Pinda: Karibu asilimia Tisini na Tisa (99%) ya Wanzanzibar ni Waislam

Status
Not open for further replies.
Maelezo hayo hapo chini yametolewa na Mch Msigwa kwenye FB yake. Ni ukweli, wazanzibari wanalazimisha watu kufunga. Ndugu zangu waislamu tuelewe, kufunga ni ibada kati ya binadamu na Mola wake. Sasa kwanini mnalazimisha watu wasio waislam au waislam wasiotaka kufungu wafunge? Ua uislam ni udikteta? Ukristo haulazimishi mtu kuishi kikristo maana imani ndio muhimu zaidi kuliko matendo:

"Siku ya ijumaa ya tarehe 20.7.2012 waziri wa Sheria na katiba mh. Abubakary Khamis alihutubia taifa la Zanzibar kupitia vyombo ya ZBc-TV na ZBc radio ,akiwataka wananchi wote wanoishi Zanzibar ,kuheshimu mfungo wa ramadhani ,na Alitoa maelekezo kwa vyombo vya dola, kuwa kamata wale wote watakaokutwa wanakula mchana. Kwa kile alichokiita kuwashawishi waliofunga. Pia alipiga marufuku migahawa yote kufunguliwa na kutoa huduma ya chakula na chai kwa wateja wakati wa asubuhi na mchana, isipokuwa usiku tu, Kama vile Hitoshi waziri huyu aliviagiza vyombo vya dola, kuwa kamata wale wote watakaovaa nguo fupi, hasa wanawake za kuwatamanisha wanaume. Katiba ya ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania inasema Kila mtu anayohaki ya kuamini dini anayotaka ,na swala la katiba ni la muungano ,katika Majibu yake waziri mkuu alinishitua sana kwa kile alichodai Zanzibar kuna waislamu wengi hivyo tamko Hilo ni halali japo ni kuikanyaga katiba, na kwa Bahati mbaya radio nyingi za dini ya kiislamu zimenishambulia na kukimbilia swala la nguo fupi,baadala ya hoja ya msingi ya Uhuru wa kuabudu ,mwislamu akiwa mmoja katika kundi la wakristo 1000 lazima haki yake ya kiimani ilindwe na kuheshimiwa,hivyo hivyo kwa mkristo,tusijaribu kupotoshwa na watu wasiotaka kufikiri,waziri mkuu amelipotosha taifa.baadala ya kutukana na jaziba jibu hoja ya kikatiba,Mbona tanga,mtwara ,lindi ambako kuna waislamu wengi amri hiyo haijatolewa, double standard............"
 
Hio sasa sio Dini tena ni Siasa, why ulazimishe watu kufunga? Hivi ni watu gani wasiotambua uwepo wa watu wa imani tofauti? Huu ni ukatili uliopitiliza na Kamwe haukubaliki
 
Na Pia wameanzisha Jeshi la kuwalinda WATALII; Kwanini Jeshi?
 
Watalii huku zenji mbona wanakula hadharani? Mtoto wa Peasant alichemka kwa majibu aliyatoa bungeni na pia huyu Waziri wa huku zenji na yeye alichemka pia.

Hivi hii CCM itakufa lini?
 
Nimejaribu kupitia hilo agizo la huyo Waziri wa Sheria lakini nimeshindwa kuona paliposema kwamba Wakristo wamezuiwa kula mchana au Wakristo wamezuiwa kuvaa nguo fupi!!! Hivi mtu akisema "kamata wale wote wanaokula mchana" ndo amesema "kamata wale wote Wakristo wanaokula mchana?" Kwani hakuna waislamu wasiofunga? Kwani hakuna waislamu wasiovaa ngup fupi Kwanini wewe na huyo Msigwa muone hilo agizo linawalenga Wakristo?! Hakika hii ni aibu....labda angelalamika kwamba kwanini kuwalazimisha wasiofunga wasiwe na uhuru wa kula mchana hapo ningeelewa hoja ya Msigwa lakini kinyume chake ni kukuza mambo!!

All in all....si kweli hata kidogo kwamba watu wanakatazwa kula mchana! Huo ni upotoshaji wa hali ya juu ambao kama kweli Msigwa alisema hivyo basi hana budi kukionea aibu kitendo hicho. Mara nyingi agizo kama hilo huwa linakataza kula hadharani mchana wa Ramadhani! Hivi hakuna tofauti hapo kati ya kukataza kula mchana na kukataza kula hadharani mchana wa Ramadhani?!
 
kwani si mlisema smz muamsho? sasa cha ajabu kipi? mara ngapi katiba inakiukwa kwa malengo ya kisiasa kote upinzani na watawala hamsemi kitu, mnatulazimisha tuamini mpo kidini na inakuumeni kuliko utamaduni wa wale jamaa.
 
Mbona CHADEMA mnashikia bango sana?

Sio CHADEMA kumbuka Zanzibar kuna Minorities wanaishi huko; USA hawasemi kuwa Christmas Kila Mtu aende Kanisani

Asieenda Kanisani siku hiyo atakiona; Zanzibar lazima wawaheshimu minorities Sio wakristo tu; kuna Hindu, Pagan pia

Dubai nimeishi huko Restaurant wanafungua, hata Saud Arabia kuna zinazofunguliwa; KWANINI ZANZIBAR...
 
Hio sasa sio Dini tena ni Siasa, why ulazimishe watu kufunga? Hivi ni watu gani wasiotambua uwepo wa watu wa imani tofauti? Huu ni ukatili uliopitiliza na Kamwe haukubaliki

Kwani kuna Mtu aliitwa kuja Zanzibar au ni njaa yake ndio iliyomfanya aje kuishi katika mazingira ya aina hii mbona wakristo wa kizanzibar miaka yote hiyo haikuwa tatizo kwao iwe leo haya makanisa ya vichochoroni
 
HIZI NDIZO HASARA ZA KUTOSHIRIKISHA UBONGO MDOMO UNAPOONGEA,kweli haki haitendeki na wanadhani ndio kutuonesha hawataki muungano kumbe no connection,hata tukivunja muungano ukristo hautavunjika na haki zao ni lazima wapate..huu ni ujinga na Mungu gani anayependa ujinga huo..shame on them:spy:
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom