Pinda: Karibu asilimia Tisini na Tisa (99%) ya Wanzanzibar ni Waislam

Status
Not open for further replies.
sasa kama hivyo ndivyo mbona mwataka kulazimisha wote wafunge? tenganisha dini na matendo ya mtu

Hehehehe, hakuna alolazimishwa kufunga, hakuna aloambiwa kuwa ukila utatiwa jela ama utapigwa fine, katika uislam Kufunga ramadhan ni kama kusali, ni juu yako mwenyewe ukila kwani si moto utapigwa wewe? Kikubwa maimamu wanahamasisha watu kufunga ma kufanya inada kwa wingi na sio kumlazimisha mtu kufunga! Unajua kulazimisha? Kulazimisha jambo ni kama mwanasheria mkuu wenu aliposema kuwa ukikataa sensa jela miezi sita ama fine laki sita, huko ndo kulazimisha
 
Hata kama ni kweli ina maana ukiwa muislam lazima kila mtu awe.kufunga ni imani kula na nguo fupi ni sehemu ya vipimo vya imani.vipi mtu upate thwawab wakati huwezi kuhimili vishawishi.kwa pinda sina la kusema kwani ni siku nyingi akili zimekimbilia kwenye masaburi.

Yatupasa kuheshimu imani ya watu wengine, ili wao waone kuwa sisi ni wapole, na wanyeyekevu, kamaBwana wetu Yesu kristo alivyosema, kama mtu akikunyang'anya kanzu mpe na joho, au akikulazimisha umpeleke kilometa mbila basi mwambie hata tatu nitakupeleka, sioni chakubishania, Mungu ndiye atakaye hukumu, yatupasa kuwa kimya huku tukiwaombea ili Roho wa Mungu awatokee kama alivyo mtokea Paul Hussen wa kigoma aliyekuwa Shekh mkuu wa Africa Mashariki na kati, fungua youtube, tuwasaidie waislam''
 
Huoni wanavyohangaika kuwachomea makanisa yao? Yaani 99% ya population inahangaishwa saaaaaaaaana na just 1%

Sasa itabidi tutafute dictionary la kiswahili, maananaona sijui kutisha vipi ulivokusudia! Hivi shetani akikutisha kama unamuogooa utamsogelea??
 
Yatupasa kuheshimuimani ya watu wengine, ili wao waone kuwa isi ni wapole, na wanyeyekevu, kama bwanwetu yesu kristo alivyosema kama mtu akikunyang'anya kanzu mpe na joho, au akikulazimisha mpeleke kilometa mbila pasi mwambie hata tau nitakupeleka, sioni chakubishania, Mungu ndiye atakaye hukumu, yatupasa kuwa kimya huku tukiwaombea ili Roho wa Mungu awatokee kama alivyo mtokea Paul Hussen wa kigoma aliyekuwa Shekh mkuu wa Africa Mashariki na kati,nenda youtube, tuwasaidie waislam''

Haswaaaa, tunatakiwa tuwe wanyenyekevu vile vile, tena na sisi tunaambiwa tuwe karibu na wakiristo ili tuwasaidie kama tulivomsaidi Sheikh MaZinge
 
Hii inawafurahisha watu kusikia 99% hata kama hizi taarifa si sahihi, but angesema wapo 50% ungesikia kelele za upande mwingine. Muhimu kujifunza hii 99% imewasaidiaje ktk maisha ya kiroho na kimwili ndo mambo ya msingi.

Na hawa waliotangaza kugoma kuhesabiwa pinda angewafurahisha pia kwa kuwaambia wapo 88% ya watanganyika wote mi nadhani ndo wangeweza kuonekana mawazo yao ya kifukara nini wanataka kufanya baada ya kuwa wamejua idadi yao.
 
Nilikaa Zanzibar miaka 4 iliyopita hakika hakuna kipindi kigumu kama hichi na Waziri mkuu ameonesha upungufu mkubwa sana katika kujibu swala hilo. Mimi huwa nasema waziri mkuu ni mnafiki sana.
 
Simba mnyama Zanzibar inawaisilamu 99% hilo halina ubishi na vile vile waliweka sheria ya kutovaa nguo fupi au kula nje mwezi wa ramadhani. Tatizo huwa hatuangalii haki ya nchi yao ila ubinafsi wetu kwasababu hazilingani na dini nyingine.

Haina maana kudharauliana katika dini kwani dini ni imani na kama imani zikitofautiana sio kumdharau mtu ila kujenga heshima miongoni mwetu. Mimi ninavoijua Zanzibar ni kwamba inazo itikadi zake na hivo tuziheshimu na tusilazimishe vitu vitakavokwenda kinyume na dini au utamaduni wao ili kuilinda historia yao.

