Dingswayo
JF-Expert Member
- May 26, 2009
- 4,019
- 2,923
Waziri Mkuu Pinda alinukuliwa katika vyombo vya habari kuwa serikali ilikuwa imekosea katika suala la gesi kwa sababu hawakutoa taarifa kamili kwa wananchi wa Mtwara kuhusu matumizi ya gesi. katika taarifa ya habari ya ITV, ameonekana akisema kuwa matukio ya Mtwara ni kutokana na uchochezi wa watu kadhaa. Taarifa yake hii inatoa kauli ambazo zinapishana, kwa vile kama serikali ilikosea na wakasema hivyo, hakuna haja ya kutupa lawama kwa wengine. Inashangaza ni jinsi gani serikali hii inataka kuonyesha kuwa kila mara iko sawa katika maamuzi hata kama sivyo.
Taarifa aliyoitoa Waziri Mkuu Pinda kwenye vyombo vya habari amepotosha uma kwa makusudi. Pinda ameenda Mtwara kusikiliza madai ya wana Mtwara,katika madai yaliowasilishwa na makundi mbali mbali hakuna hoja hata moja iliyojibiwa bali ni usanii uliendelezwa kama kawaida kwa mawaziri wake kuelezea mambo kwa mdomo bila vitendo.
Mh. Pinda ameleza vyombo vya habari kuwa amefanya mazungumzo na wananchi wa Mtwara na wamefikia maridhiano. Suala hilo si kweli Mh. Pinda amazungumza na makundi mbali mbali ya wawakilshi kwa wananchi hivyo kama ni kweli wale ni wawakilishi waliotumwa na wananchi inapaswa hao wawakilishi waende sasa kwa wananchi watoe taarifa/wawaeleweshe juu ya hayo mazunguzo kisha wananchi waamue/wapime hayo mazuri walioelezewa na Mh. Pinda. Alichokifanya Mh. Pinda ni kwamba anahalalisha kuwa madai yale sio ya Wananchi bali ni ya Wawakilishi wa makundi mbalimbali ya kijamii.
Kilichoshangaza kwenye serikali hii juu ya sakata hili ni kuwa wakati Mh. Pinda anazungumza na wawakilishi wa makundi mbalimbali huko Mtwara, kwa upande wa wizara yenye dhamana ya masuala ya Gas Waziri Prof. Muhongo anazungumza kwa kejeli kwenye kipindi cha nipashe Radio One na jioni yake Naibu Waziri Simbachawene (Kipindi cha Dakika 45 ITV) anawatisha wananchi kuwa ikiwezekana nguvu ya dola itatumika kupeleka Gas Dar.
Suala la Gas Mtwara ndio kwanza linaanza kwa mchezo mchafu serikali inaoufanya. Mh. Pinda kwenye mkutano ule ulijichanganya ukasema "Wananchi hawakueleweshwa vyema kwamba Kiwanda cha kusafishia GAS kitajengwa Madiba -Mtwara " ,Hapo ni kama uliwatusi tena wana Mtwara, Mh. Jk bosi wa Pinda alitamka wazi kiwanda kitajengwa kinyerezi na ndipo uzinduzi na sherehe ilifanyika. Kwa hiyo hilo la kujenga plant ya kusindika na kusafisha Gas Mtwara ni jipya.
Kwenye RCC ya Mtwara mwaka jana ,yalifikiwa maamuzi kuwa makao makuu ya TPDC yajengwe Mtwara hilo hujalizungumzia kwa kuwa unajiua fika Gas itapelekwa Dar/Bagamoyo so makao makuu yatakua huko huko.
Serikali ya JK imefanya usanii kwenye mengi sana ila kwa hili serikali isikurupuke kucheza na vyombo vya habari kupotosha uma ili wana Mtwara waonekane wabinafsi/wapuuzi. Kumbuka watu walioongea na waziri Mkuu Pinda kwa minajili ya kufikisha ujumbe kwa wananchi waliisii Serikali wasitishe kwanza mpango wao wa kupeleka Gas kwani mradi wenyewe umeonyesha una utata. Makundi hayo Maaskofu/wachungaji,Maimamu/Mashekh,Wafanyabiashara,WanaCCM(kamati ya Ushauri ya Mkoa) ,Wenyeviti wa Vijiji na Madiwani,Wawakilishi wa asasi za kirai na Viongozi waandamizi wa serikali pamoja na vyama vya upinzani. Makundi haya sio ya kupuuzwa kwa wewe kujitapa kuwa umepata suluhu ili hali hawajapeleka mrejesho.
Hili swala likilazimishwa litaleta madhara makubwa kwani wananchi Mtwara wanasema wazi kuwa makubaliano yale kama yalifanywa wao hawayatambui kwani hayajawafikia. Migogoro ya namna hii ikipuuzwa huwa ni sumu kwa maendeleo ya nchi na ustawi wa utawala bora.
Subira huvuta heri na pia Uhondo wa ngoma ingia ucheze. Prof. Muhongo alisema wana Mtwara wanacheza ngoma wasioijua akasahau ngoma nyingi za asili zinapatikana kusini na ni jadi yao(Ngoma ni utajiri wa wanakusini-Rejea Makuya festival).
Mungu ibariki Tanzania.