Nimewahi ku-comment humu kuwa Pinda kawekwa pale kwenye ile nafasi na mr. Dhaifu kwa maslahi fulani. Kwa kujua au kutokujua anatumika kama kipoozeo hali ya joto inapoongezeka. Nimewapenda wabunge waliokuwemo bungeni leo kwa jinsi walivyomzomea baada ya kauli yake ya eti, busara itumike katikka kuwajadili wezi.
Rai yangu kwake ni kuwa arudishe ofisi ya watu na amwambie dhaifu alete zile epa tuzipangie matumizi.
Ndugai big-up sana kwa hekima zako na ahadi yako kwa umma juu ya mjadala kuendelea kama ulivyoupanga. Kumbuka bunge la katiba lilipelekwa mahakamani likapuuzia na kuendelea na vikao vyake. Je, hali ile imatofautianaje na hii ya sasa?. Pinda acha kupindisha hoja ziache zinyooke na kuwanyoosha wezi. Natamani nimwone ngedere ni nani kati ya wale walioitana.
Bunge likishindwa kuamua tutawaamulia kwenye masanduku ya kura na mtaani.
Busara anayoitaka akaichukue kwa Tunu na si hapo. Aende na mwanasheria wake kuzimu ikibidi.