Nadhani wanapenda zaidi kuzilinda historia zao na ni kitu kibora zaidi kuliko na ndio kivutio kimojawapo kwa watalii.Kwani watalii wanapenda nchi zenye kutunza historia.
 
Tuache upotoshaji. kauli ya mh. Msigwa sio kauli ya CHADEMA. Mh.. Msigwa sijui kama anayaelewa mazingira ya Zanzibar na hata yale ya Mafia. Na sina uhakika kama Mh msigwa anaishi na wakristo tu huko Iringa. Mh Msigwa asijaribu kuwagombanisha watu wa dini mbalimbali kule Zanzibar. Tangazo hilo limetolewa bila shaka kuwapa taarifa watu wageni wa taratibu za mwezi wa Ramadhani kama kina Msigwa. Kwa wenyeji wa dini zote Zanzibar hili sio geni na wala haliwapi shida.

Sina uhakika na kiwango chako cha kufikiria!! Hivi hoteli kuzuiliwa kupika chakula cha mchana kwako ni sawa tu kwa sababu waislamu wamefunga! Hiyo si ni sawa na kufukuza wageni ambao wengi wao ni watalii? Hizi tunaziita imani za kushikiliwa.
 
Zanzibar inawaisilamu 99% hilo halina ubishi na vile vile waliweka sheria ya kutovaa nguo fupi au kula nje mwezi wa ramadhani.Tatizo huwa hatuangalii haki ya nchi yao ila ubinafsi wetu kwasababu hazilingani na dini nyingine.Haina maana kudharauliana katika dini kwani dini ni imani na kama imani zikitofautiana sio kumdharau mtu ila kujenga heshima miongoni mwetu.Mimi ninavoijua Zanzibar ni kwamba inazo itikadi zake na hivo tuziheshimu na tusilazimishe vitu vitakavokwenda kinyume na dini au utamaduni wao ili kuilinda historia yao.Nadhani wanapenda zaidi kuzilinda historia zao na ni kitu kibora zaidi kuliko na ndio kivutio kimojawapo kwa watalii.Kwani watalii wanapenda nchi zenye kutunza historia.
Niambie sheria hiyo inaitwaje na ninaweza kuisoma wapi?
 
Niambie sheria hiyo inaitwaje na ninaweza kuisoma wapi?

Sina cmputer ya uhakika lakini kama utaweza kui-google historia ya Zanzibar na kama utaitafuta kwa nia njema basi utaipata.

Kwasababu sina au siwezi kusema jina la sheria lakini kitu ninachokumbuka niliwahi kusoma ktk internate kuhusu sheikh Abeid Karume jinsi alivoweka sheria kwa watalii wakiingia uwanja wa ndege watalii wapewe kanga au mitandio na wasivae nguo fupi.

Na mwezi wa ramadhani haruhusiwi mtu kufungua hoteli au mtu kula hovyo njiani na akikamatwa huchukuliwa hatua.
 
Pamoja na waziri mkuu kujibu swali la mbunge wa Iringa mjini leo asubuhi juu ya
matamshi ya waziri wa sheria na katiba wa zanzibar kuzuia Hotel zote zifungwe wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani na hata kuchukuliwa hatua hatua kwa mtu yeyote atakayeonekana anakula mchana zanzibar ni kitendo kisicho vumilika naasikitika kupingana na hoja hii kiimani kwani binafsi si muumini sana miongoni mwa wanao amini zaidi ya mapokeo ya kifamilia na kijamii.

Kitendo cha serikali kukubali kuwa hoja iliyotolewa na waziri zanzibar juu ya mwezi huu mtukufu unatutoa kwenye hatua moja ya kimaisha hadi hatua nyingine kwani nataraji siku moja kusikia wakristo nao wakidai kuwa kipindi cha kwaresima hotel zote zifungwe na atakayeonekana anakula mchana wakati wa kwaresima basi achuliwe hatua kali za kisheria (ipi?) kula mchana.

Hoja zangu za msingi hapa ni hizi zifuatazo
1. serikali haina Dini?
2.zanzibar ni nchi au siyo nchi
3.Zanzibar imo ndani ya muungano au nje ya muungano?
4.jibu lolote la swali la kwanza hapo juu jee mambo ya Dini ni mambo ya muungano au la?
5.Sensa ya kuwa Zanzibar ina idadi kubwa ya waislamu ilifanyika mwaka gani na takwimu zikoje?
6.wanaodai kipengele cha Dini kiwemo kwenye Dodoso la sensa mwaka huu wapo sahihi au hawapo sahihi?

Mwisho lakini si kwa umuhimu yeyote atakaye changia hoja hii ahakikishe aliangalia kipindi cha maswali na majibu ya papo kwa hapo ya waziri mkuu leo asubuhi kwa kurejea swali lililouzwa na Mh Msigwa.
karibuni sana!
 
