishe? Je?unadhani msuya kwa kuanzisha wilaya ya mwanga alikosea? Je?msuya alianzisha wilaya ya mwanga peke yake?hivi unafikiri pinda anasababu gani yakuanzisha mkoa wa mjini magharibi?
 
Matola

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
42,142

Pinda hana madaraka kwenye Jamhuri ya watu wa Zanzibar, madaraka yake yanaishia pale Ferry.
 
HUGO CHAVES

JF-Expert Member
Mar 25, 2011
2,045
1,500
historia itamhukumu vibaya mh.pinda ametumikia tamisemi kama waziri na sasa waziri mkuu .akiwa tamisemi amekuwa na maoni tofauti ili maendeleo yafike sehemu fulani tugawe ile wilaya ,au mkoa ,hulka hii amehamia nayo pamoja na kuwa ni waziri mkuu bado mgawanyo umekuwa wa kasi ,kule mwanza hatujasikia akitoa tamko kulaani tunamsikia akiunga mkono huku gharama za uendeshaji zikiwa juu ,wenzetu hufikiria uwezekano wa kuungano kuleta unafuu katika nchi zao ,huku tunagawa gawa viwilaya ,vimkoa ,kwa maslahi ya nani ,pamoja na kugawa kwa maslahi ya kisiasa hii ni dhambi maendeleo yanaweza kufika bila fulani ndio awe pale kama mkuu wa mkoa au wilaya .tunaona zambi hii inashika kasi zanzibar wanataka wawe huru tunajifunza nini hapa kwenye ofisi hii ya waziri mkuu .tuache kugawa wilaya au mikoa huduma na huduma zifike ,zsipofika tutamhoji kwa ni ni
 
aloycious

JF-Expert Member
Dec 17, 2012
5,980
2,000
Pamoja na mambo mengine wanarukwa tunalia mgawanyo usiosawa wa rasilimalia ardhi baina ya katavi na rukwa(mkoa mama).
Mkoa wa rukwa umegawanywa kupata katavi na utabaki na km za mraba 27,765 na wilaya 3,majimbo 4,tarafa 16,kata 64,vijiji 316,mitaa 196 na vitongoji 1658.
Katavi(mkoa mpya) una km za mraba 47,485 ikiwa na mara mbili ya rukwa,majombo 3,tarafa 10,kata 42,vijiji 124,mitaa 14 na vitongoji 671.
Ni dhahiri kuwa kuna upendeleo mkubwa wa rasilimali ardhi kwa mkoa wa katavi huku maeneo yote potentials na ya kimkakati wakichukua wao.
 
gfsonwin

JF-Expert Member
Apr 12, 2012
18,263
2,000
hivi kwanza ukubwa wa mkoa wa katavi ni mita za eneo kiasi gani??
na je wilaya anayoitaka iwena halmashuri mbili ina ukubwa gani??
atukipata jibu hapa ndipo tutakapo jua kama ni mwadilifu ama la. ila sala la kuwa na halmashuri mbili ni mzigo kwetu hilo twapaswa kulipinga kwa herufi kubwa. mbona hata wilaya ya kibaha vijijini ni kubwa sana ama ya bagamoyo mbona sijaona halmashauri mbili kwazo ama zinazo?
 
WildCard

JF-Expert Member
Apr 22, 2008
7,511
2,000
Kwani pinda kaanzisha mkoa na wilaya kwake tu? Je?alitakiwa aanzishe kwengine lakini kwake asianzishe? Je?unadhani msuya kwa kuanzisha wilaya ya mwanga alikosea? Je?msuya alianzisha wilaya ya mwanga peke yake?hivi unafikiri pinda anasababu gani yakuanzisha mkoa wa mjini magharibi?
Kwanini awe yeye Pinda na sio Lowasa au Sumaye( naye alianzisha Manyara!)? Hivi kweli unaposimamia eneo unakotoka lipate mkoa au wilaya utaelewekaje? Tanzania tunahitaji mikoa na wilaya nyingine kwa gharama ya nani?
 
Kijakazi

JF-Expert Member
Jun 26, 2007
3,548
1,225
Sikumtarajia Pinda, mwanasheria wa siku nyingi, mtu aliyefanyakazi na Mwalimu kwa karibu, abadilike, afanye haya. Uliokuwa Mkoa wa Rukwa ulikuwa na ukubwa kiasi gani, ulikuwa na idadi gani ya watu. Hivi kweli shida ya mkoa ule ilikuwa ni kuongeza mkoa na wilaya nyingine?

Tatizo sio Bw.Pinda au sijui Bw.Nyerere, tatizo ni jamii yetu jinsi ilivyo na jinsi inavyoangalia mambo, wewe unaweza kuwa umeona hilo ni tatizo lakini Watanzania wengi wasione tatizo liko wapi, na ndio maana wachangiaji kwenye hii mada ni wachache ikilinganishwa na kama ungeleta mada kama fulani kafumaniwa gesti, au Bw.Rizwani anunua Magomeni yote, kurasa zote zingejaa wachangiaji hasa kwenye mambo ya Ngono, lakini jambo kama hilo wengi humu hawaoni tatizo na wala haliwashtui, hivyo anayoyafanya Bw. Pinda au sijui Bw.Msuya yangefanywa na Mtanzania yoyote au Watanzania walio wengi pindi wangepata hiyo nafasi, hata Kardinali Pengo alilisema hilo, anayelia ufisadi katika jamii yetu ni kwamba hajapata hiyo nafasi, lakini akiipata atafanya yaleyale, alikuwa sahihi kabisa na hii ndio tafsiri yake!
 
Kaunga

JF-Expert Member
Nov 28, 2010
12,546
2,000
Labda mpewe Katavi NP maana, ukilinganisha Rukwa na Katavi, katavi ardhi yake kubwa ni protected land au general land iliyoko North of Mpanda boardering Kigoma na Refegee camps; ofcourse na East ambapo kuna N.Park. Rukwa mmejaa kila mahali, pop kubwa!

Pamoja na mambo mengine
wanarukwa tunalia mgawanyo usiosawa wa rasilimalia ardhi baina ya katavi na rukwa(mkoa mama).
Mkoa wa rukwa umegawanywa kupata katavi na utabaki na km za mraba 27,765 na wilaya 3,majimbo 4,tarafa 16,kata 64,vijiji 316,mitaa 196 na vitongoji 1658.
Katavi(mkoa mpya) una km za mraba 47,485 ikiwa na mara mbili ya rukwa,majombo 3,tarafa 10,kata 42,vijiji 124,mitaa 14 na vitongoji 671.
Ni dhahiri kuwa kuna upendeleo mkubwa wa rasilimali ardhi kwa mkoa wa katavi huku maeneo yote potentials na ya kimkakati wakichukua wao.
 
Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
8,810
2,000
Kwanini awe yeye Pinda na sio Lowasa au Sumaye( naye alianzisha Manyara!)? Hivi kweli unaposimamia eneo unakotoka lipate mkoa au wilaya utaelewekaje? Tanzania tunahitaji mikoa na wilaya nyingine kwa gharama ya nani?
kwa hiyo ulitaka kila waziri akiingia kazi iwe kuanzisha mikoa na wilaya tu.kwani wewe ulitaka tuwe na mikoa mingapi badala ya mingapi na kwa nini?
 
Hemed Maronda

Senior Member
Oct 27, 2010
138
0
Badala ya kumuunga mkono Maghufuli na Mwakyembe kujenga miundombinu mizuri na imara ili nchi ifikike kiurahisi wakati wote popote, wao wanaongeza gharama za kiutawala halafu wanazifanya kiukabila na nguvu za nafasi zao. Pinda hatuibii lakini maamuzi kama haya ni zaidi ya wizi.
Kuna maeneo mengi ya Kusini ya Tanzania na Nyanda za Juu Kusini waliacha nyuma kimaendeleo ni fedha hizo hizo alizotumia Sumaye kujenga uwanja wa ndege wa Arusha ili kuufanya uwe wa Kimataifa wakati kilometa chache upo uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro je huo usio wizi? Kama Mramba alikuwa andandua lami na kuweka lami mpya kwenye Mkoa wa Kilimanjaro wakati sehemu zingine kama Lindi na huko Kigoma na Rukwa hawana lami toka Nchi hii inapata uhuru je nao siyo wizi? Tufike mahali tukubali kuwa sehemu zingine zinatakiwa kupata maendeleo
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom