Pinda kama Makamba, kila anapotoa kauli anaboronga

BAK

JF-Expert Member
Feb 11, 2007
124,790
288,109
Pinda azua balaa Mwanza
SAKATA LA UWANJA WA NYAMAGANA

na Deus Bugaywa, Mwanza
Tanzania Daima~Sauti ya Watu

HATUA ya Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, kuunga mkono mabadiliko ya matumizi ya Uwanja wa Nyamagana, imezua mjadala mkali jijini hapa, ambapo baadhi yao wamefikia hatua ya kusema, wameanza kukosa imani naye.

Wakizungumza kwa nyakati tofauti jana, wakazi wa jiji hili, wameonyesha kusikitishwa na Pinda aliyeonekana kukubali mabadiliko ya matumizi ya uwanja huo wa michezo.

Juma Hemed, mkazi wa Nyamanoro jijini hapa, amesema baada ya kusikia majibu ya Waziri Mkuu Pinda bungeni, wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo juzi, ameanza kukosa imani na waziri huyo ambaye uteuzi wake uliungwa mkono na wengi.

“Siku ile ya kwanza kujibu maswali, Spika alisema Pinda ameteuliwa na Mungu, lakini kwa hiki anachotaka kufanya, kama kweli ni Mungu, binafsi nina wasi wasi na aina ya Mungu huyo, kwa sababu kwa kiongozi makini huwezi kusema Nyamagana haufai, kwani umuhimu wake tunaujua sisi wakazi wa Mwanza,” alisema.

Mwingine aliyeelezea masikitiko yake kuhusiana na kauli ya Pinda, ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka mkoani Mwanza (MZFF), Jumbe Magati, aliyemtaka waziri mkuu kuhisi uchungu wa watu wa Mwanza, abaki kama mbunge na akatoe wazo la kuuza Uwanja wa Nelson Mandela mjini Rukwa ambao uko karibu kabisa na soko, aone kama wananchi watakubali.

Jumbe, alisema huenda waziri mkuu anaujua Uwanja wa Nyamagana, lakini inawezekana haijui Mwanza kwa sababu, viwanja na maeneo yote ya wazi katikati ya jiji hilo yameuzwa na jiji, hivyo Nyamgana ndiyo mkombozi pekee kwa wakazi wa jiji hilo.

“Uwanja wa Nyamagana si tu muhimu kwa michezo, lakini pia ni kimbilio wakati wa majanga, mara nyingi tunaona duniani kote panapotokea matetemeko, mafuriko majanga, lolote lile, watu wanakusanya kwenye viwanja, sisi wakiuza huu tutakwenda wapi?” alisema Magati. Aliongeza kwamba, kitaalamu uwanja huo si mdogo, una uwezo wa kuchukua watu 15, 000 ambayo ni idadi tosha kwa shughuli za michezo kwa Jiji la Mwanza. “Wanachotaka kufanya serikali ni kama mtu amekuja kuposa kwako, akakuta binti zako, lakini pia yuko mama yako ambaye ana afya njema na ni mzuri, badala ya kuposa binti yako, mleta posa huyo akataka kuposa mama yako. “Nyamagana ni kama mama yetu, kuubadilishia matumizi ni kutaka kuposa mama yetu badala ya binti zetu,” alisema Jumbe.

Mkazi mwingine aliyezungumzia suala hilo, ni Maduhu James, aliyesema kuwa Pinda anatakiwa awe makini sana katika kauli zake, kwani zingine zinawatia mashaka wananchi kama imani waliyokuwa nayo kwake kuwa ni kiongozi shupavu na mwadilifu ni sahihi kiasi gani.

“Waziri mkuu wetu awe makini anapounga mkono hoja ambayo kila mkazi wa Mwanza anajua ina mambo mengi yaliyojificha, anatuacha njia panda, au anataka tuamini kwamba na yeye ni wale wale?” alihoji James.

Aliongeza, kwa ujumla waziri mkuu ameonyesha kukubaliana na wazo la kubadili matumizi ya uwanja, lakini hakutaka kwenda moja kwa moja.

“Tunamshauri Pinda huko alikochagua siko, watu wanajua nini kinaendelea pale jijini na kwa nini wanashinikiza wauze, kama na yeye anajiunga nao, hatuwezi kushangaa sana maana hii ndiyo Tanzania, lolote linawezekana,” alisema mkazi huyo.

Mkazi mwingine aliyejitambulisha kwa jina moja la Mwanahawa, alisema kama Nyamagana ni pafinyu kwa mpira, iweje patoshe kwa biashara? Na kama ni suala la ufinyu, umesababishwa na jiji wenyewe na akaongeza kuwa hata jiji wanaposema kuwa wataweka michezo ya ndani si kweli.

“Wewe (mwandishi) si unaijua sehemu inayohusika na michezo ya ndani kwamba ni Community Center, hebu nenda huko leo ukaone, kule kote wamejaza maduka halafu leo wanatuambia habari za michezo ya ndani, hiyo ni danganya toto, lazima uwanja wetu ubaki na kesho (leo) tunaandamana mpaka kieleweke,” alisema kwa jazba.

Yote hayo yametokana na kauli ya Pinda aliyotoa juzi bungeni wakati akijibu swali la Mbunge wa Misungwi, Jacob Shibiliti, wakati wa kipindi cha maswali ya papo kwa papo bungeni, kwamba kwa maoni yake anadhani Uwanja wa Nyamagana umechakaa na ni mdogo, hivyo ingefaa ubadilishiwe matumizi, ingawa suala hilo aliliaccha mikononi mwa wakazi wenyewe wa Mwanza.

Uwanja huo ndio uwanja pekee wa serikali, unaomilikiwa na halmashauri ya Jiji la Mwanza, ukiondoa wa CCM Kirumba unaomilikiwa na CCM.

Wakati hali ikiwa hivyo, wananchi wa jijini hapa, leo wameandaa maandamano makubwa ya kupinga kubadilishwa kwa matumizi ya uwanja huo, yatakayoanzia na kuishia katika uwanja huo kupitia mitaa mbali mbali ya jiji na kupokewa na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Dk. James Msekela.

Wakati wakazi wa Mwanza wakiwa na msimamo huo, Shirikisho la Soka Tanzania (TFF), jana lilitoa taarifa kuunga mkono juhudi za kuhakikisha Uwanja huo wa Nyamagana unabaki kwa shughuli za soka na si vinginevyo.
 
Ukiwa CCM na hata ukisha shika hatamu na utamu unakuwa kama umerogwa .Kama huamini basi haya hapa .Kwanza unakuwa na imani na Pinda kwa lipi ? Alifanya nini akiwa waziri wa kawaida ? Lazima watanzania waamke .Mlikuwa na imani na JK bila kuuliza rekodi yake .Leo yale yale kwa Pinda bila rekodi ? Watanzania nyie nani kawaroga naimani zetu hizi ?
 
Walikuwa wanasubiri Mhe. John Pombe Magufuli aondolewe Wizara ya Ardhi. Chiligati Chiligati umempa Pinda ushauri gani? acha U-CCM kwenye masuala ya jamii. Tatizo ni kupenda vijipesa tu. Ndiyo maana miliuza hata maeneo ya mnazi mmoja Dar, Makaburi ya boma (Ilala). Mshindwe kabisa...
 
Kwa waliosikia majibu ya Pinda jana kwenye hoja ya kumshitaki Mkapa sidhani kama wanashangaa kwa hili pia. Huyu Pinda anatia huruma sasa.
 
Tatizo moja anadhani bado ni waziri anaesubiria tamko toka kwa EL hilo ndio tatizo lake.....hajui kuwa yeye anatakiwa atoe tamko la mwisho sio asubiri asaidiwe na PM.....hana msimamo na maamuzi yake....anatakiwa ajifunze kwa lolote lile awe ameshalifanyia maamuzi kabla..anasubiri afuatwe ndio aanze kufikiriaa...atalijua joto jiwe nini maana ya PM
 
Wakuu,

Uongozi mgumu sana, hasa kwenye hii dunia ya utandawazi na JF kufuatilia kila neno linalosemwa.

Ni ni muhimu kuwa na viongozi wenye visions ambao wako tayari kuitekeleza hata kama watazomewa na kila mtu. Baada ya muda inaweza kuja onekana walikuwa right.
 
Mtanzania hivi wewe ulitegemea huyu Pinda afanyeje na kwa rekodi ipi ? Alikokuwa kama waziri alifanya nini ? Maana watu wamekula sana na yeye akawa kimya .
 
Mtanzania hivi wewe ulitegemea huyu Pinda afanyeje na kwa rekodi ipi ? Alikokuwa kama waziri alifanya nini ? Maana watu wamekula sana na yeye akawa kimya .

Lunyungu,

Nakubaliana na wewe kuhusu utendaji wa Pinda kule alikotoka. Pia mimi sitegemei afanye maajabu baada ya kuwa PM.

Ila pia sitamlaumu kwa kuchukua maamuzi magumu maana uongozi ni kuhusu conflicting arguments, kama kiongozi inatakiwa uamue upande mmoja. Sio kitu rahisi kabisa.
 
Lunyungu,

Nakubaliana na wewe kuhusu utendaji wa Pinda kule alikotoka. Pia mimi sitegemei afanye maajabu baada ya kuwa PM.

Ila pia sitamlaumu kwa kuchukua maamuzi magumu maana uongozi ni kuhusu conflicting arguments, kama kiongozi inatakiwa uamue upande mmoja. Sio kitu rahisi kabisa.

Mtanzania,

Tatizo la pinda sio kuchukua maamuzi mazito, tatizo lake ni kutoa matamko ambayo baadaye analaumu vyombo vya habari kuwa havikumuelewa. Usishangae kesho ofisi yake ikatoa tamko kulaumu vyombo vya habari kuwa vimemquote vibaya kwenye issue ya nyamagana.

hii issue ya nyamagana imejaa rushwa na ningewashauri viongozi wakuu wa ccm wakakaa mbali nayo au wakajiandaa namna ya kuielezea
 
Mtanzania,

Tatizo la pinda sio kuchukua maamuzi mazito, tatizo lake ni kutoa matamko ambayo baadaye analaumu vyombo vya habari kuwa havikumuelewa. Usishangae kesho ofisi yake ikatoa tamko kulaumu vyombo vya habari kuwa vimemquote vibaya kwenye issue ya nyamagana.

hii issue ya nyamagana imejaa rushwa na ningewashauri viongozi wakuu wa ccm wakakaa mbali nayo au wakajiandaa namna ya kuielezea

Mwafrika wa Kike,

Hii habari sijaisoma yote ila naona ni kama Richmond tu.

Watanzania tuna kazi kweli, sijui nani atatuokoa!

Nchi imeoza kuanzia kwenye shina mpaka Ikulu.
 
Mwafrika wa Kike,

Hii habari sijaisoma yote ila naona ni kama Richmond tu.

Watanzania tuna kazi kweli, sijui nani atatuokoa!

Nchi imeoza kuanzia kwenye shina mpaka Ikulu.

Mimi ningeshauri Mzee wetu Pinda apunguze kutoa matamko bungeni kwa sasa. Na kwa sababu Tanzania uongozi wetu sio wa bunge na waziri mkuu kama UK, sidhani kama ni lazima atoe majibu bungeni.

Yeye awaachie mawaziri wanaoboronga wakaangwe na wabunge na wala asiitishe vikao vya kuwaweka sawa wabunge kama Lowasa na hiyo serikali yake itakuwa na unafuu kidogo.
 
Back
Top Bottom