Waziri Mkuu kadanganya Bunge, athibitishe kama kweli Waislam Zanzibar ni 99%. In any case hata 1% si wana haki? Mbona Mikoa yenye Wakristu wengi hawabani wengine wakati wa Kwaresma

Toka nizaliwe sijawahi kumuona mtu aliyefunga kwaresma seriously ........ majority huwa wanasema kuwa, kama unakunywa laga kreti moja nzima inatakiwa upunguze unywe labda laga 18 hivi. Na kama mtu huwezi kujistiri au kujizuia kula hadharani PIGA MBIZI hadi dar uamishie makazi yako huku.
 
level of significance 0.05 and confidence interval 95%, since p>significance level, then accept the null hypothesis

Kama wewe ni mkuu wa chuo basi kazi ipo. ikiwa level of significant ni 0.05 na ukapata p value ya 0.2 ina maana huna evidence za kwenda kinyume na null hypothesis, hivyo kile kinachoaminika kuwa sahihi kitaendelea kubakia kama kilivyo. pia kuna discussion kwa mastatistician juu ya kukubalika/.kutokubalika kusema una accept null hypothesis.
 
Toka nizaliwe sijawahi kumuona mtu aliyefunga kwaresma seriously ........ majority huwa wanasema kuwa, kama unakunywa laga kreti moja nzima inatakiwa upunguze unywe labda laga 18 hivi. Na kama mtu huwezi kujistiri au kujizuia kula hadharani PIGA MBIZI hadi dar uamishie makazi yako huku.
Huoni huyo ana afadhali? wewe si umebadilisha tu masaa ya kula! tena kiuhalisia utakuwa unakula zaidi ya siku za kawaida kama ulivyozoea.
 
mimi ni mmoja wa ambao hawana ndio maana najisikia niko huru kwani hata nikichangia huwa siwezi kuegemea upande wowoyepili siwezi kugombana kwa tamaduni za watu ninawaacha watumwa wa fikra na kitamaduni walumbane na sasa wanakaribia kuivuruga nchi.
Ila nchi itakapovurugika unaweza usiwe huru kama unavyofikiri sasa.
 
Huoni huyo ana afadhali? wewe si umebadilisha tu masaa ya kula! tena kiuhalisia utakuwa unakula zaidi ya siku za kawaida kama ulivyozoea.

Haya makelele mnapiga humu JF ni buree tu, Wazanzibari wakristo wanajihifadhi kama waislam as part ya utamaduni wa Mzanzibari. We endelea kupiga kelele tu.
 
Swala hili limeibuka baada ya waziri mmoja wa serikali ya mapiduzi zanzibar kutangaza kuwa, ni marufuku kwa wafanya biashara ya vyakula kuuza vyakula wakati wa mchana ktk kipindi hiki cha mfungo wa ramadhani. Hii ikiwa na mantiki kuwa ni shurti kila mtu afunge. Je, ni sawa kwa kiongozi wa serikali ya nchi isiyokuwa na dini kuutangazia umma jambo kama hili.
Zaidi ya hapo suala hili limeibuka huko bungeni leo, ktk kipindi cha maswali ya papo kwa papo kwa mh. Pm, Pm akajibu kuwa znz zaidi ya waznz 99% ni waislamu, hivyo ni muhimu wa znz wakatii agizo hilo. Je, Kuwa na zaidi ya 50% ya wakazi ktk eneo moja la TZ inahalalisha eneo hilo kuongozwa kwa kanuni za kidini?.
 
Haya makelele mnapiga humu JF ni buree tu, Wazanzibari wakristo wanajihifadhi kama waislam as part ya utamaduni wa Mzanzibari. We endelea kupiga kelele tu.
Kama wanajihifadhi kama waislam, hii amri imetoka wapi sasa? common sense inaniambia kama wangekuwa wanajihifadhi kama waislam hii amri isingekuwapo. Hivi kujihifadhi kama waislam nayo ni utamaduni wa Zanzibar? Ba...
 
SI HAKI KUWAAMBIA WAZAZIBAR WASIO WAISLAM WASIFANYE BIASHARA KAMA UNAFUNGA NI WAO MBONA WAKRSTO WAKFUNGA HAWAFUNGI BIASHARA ZAO BARA Eg; KARIAKO NYIE KINA MWIBA BWANA IMANI ZENU ZISIVURUGE UTAMADUNI WA WATU ALAFU MBONA KILA KITU MNATAJA DINI YENU HIVI HAMUWEZ KUJENGA HOJA ZA MSINGI KILA KITU ADUI WA UISLAM FANYEN KAZI ACHEN CHOCHOKO
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom