LINCOLINMTZA
JF-Expert Member
- Mar 15, 2011
- 1,639
- 516
Tatizo sio Bw.Pinda au sijui Bw.Nyerere, tatizo ni jamii yetu jinsi ilivyo na jinsi inavyoangalia mambo, wewe unaweza kuwa umeona hilo ni tatizo lakini Watanzania wengi wasione tatizo liko wapi, na ndio maana wachangiaji kwenye hii mada ni wachache ikilinganishwa na kama ungeleta mada kama fulani kafumaniwa gesti, au Bw.Rizwani anunua Magomeni yote, kurasa zote zingejaa wachangiaji hasa kwenye mambo ya Ngono, lakini jambo kama hilo wengi humu hawaoni tatizo na wala haliwashtui, hivyo anayoyafanya Bw. Pinda au sijui Bw.Msuya yangefanywa na Mtanzania yoyote au Watanzania walio wengi pindi wangepata hiyo nafasi, hata Kardinali Pengo alilisema hilo, anayelia ufisadi katika jamii yetu ni kwamba hajapata hiyo nafasi, lakini akiipata atafanya yaleyale, alikuwa sahihi kabisa na hii ndio tafsiri yake!
Kwa hiyo tuendelee na lao mpaka lini? Acha kupoteza matumaini mkubwa katika kutatua matatizo. Lazima matatizo tuyatatue bila kujali gharama zate au ukubwa wake.