Pinda ni mzigo katika serikali ya Kikwete | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Pinda ni mzigo katika serikali ya Kikwete

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Lukolo, Jul 27, 2011.

 1. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #1
  Jul 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ninaamini kwamba wengi wenu mtanipinga kwa kuwa mnamwona Pinda ni mpole, mwenye hekima na asiyependa kupayuka hovyo. Lakini kwa mtizamo wangu, baada ya nchi kuwa na Rais asiye mtendaji, tulipaswa kuwa angalau na waziri mkuu anayeziba mapungufu ya Rais. Lakini huyu waziri mkuu alivyo, ni bora hata ya Kikwete mwenyewe. Ni waziri mkuu asiye na maamuzi, kila jambo atajibu "nafikiri" (nafikiri kuna haja ya kupunguza matumizi serikalini - majibu yake haya) hana majibu na mamlaka ya kuagiza kama waziri mkuu. Hajitambui wala hajui kama yeye ndiye msimamizi mkuu wa mawaziri wote. Hana sauti wala hawezi kuwakemea mawaziri wake. Wakati tunalalamikia utendaji wa baadhi ya mawaziri wa Kikwete, ni vema pia tukasema ule ukweli kwamba huo utendaji mbovu wa mawaziri wengine unaanza na Pinda mwenyewe.

  Ukiangalia serikali zote zilizopita, kulikuwa angalau kuna mmojawapo kati ya Rais au waziri mkuu ambaye alikuwa na nguvu sana kumshinda mwenzake na alikuwa na uwezo mkubwa wa kufanya maamuzi ya haraka kwa niaba ya serikali. Sasa hawa tulionao hakuna mwenye unafuu kuliko mwenzie. Huyu ni waziri mkuu aliyeshindwa kusimamia project yoyote ya serikali. Ameanzisha Kilimo kwanza kwa gharama kubwa, akawaacha mawakala wanaiba pembejeo matokeo yake project imekufa bila kuleta mafanikio yoyote. Jana tumesikia wilaya 56 zina upungufu wa chakula. Hicho kilimo kwanza kimetusaidiaje? Kama JK anataka kufanya mabadiliko yoyote ya mawaziri, basi na waziri mkuu pia amuondoe. Huyu bwana ni mzigo mwingine kwa serikali.
   
 2. Ndibalema

  Ndibalema JF-Expert Member

  #2
  Jul 27, 2011
  Joined: Apr 26, 2008
  Messages: 10,916
  Likes Received: 132
  Trophy Points: 160
  Ndugu yangu kwa hali halisi ilivyo ktk Serikali nzima, Pinda hana budi kuwa kama alivyo sasa.
   
 3. Gobret

  Gobret JF-Expert Member

  #3
  Jul 27, 2011
  Joined: Jun 11, 2010
  Messages: 320
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Pinda anatofautiana sana na jina lake. Amepinda maana yake anachapa kazi kweli lkn ni tofauti kwa huyu Pinda. amezubaa sana. Lakini ni nafuu sana ukimlinganisha na *kwere. Hana maana ya kuwa rais wa nchi
   
 4. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #4
  Jul 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Ndibalema hebu tupe mauzoefu hapo. Hali gani inayosababisha Pinda awe hivyo alivyo? Yaani Pinda alivyo, ni nafuu hata ya Kawawa.
   
 5. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #5
  Jul 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  kwa kweli na mimi naona hivyo. Jamaa utendaji wake ni wa mashaka sana. Hata sioni maana ya yeye kuwa waziri mkuu.
   
 6. THINKINGBEING

  THINKINGBEING JF-Expert Member

  #6
  Jul 27, 2011
  Joined: Aug 9, 2010
  Messages: 2,726
  Likes Received: 854
  Trophy Points: 280
  Hapo hakuna ambaye ni mzigo kwa mwenzie.Hiyo ni mizigo miwili.
   
 7. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #7
  Jul 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Haha!! Nice comment! Kwa hiyo kila mmoja ni mzigo kwa mwenzie? ha ha ha haaa!!
   
 8. Mzalendo80

  Mzalendo80 JF-Expert Member

  #8
  Jul 27, 2011
  Joined: Oct 30, 2010
  Messages: 2,385
  Likes Received: 122
  Trophy Points: 160
  Si bora ya Pinda amekuwa Mzigo kwenye Serikali ya Fisadi papa Kikwete, Kuliko Huyu Fisadi Papa Kikwete amekuwa Mzigo kwa Watanzania. Unajua Ni kiasi gani kila akienda kuomba huko Ughaibuni analigharimu Taifa? Kikwete amekuwa ni Mzigo kwetu na anatafuna Kodi zetu bila ya huruma na hana Uzalendo la Hili Taifa
   
 9. P

  Paul S.S Verified User

  #9
  Jul 27, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu unajua ni kwanini Pinda alikuwa anakataa kuendelea na na nafasi hii kabla hajabembelezwa sana na kukubali?
   
 10. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #10
  Jul 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Hakuna ushahidi wowote kwamba Pinda alikataa kuendelea na hii nafasi. Wewe umetoa wapi hizo taarifa? Au unafanya kazi Ikulu?
   
 11. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #11
  Jul 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mkuu, si unajua kwamba Malecela alikataliwa na Nyerere kutokana na kushindwa kumshauri vizuri Mwinyi? Kwa hiyo ina maana waziri mkuu anayo nafasi ya kumshauri Rais wake. Na kwa vyovyote vile Rais akitaka kufanya jambo lolote mtu wa karibu anayeshauriana naye ni Waziri Mkuu na makamu wa rais basi. Kwa hiyo Pinda huwa anashindwaje kumwambia Kikwete kwamba hiki no na hiki yes, kama kweli Pinda mwenye ni mzalendo kwa Taifa? Hawa wote uwezo wao unalingana. Hakuna mwenye nafuu hapa.
   
 12. k

  kluvert Member

  #12
  Jul 27, 2011
  Joined: Jul 26, 2011
  Messages: 71
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 15
  licha ya kuwa ni mzigo,pia ni mnafiki amejifanya kukataa gali mpya v8 uku msafala wake unajaa magali ayoayo
   
 13. P

  Paul S.S Verified User

  #13
  Jul 27, 2011
  Joined: Aug 27, 2009
  Messages: 5,933
  Likes Received: 276
  Trophy Points: 180
  Mkuu Tz ya sasa kuna siri? uliza akina mwanahalisi unao waamini wanatoa wapi taarifa za ndani? akina Slaa, akina Mama Shelukindo nk anyway tuyaache
  Hivi mashauri si anashauri tu kisha kazi inabaki kwa mshauriwa kufuata au kupuuzia. Mkuu si mtetei Pinda kivile lakini System inalazimisha kuwa vile, na kiukweli Pinda ha fit kabisa kufanya kazi na JK maana "si miongoni mwao", Amezungukwa na wanamtandao ambao JK mwenyewe hasemi kitu kwao, sembuse yeye.
  Na kikubwa kinachoonekana kumuangusha pindi ni pamoja na maswali ya papo kwa papo anayoulizwa ambayo ni uvundo wa maswahiba wa JK, mengi yamefanyika nyuma ya pazia sasa anapotakiwa kutoa tamko kama Serikali anajaribu sana kutokujibu asiyoyajua
   
 14. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #14
  Jul 27, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Naona tunakwenda sawa. Pinda alishakuwa na JK, kwa hakika alikuwa anajua ni kiasi gani JK ni mzigo kufanya naye kazi. Kwanini alikubali tena kurudi hata baada ya kubembelezwa? Maana unasema alikuwa anakataa, ilikuwaje baadaye aje akubali? Maana kwa hakika anayeonekana bogus hivi sasa ni yeye. Anakuwaje waziri mkuu katika serikali ambayo hana uwezo wa kutoa tamko wala maamuzi yoyote yanayoihusu? Sasa ana tofauti gani na Makamu wa Rais? Ukiachilia mbali maswali ya papo kwa papo, Pinda ameonyesha udhaifu mkubwa hata katika harakati za kupinga matumizi mabaya ya pesa za serikali. Ni siku nyingi Pinda amekuwa akilalamikia matumizi makubwa ya serikali. Je alishawahi kuwaonya au kutoa order kwa watendaji wake wapunguze hiiki au kile? Alichokifanya ni kukataa shangingi na bado akakubali apewe mwingine. Sasa kwa huyo mwingine halitatumia mafuta? Pinda no bwana!!!
   
 15. J

  JACADUOGO2. JF-Expert Member

  #15
  Jul 27, 2011
  Joined: Dec 13, 2010
  Messages: 930
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Tatizo Pinda ana kichwa kikubwa mno na vile vile sura yake pia ni mbaya sana kwa hiyo anaposimama kuongea mbele ya watu anaongea haraka haraka akihisi watu watamcheka kwa sababu ya ukubwa wa kichwa chake na sura yake ndiyo maana aliamua kujiita mtoto wa mkulima!
  Ila kiukweli kabisa watanzania hatuma waziri mkuu wala rais. Wote ni mizigo kwa taifa!
   
 16. Chimunguru

  Chimunguru JF-Expert Member

  #16
  Jul 27, 2011
  Joined: May 3, 2009
  Messages: 9,843
  Likes Received: 270
  Trophy Points: 180
  serikali yote na wabunge wote wa ccm ni mzigo uliotweta maji!
   
 17. Desteo

  Desteo JF-Expert Member

  #17
  Jul 27, 2011
  Joined: Jul 27, 2011
  Messages: 448
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 35
  Pinda naweza mtetea. Ila huyu shosti akitoka mtwara utasikia yuko mawinguni. Huyo ndio tatizo. Kazi yake uzinduzi, safari na kuomba tu. Zikija hoja ngumu anasingizia nature.
   
 18. K

  KALABASH JF-Expert Member

  #18
  Jul 28, 2011
  Joined: Jan 26, 2011
  Messages: 465
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 35
  Well spoken! Hii inashabihiana na thread niliyoandika hapa wiki chache zilizopita yenye kusema: "Tanzania kuna rais wa kucheka cheka na waziri mkuu wa kulialia"
   
 19. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #19
  Jul 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Mkuu, huku mimi simo. Ni vizuri tujenge hoja badala ya kudescribe physical features za mtu. Kwa kufanya haya tunaweza kujikuta tunawalaani hata vilema. Sura na morphology ya mtu hata siku moja huwa haina reflection ya akili na uwezo wake wa kufanya mambo. Huku nafikiri umepotea mkuu. I am sorry kama nitakukwaza kwa namna yoyote.
   
 20. Lukolo

  Lukolo JF-Expert Member

  #20
  Jul 28, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 5,137
  Likes Received: 76
  Trophy Points: 145
  Lakini Pinda anayo nafasi ya kumwambia rais wake "this is enough" tulia tujenge nchi. Kama anashindwa kufanya hayo basi na yeye ana shida. Na ndipo ninaposema hana uwezo wa kuwa waziri mkuu.
   
Loading...